Uchaguzi 2020 Hatimaye CCM na mgombea wao waanza kutumia chopa kama usafiri wa kampeni

Usafiri wa chopa sio salama kabisa, usije ukawapiga chini kama wale wa 2015.
 
Mkuu I
Barafu mtaalam wa midege is back.

Kaka toka jamaa asitishe kulete midege,ukatuacha humu jukwaani.

Nikadhani umetoweka. Nafurahi kukuona tena.
Mkuu ID name yako inanikumbusha mbali sana kuhusu wazungu wawili wenye gari ya Malawi
 
Jamaa alishadondoka na helicopter...nikae kimya
 
Kweli nimeamini tuonyeshe rafiki zako tukujue tabia zako
 
Yalimuonea wivu Lissu alipotaka kutumia helikopta ushamba na ulimbukeni nizigo mzito sana .
 
Alafu kuna lijitu hapa linapiga kelele Eti magufuli apewe tano tena!!!

Nimeshasema na nasema tena kwa ufedhuli na uzandiki alioufanya Magufuli dhidi ya watanzania wenzake tukimpa tena miaka 5 hata shetani atatushangaa
 
Alafu kuna lijitu hapa linapiga kelele Eti magufuli apewe tano tena!!!

Nimeshasema na nasema tena kwa ufedhuli na uzandiki alioufanya Magufuli dhidi ya watanzania wenzake tukimpa tena miaka 5 hata shetani atatushangaa!!

Yaani Chadema wamefanyiwa figisu za wazi kabisa mchana kweupe kuhusu kutumia chopa alafu CCM haohao nao wanaenda kutumia Chopa alafu Kuna mtu na akili zake bado anashawishi magufuli achaguliwe tena!!!

Kati ya kipindi murua ambacho Mungu katuwekea kutupima akili Watanzania ni kipindi hiki. Kusema kweli kwa roho mbaya na uzandiki wa Magufuli na CCM yake hata shetani atatushangaa tukimchagua tena. Si Mungu tu!
 
Maelezo mengine hayakuwa na umuhimu kabisa.
 
Hapo ndipo mnapokosea
Siku nyingine huwa nawaeleza halafu hamfuati, niliwaambia mnichague mimi mkasema sawa, nikawaambia mnichagulie na mbunge wa CCM hamkunichagulia, nataka niwaeleze ukweli wala siwafichi asingekuwa Kapuya hii barabara nisingeijenga". Dkt.Magufuli
 
Mtu mwenye roho mbaya anajenga barabara, hospitali, kusaidia walioonewa, kupambana na rushwa na uonevu?

Mtu mwenye roho mbaya hafanani hata kidogo na Rais Magufuli
 
Kwahiyo kutumia chopa ni kuishiwa pumzi?

CHADEMA ina watu wengine wa hovyo kabisa mmoja wapo ni wewe
Kutumia Chopa kwa hali ya kawaida si kuishiwa pumzi hata CHADEMA walipanga kutumia Chopa wafike nchi nzima lakini kwa kuwa hawakuonyesha wameishiwa pumzi walizuiwa kutumia Chopa na wanaendelea na kampeni. CCM baada ya karibu mwezi kwenye kampeini wamegundua wameishiwa pumzi na kuamua kutumia Chopa muda uliobaki lakini ili nao wasizuiwe wanaithibitishia Mamlaka ya Safari za Anga kuwa wako hoi kwa kupiga push-up mbele ya Chopa. Watapata kibali hata kama Nyachae (babu wa rubani wa CHADEMA) mwenyewe atakuwa rubani.
 
Mtu mwenye roho mbaya anajenga barabara, hospitali, kusaidia walioonewa, kupambana na rushwa na uonevu?

Mtu mwenye roho mbaya hafanani hata kidogo na Rais Magufuli
Hata tupate raisi Jini hospitali zitajengwa tu!! Hajengi kwa pesa zake ni hela za kodi za wananchi.
Roho mbaya ya mtu inaonekana kwenye matendo yake dhidi ya watu wengine hasa anaoona wamemzidi au wako kwenye nafasi ya kumzidi.
 
Magufuli anahangaikia nini?? Si amejenga mabarabara na amenunua madege na ameunda meli??!!
 
Kwa hiyo hawataki kutumia barabara walizozijenga?
 
Wakati Chadema wamejiandaa kutumia chopa na kisha kuzuiwa...Polepole alisema wao wanatumia barabara ili wakutane na wapiga kura.
Leo imekuaje tena?
Pole pole ni wa kupuuzwa tu wadudu wameshachanganya mashudu tu ndiyo yanambeba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…