Hatimaye nimerudiana na mpenzi tulieachana naye

Npe location
Ukitoka hapo kwa mangi, njoo na hii bara bara ya toroka uje, utanikuta nimesimama bara bara ya kushoto nikiwa nimevaa tisheti nyeusi 😀
 
Nmekuona aya vuka huku nmevaa pama la babu yangu
Nimekuona, kwa pigo hilo ulilovaa utaniharibia siku, rudi nyumbani ukavae lile pigo lingine la ubarikio ndio uje 😀 😀
 
Ilikua wkend moja, nimeamka asubuhi nikahisi kuchoka choka kutokana na mawazo pamoja na majukumu ya kila siku.

Ikabidi nioge haraka haraka, na kuamua kwenda chimbo moja angalau nikapate supu ili mwili ukae sawa.

Katika lile chimbo, kwa bahati mbaya alikuwepo yule mpenzi wangu tulie achana naye; akawa ameniona ila mimi sikumuona.

Kutokana na uwepo wangu pale, yule bibie akawa anavuta kumbukumbu ya mahusiano yetu yalivyo kuwa, ingawa hakupata ujasiri wa kunifuata nilipokuwa.

Bila kujua hili wala lile, nikalipa bili yangu na kuamua kuondoka; ilipofika usiku nikaamua kwenda kiwanja kimoja chenye 'vibe' kali, ambacho nilikuwa nikienda na bibie.

Baada ya kufika pale, mhudumu akanisogezea meza pamoja na vinywaji vyangu ninavyovipenda.

Baada ya kufika saa sita usiku, naona na bibie akiwa na wenzake wakaingia huku yeye akiwa amevaa kipedo cheupe na shati la maua maua.

Kwa kuwa mara nyingi tulikuwa tukienda naye kwenye kile kiwanja wahudumu walishamkariri; ndipo mhudumu mmoja akamwambia equation x yupo pale.

Bibie akamjibu, '' nimeshamuona ila leo nimekuja na wenzangu'', nami nikavunga kama vile sijamuona. Nikaendelea kupiga mvinyo taratibu.

Muda unavyozidi kwenda, bibie akawa anazidi kulewa zaidi kutokana na mawazo, pia akawa anacheza mziki katika mazingira ya kumshawishi mwanaume yeyote, ukichangia na chura aliyonayo.

Ilipofika majira ya saa nane usiku, ndipo nilipoamua kuchukua ujasiri wa kiume na kunyanyuka nilipokuwa nimekaa na kumfuata nyuma bila yeye kujua.

Baada ya kumfikia nikashika rasta zake kwa ubunifu wa hali ya juu; alihisi kama mwili umepigwa ganzi na vinyweleo vya mwili wake kusimama.

Alipogeuka, akakutana na sura yangu; alichokifanya ni kunikumbatia na kuanza kubadilishana ndimi huku akilia.

Ndipo nikamwambia, ''the man is back''; hapo alianza kulia zaidi huku tukiwa tumekumbatiana.

Baada ya muda tukatoka naye kidogo, angalau kwenda kumchangamsha kidogo ili awe sawa.

Baada ya kama dakika 45 tukawa tumerudi na kuendelea na mitungi pamoja na kucheza mziki.

Kwa sasa tupo pamoja, ni shoo shoo tu.​
Ashakumu si matusi, "hatimaye mavi imerudi kwa matako baada kunya"
 
Genuine and well made
 
Back
Top Bottom