Hakika lakuvinda halina ubani,unaweza kusema hivyo kwa huyu dogo.
Baada ya kukabidhiwa usemaji wa chama akawa sasa ni mtu wa kutanua kifua na kuwashurutisha mawaziri.
Juzi tu akamtisha mdogo wake mfanyabiashara na kumwambia sasa utanijua,unajua mimi ni nani ndani ya chama?
Juzi juzi pale Kipawa anamfananisha Rais Samia na marehemu kuwa kila anachofanya Rais wa sasa ni kumuiga marehemu Magufuli.
Kitendo cha kumsema Rais wa nchi kuwa kila anachokifanya ni Sawa na alichofanya marehemu ni kumvunjia heshima kiongozi aliyepo madarakani.
Hili litakuwa ni fundisho kubwa Sana Kwa huyu kijana maana sasa anenda kuwa uraiani na kuhangaishana na kina Lema mitaani na jila lake la Bashite linaweza kutumika sasa.
View attachment 2949650