SIHA :- MWANRI AWA MUINJILISTI
Aliyepata kuwa mtumishi wa Serikali akihudumu katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo ya Unaibu Waziri na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri (Pichani: Katikati) amethibitisha kuingia rasmi katika utumishi wa Mungu kama Mwinjilisti katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).
Uthibitisho huo umekuja siku chache baada ya kusambaa kwa uvumi katika mitandao ya kijamii kwamba Mkuu huyo wa Mkoa Mstaafu Aggrey Mwanri ameanzisha kanisa.
Habari hiyo ilisambaa kwa wingi na kasi mitandaoni ukimwonyesha Mwanri akiubiri huku akiwa amevalia joho la utumishi wa kiroho ndani ya moja ya kanisa katika wilaya Siha mkoa wa Kilimanjaro
Katika kuondoa utata huo na kuweka bayana kinachoendelea kwa sasa Mwanri mwenyewe anafanua kwamba alitunukiwa Uinjilisti wa kanisa la KKKT kwa kupata baraka zote za viongozi wa dhehebu hilo
Mkuu wa Mkoa mstaafu Mwanri katika utumishi wake serikalini amekuwa maarufu sana katika matumizi ya misemo mbalimbali ambayo aliitumia kama msisitizo wa jambo wa jambo fulani kwa lengo la kufikisha ujumbe kwa urahisi katika jamii.
Sasa ameingia katika kuwatumikia wananchi kiroho anazungumziaje, Je ataendelea kutumia misemo hiyo katika kufikisha neno la Mungu kwa urahisi kwa waumini?
Licha ya kuwa mkuu wa Mkoa Mwanri amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ambazo ni pamoja na Naibu waziri wa Nchi ofisi ya waziri Mkuu-Tamisemi, Mkuu wa wilaya ya Arusha, mbunge wa Siha na pia Katibu wa Itikadi na uenezi wa taifa wa CCM.
SUKUMANDANI...
https://m.youtube.com/channel/UCUzK7v2L8t7qH0mDQ_7CuWg
Login • Instagram
Kasomi