Kabla hujamdhihaki mtu kasome maandiko matakatifu ujifunze vizuri. Mfano kaangalie wale mitume walikotokea. Pia mtazame mtu Kama Paulo alikotokea. Kwangu sioni ajabu kwani Mungu ana njia zake ambazo wewe mwanadamu huwezi muelewa Kama hupo karibu naye. Pia utumishi kwa Mungu upo wa namna nyingi sana hata huko serikalini unaweza ukakuta aliwekwa na Mungu kumtumikia kwenye nafasi hiyo. Nimeshuhudia kwangu mwenyewe hata kwa mke wangu Kuna taasisi alituweka kwa maelekezo yake mwenyewe akitutaka tufanye kazi Fulani kwenye ile taasisi.