Hatimaye nimepata wa kunituliza, hivi sasa mimi ni "Miminimama wa Tajiri"

Hatimaye nimepata wa kunituliza, hivi sasa mimi ni "Miminimama wa Tajiri"

Mama G anahitaji baby shower kwakweli..😂😂.

Am happy for you my dear..Mungu wetu azidi kuwalinda na mzeeke pamoja wallah..💞

Hivi G ana kaka ake ?🤔😂😂
 
Naamini siku yangu itaenda poa kwa kukutana na uzi huu asubuhi hii,

Hongera sana best yangu kwa kupata kile moyo wako unapenda, ukamtunze, ukamuheshimu, ukambeleze mwanaume wako, wanaume aina hiyo hawapatikani kwa dunia hi tuliyomo, nimefurahi sana pamoja na wewe,

Kawe mwaminifu kwa gharama yoyote ile, hata ukiomba chochote kwa muumba wako utakipata Tena kwa wakati, usikubali kulala pasipo kusawazisha mgogoro wowote wewe na G, hata uwe ni mdogo vipi, jinyenyekeze kwake na kwa hakika kifo ndo kitawatenganisha

Kila la heri kwenu
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Ana cousin wake.
Ahsante mpenzi nakumbuka ulikuwa unaniuliza kama kweli au natania.
Nilikuwa namaanisha na Mungu akanipendelea akanipa zaidi ya nilichoomba.
Kuna watu tunakutanishwa nao kwa sababu maalum.
Natamani uone jinsi mwanangu alivyo na furaha.
 
Labda ngoja nikuambie ukweli ambao hakuna wa kukuambia!Kama hutaki kurudi tena Misri achana na kuwekeza imani yako,moyo wako,mapenzi yako,muda wako na nguvu zako kwa mwanaume badala yake jikite kwenye kuondoa umasikini wa kipato.Kwenye dunia hii hakuna kinachotesa kama umasikini wa kipato.Mwanaume anaweza kubadilika anytime.
 
Mtoto wako ni rafiki yangu lakini ukinikubalia ombi langu sitajali kuwa Baba yake wa kambo pia
 
Back
Top Bottom