Hatimaye picha kutoka James Web telescope zimetolewa rasmi kwa umma

Daah mwenzenu nawaza sana kama JWST itatoboa miaka 20 ambayo inatakiwa kuwa operational. Kwani imeshatobolewa na microkimondo huko anga za majuu na leo NASA wametoa picha ya assessment of impact. Daa sijui niwapatie ushauri gani kuzuia tukio kama hili kujirudia, maana katika hesabu zao hawakupigia kukutana na that size ya microkimondo. Ni changamoto sana 10 billion USD.

Hii picha kushoto is new and right is damaged mirror segment.
 
wanachonifurahisha wakienda wakati wa kurudi huwa wanaenda kuchukuliwa na Mrusi.
 
Mimi huwa najiuliza hivi mnawezaje kutofautisha hizi picha na picha za kutengeneza ? Yaani mnajuaje kama hizi ni picha halisi na siyo za kutengeneza ? Au huwa mnapenda kuona kuliko kujadili ?
 
speed ya mwanga ni 3x10^8
Hivi hii speed ilipimwaje mpaka ikapatikana hii thamani ?
Hii miaka billion 4.5 waliijuaje ? Naomba ufafanuzi kidogo nipate kuelewa.
 
Sayansi raha sana!
Shida ya Sayansi ipo katika kukufanya uujue ukweli au kukupeleka katika kuujua ukweli, hapa ndipo kuna mauza uza ya Sayansi.

Maana imewasilishwa, sijaona hata mmoja akihoji kuhusu au juu ya ukweli wa hizo habari. Lakini kwa maendeleo ya sasa katika usawirishaji wa mambo watu kutengeneza picha kama hizo wanaweza sana. Sasa tunapoletewa habari kama hizi watu wanatakiwa waumize akili na kufikiri na kuhoji, kinyume na hapo tutishi miaka yote tukiamini mambo ya uongo na uzandiki tu.
 
Katika picha hii unaweza kuona maelfu ya galaxy yakiwa umbali wa 4.5 billion light years away. Yaani tunaona leo hizo galaxy jinsi zilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita.
Camera iliyotumika kupata hii picha inaitwa Web near infrared camera.
Hapa sijakuelewa mtoa mada, ufafanuzi tafadhali. Hapo zinavyo onekana ndiyo ndivyo zilivyokuwa miaka 4.5billion sasa nikitaka kuona zilivyo leo hii nafanyaje au nasubiri tena miaka 4.5billion ijayo ?

Lakini jambo hili linawezekana vipi ? Kwa hiki ulichokiandika.
Picha hii na taarifa zote zinazokisanywa zinaenda kutusaidia kutupa majibu ya maswali kuhusu mwanzo wa ulimwengu huu. Namna galaxy zilivyokuwa formed etc.
Early Universe
Hili linawezekana vipi ? Hivi mfano wewe ukitaka kujua miaka 300 hali ilivyo kuwa ni lazima utumie hiki kifaa au upate taarifa kutoka kwenye the "Primary Source" ?

Hapa akili zetu zinatakiwa zitumike vizuri. Yaani unawezaje kujua hali ya dunia kutokea au kuwepo pasi na kuwa na taarifa za walio shuhudia tukio hilo ?

Wanasayansi kuna muda wanakuwa hawaeleweki kabisa, au mimi ndiyo siwaelewi ?
 
Wale jamaa wa Mudi wanakuja muda c mrefu kupinga na vipedo vyao
Nipo hapa tayari. Siyo tunapinga bali tuna hoji ili tuujue ukweli, sababu hizi zama zina uongo mwingi kuliko ukweli na watu si wenye kuhoji bali wanapenda kuona kuliko kuhoji na kujadili.

Kwa zama zilizo fika hasa kwa kutumia picha ni ngumu sana kuujua ukweli mpaka watu wasogee mbele zaidi katika kuhoji na kutafakari.

Yaani kwa picha hizo kutumika kama ushahidi kwa mtu makini ni ngumu sana, sababu hizo picha watu wenfi wa graphics au wajuzi wa graphics wanatengeneza sana backgrounds na Walla paper za hivyo. Sasa umakini unatakiwa sana.

Sasa kama kichwa chako au akili yako huishughulishi utabeba kila unachokisikia.
 
Mimi huwa najiuliza hivi mnawezaje kutofautisha hizi picha na picha za kutengeneza ? Yaani mnajuaje kama hizi ni picha halisi na siyo za kutengeneza ? Au huwa mnapenda kuona kuliko kujadili ?
Ni kweli mkuu hizi picha ni za kutengenezwa na kamera za "Infrared Camera" ambapo jicho la binadamu haliwezi kuona miale(electromagnetic) ya kiwango cha Infrared..
Halafu zinatengenezwa kwa kufuata sensor za rangi tatu zilizo katika retina ya jicho yaani Nyekundu(Red), Kijani(Green) na Bluu(Blue) ili kuwezesha jicho la binadamu kuona kama vile lingekuwa na uwezo wa kuona miale ya "Infrared"... 🙃
 
Yawezkana pia mbingu ikawa ipo katika moja wapo ya galaxies zainazo exist.

Japo concept yako ya limitations ya physical body ina make sense kiasi.
Yaan una maanisha Mungu Baba wa majeshi akawa yupo kwenye moja ya hizo galaxies?
 
Mimi huwa najiuliza hivi mnawezaje kutofautisha hizi picha na picha za kutengeneza ? Yaani mnajuaje kama hizi ni picha halisi na siyo za kutengeneza ? Au huwa mnapenda kuona kuliko kujadili ?
Picha zinazotumwa na Jwst huwa zinafanyiwa color coloration ili ziweze kuwa visible katika macho yetu.

Kwa sababu details za picha hizi zinachukuliwa katika midrange infrared. Ambayo macho ya bianadamu hayawezi kuona.

 
Inashangaza!
 
Hivi hii speed ilipimwaje mpaka ikapatikana hii thamani ?

Hii miaka billion 4.5 waliijuaje ? Naomba ufafanuzi kidogo nipate kuelewa.
Soma hapa




Miaka billion 4.5 iko hivi hiyo picha ya smacs. Ulimwengu unatanuka kwa speed kali sana. Sasa huo mwanga ulioweza ku be captured na JWST ulitoka katika hilo eneo miaka 4.5 iliyopita kwa maana hiyo ni kwamba hapo unatazama hilo eneo lilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita.
 

Kisai asante kwa comment yako.
Space exploration ni suala linafanyiwa kazi na matawi ya sayansi ya cosmology na Astronomy. Hizi branch of knowledge ambazo ni tata kweli kweli.
Kwa bahati nzuri kwa sababu ya maendeleo ya ICT tuna uwezo wa kupata elimu juu ya cosmology na Astronomy japo basic tu.

Picha hizi zilipotolewa ufafanuzi wake ulitolewa live on the spot.
Pia mijadala mbalimbali inafanyika katika sehemu mbalimbali mtandaoni na katika TV.

Ndo maana hata hapa jamii forum kuna mijadala ya kina juu ya kazi hii ya kipekee ya bianadamu.

PIA NASA wao wanatoa ufafanuzi wa kina katika media zao. So kama una swali lolote juu ya picha hizi majibu yake yako mtandaoni.

Na bahati nzuri hizi picha zilishachukuliwa pia na vyombo vingine vya space exploration so siyo kitu kipya sana kwa wafuatiliaji wa hizi mambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…