Hatimaye Aggrey Mwanri awa Mchungaji rasmi. Sasa ukisikia soma hiyoo! Ujue ni somo la Injili

Hatimaye Aggrey Mwanri awa Mchungaji rasmi. Sasa ukisikia soma hiyoo! Ujue ni somo la Injili

๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ hakuna namna itabidi tu niende kanisani kwake
 
Kwa warutheri Hilo joho huvaa wainjilisti ama muhubiri wa siku hiyo. Mwamri alilivaa Sana huko tabora maana alikuwa akihubiri sa sijui Kama kweli ameenda kuwa muinjilisti kabisa
 
Hakika shambani kwa bwana mavuno ni mengi lakini watenda kazi ni wachache.

Heri wamchaao bwana maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Agrey mwaniri sasa ni mpakwa mafuta.

Ni mchungaji aliyeamua kuacha kondoo 99 na kumtafta yule mmoja aliyepotea ili asishambuliwe na mbwa mwitu.

Mavuno ni mengi watenda kazi ni wachache shambani mwa BWANA. Binafsi pia ni mtumishi wa Mungu hivyo nimefurahi sana kusikia mzee wetu amekuja shambani mwa BWANA
 
Anawaandaa watu kuwaelekeza kwa Mungu yupi,au yule yule ambaye anatakiwa kumshukuru magu kwa uongozi mzuri
Umeona eenhh?!!,Huyo jamaa mjinga sana, unless km alitubu hawa kwa kauli zao inawezekana wamesababisha Mungu achukie Hadi kuamua kumtwaa jiwe, maana walisifu na kuabudu kwa kiwango cha juu mno wakasahau Kumpa Mungu Utukufu.
 
Kabla hujamdhihaki mtu kasome maandiko matakatifu ujifunze vizuri. Mfano kaangalie wale mitume walikotokea. Pia mtazame mtu Kama Paulo alikotokea. Kwangu sioni ajabu kwani Mungu ana njia zake ambazo wewe mwanadamu huwezi muelewa Kama hupo karibu naye. Pia utumishi kwa Mungu upo wa namna nyingi sana hata huko serikalini unaweza ukakuta aliwekwa na Mungu kumtumikia kwenye nafasi hiyo. Nimeshuhudia kwangu mwenyewe hata kwa mke wangu Kuna taasisi alituweka kwa maelekezo yake mwenyewe akitutaka tufanye kazi Fulani kwenye ile taasisi.
Hivi Kuna mtu amemdhihaki eenhh???
 
Acha usushi. Uliza uambiwe. Hilo sio vazi la kichungaji. Hilo Ni vazi la muinjilisti.
 
Back
Top Bottom