Hatimaye picha kutoka James Web telescope zimetolewa rasmi kwa umma

Hatimaye picha kutoka James Web telescope zimetolewa rasmi kwa umma

"Katika picha hii unaweza kuona maelfu ya galaxy yakiwa umbali wa 4.5 billion light years away. Yaani tunaona leo hizo galaxy jinsi zilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita."


Mkuu hayo maelezo hapo yana kiuchachu fulani hivi.
kivipi?? Maana yake ni kuwa huo mwanga unaofika leo duniani ulisafiri kwa takribani miaka billion 4.5 ndo umefika leo duniani. Hata unapoliangalia jua, sio kwamba ndiyo liko hivyo unapoliangalia, Lilikuwa hivyo dakika 8 zilizopita..Mwanga ndo umefika duniani hapa baaada ya dakika 8
 
4.5 billion light years ni parefu sana swali kwako ni je wamewezaje kuona huo mwanga wake? Na je hiyo teknolojia haiwezi kuongezwa zaidi ili kuzoom kilichopo ndani yake?
mwanga umefika duniani. kumbuka mwanga unasafiri, ndomaaana wameweza kuona.
Hiyo teknology ya kuzoom bado haijagunduliwa.
Kwenye picha kama hizo, distance kutoka Dot moja ya kanyota/galaxy kwenda dot nyingine ya karibu inaweza kuwa ni mamillioni ya lightyears. (Yaani umbali ambao mwanga utasafiri kwa mamilioni ya miaka) Kumbuka kwa sekunde moja mwanga unaweza kuizunguka dunia mara 8.

Sasa kama teknolojia ya kuzoom kutoka Dar-Moro hatuna, sembuse hiyo??

Labda itakuja kuwezekana miaka billioni mbili ijayo
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Yani huyo kweli bi wale dunia ni tambarare
 
Unajua hujaeleza jibu kwa mujibu wa, Sayansi inavyoelezea mambo, bali umeleezea kifalsafa sababu kuna maswali hujajibu. Mfano hujaonyesha starting point kama marejeo ni ipi ?

Alitumia kifaa gani kujua hiloi, je alifika kwenye Sayari ya Jupiter ? Sababu ili ujue mwendo lazima ujue umbali husika kuanzia mwanzo na mwisho. Hili walilijuaje ?

Dunia inakuwa mbali na Jupiter kivipi na kipindi gani na kwa sababu gani ?
Mzee baba naona ntapoteza muda. Unajua hesabu za ellipse. Orbit sio circual but elliptical na kupata hizi facts na mathematical proven ni simple Google mathematics explanation ya hizo distance utagundua tuu
 
mwanga umefika duniani. kumbuka mwanga unasafiri, ndomaaana wameweza kuona.
Hiyo teknology ya kuzoom bado haijagunduliwa.
Kwenye picha kama hizo, distance kutoka Dot moja ya kanyota/galaxy kwenda dot nyingine ya karibu inaweza kuwa ni mamillioni ya lightyears. (Yaani umbali ambao mwanga utasafiri kwa mamilioni ya miaka) Kumbuka kwa sekunde moja mwanga unaweza kuizunguka dunia mara 8.

Sasa kama teknolojia ya kuzoom kutoka Dar-Moro hatuna, sembuse hiyo??

Labda itakuja kuwezekana miaka billioni mbili ijayo
Mwambie tuu kutoka duniani kwenda mars ni safari ya miezi 6[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au solar system tuu mpaka next star ni 5 light year [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] galaxy yetu na Andromeda ni 2m light year [emoji23][emoji23][emoji23]
 
tatizo letu kila kitu tunaleta masihara, ndio maana tunaishia kula na kuhonga, huwa hatupendi kushughulisha akili zetu kufikiria na kuongea mambo yenye tija.
 
Mwambie tuu kutoka duniani kwenda mars ni safari ya miezi 6[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au solar system tuu mpaka next star ni 5 light year [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] galaxy yetu na Andromeda ni 2m light year [emoji23][emoji23][emoji23]
😀 Kwenye galaxy yetu hapahapa tu, kutoka upande mmoja kwenda mwingine (diammeter) mwanga unatumia miaka laki 1 😀 😀
 
N
Leo tarehe 12/7/2022 ni siku muhimu sana kwa wapenzi wa space exploration.

Furaha hii inachangiwa na NASA wakishirikiana na agencies wengine kuweza kutoa rasmi picha na tafiti za kwanza kabisa kutoka katika darubini 🔭 ya JWST.

Kabla ya kuendelea ningependa kushare na wewe msemo huu kuwa ili civilization yoyote iweze ku survive ina wajibu wa kuwekeza kwenye space exploration.

Kwa kulijua hilo kazi hii ya kipekee ya NASA imekuja na majibu ya kuvutia na kuweza kuisaidia tasnia ya Astronomy.

Picha za kwanza za JWST zilizotoka ni

SMACS 0723
View attachment 2288405
Hii ni picha ya kwanza kabisa ambayo inaonyesha eneo la mbali zaidi kabisa kuweza kuonekana na binadamu.

Picha hii inaitwa Web first deep field.

Katika picha hii unaweza kuona maelfu ya galaxy yakiwa umbali wa 4.5 billion light years away. Yaani tunaona leo hizo galaxy jinsi zilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita.
Camera iliyotumika kupata hii picha inaitwa Web near infrared camera.

The NASA/ESA/CSA James Webb Space Telescope has produced the deepest and sharpest infrared image of the distant Universe to date. Known as Webb’s First Deep Field, this image of galaxy cluster SMACS 0723 is overflowing with detail.

SMACS 0723: Webb has delivered the deepest and sharpest infrared image of the distant universe so far – and in only 12.5 hours. For a person standing on Earth looking up, the field of view for this new image, a color composite of multiple exposures each about two hours long, is approximately the size of a grain of sand held at arm’s length.

This deep field uses a lensing galaxy cluster to find some of the most distant galaxies ever detected. This image only scratches the surface of Webb’s capabilities in studying deep fields and tracing galaxies back to the beginning of cosmic time.

Picha hii na taarifa zote zinazokisanywa zinaenda kutusaidia kutupa majibu ya maswali kuhusu mwanzo wa ulimwengu huu. Namna galaxy zilivyokuwa formed etc.
Early Universe

WASP-96b (spectrum):
View attachment 2288410
A transmission spectrum made from a single observation using Webb’s Near-Infrared Imager and Slitless Spectrograph (NIRISS) reveals atmospheric characteristics of the hot gas giant exoplanet WASP-96 b. ILLUSTRATION: NASA, ESA, CSA, STScI.

James Web Space Telescope imetuletea details za hii exoplanet na imetuonyesha kuwa anga lake lina H20 yaani lina maji. Hii tafiti inataka kutupa majibu kuwa kuna uwezekano wa uhai katika exoplanet hii?

Tafiti za mwanzo hatukuweza kuona mawingu na aina ya anga hewa la exoplanet hii lakini sasa tumeweza kuona na kujifunza zaidi kuhusu exoplanet hii iliyoko umbali wa zaidi ya 1000 light years away.

James web Telescope inaenda kutafiti uwepo wa sayari zenye sifa kama dunia yetu. Na kazi ya kwanza ndo hiyo imeanza.

Southern Ring Nebula:
View attachment 2288414

This side-by-side comparison shows observations of the Southern Ring Nebula in near-infrared light, at left, and mid-infrared light, at right, from NASA’s Webb Telescope. IMAGE: NASA, ESA, CSA, STScI

JWST Imetupa nafasi ya kuweza kuona namna ambavyo nyota zinavyokufa polepole.

Southern Ring Nebula:

This planetary nebula, an expanding cloud of gas that surrounds a dying star, is approximately 2,000 light years away. Here, Webb’s powerful infrared eyes bring a second dying star into full view for the first time. From birth to death as a planetary nebula, Webb can explore the expelling shells of dust and gas of aging stars that may one day become a new star or planet.
Webb: Southern Ring Nebula comes into full view – Astronomy Now

Stephan’s Quintet:
View attachment 2288510

Hili ni kundi la galaxy 5 kuwahi kuonekana na sayansi ya bindamu. Webb imetusaidia kuweza kuliona karibu na kutupa nafasi ya kujifunza. Kupitia Stephans Quintet tutaweza kujifunza namna interaction ya galaxies inavyokuwa na ilileta impact gani cosmically kwenye formaton of early universe.

Webb’s view of this compact group of galaxies, located in the constellation Pegasus, pierced through the shroud of dust surrounding the center of one galaxy, to reveal the velocity and composition of the gas near its supermassive black hole. Now, scientists can get a rare look, in unprecedented detail, at how interacting galaxies are triggering star formation in each other and how the gas in these galaxies is being disturbed.

Pembeni ya Stephan’s Quintet WEBBS imeweza kutuonesha uwepo wa black hole yenye mass ya 24 million equivalent to our sun mass.

Carina Nebula: Webb’s look at the ‘Cosmic Cliffs’ in the Carina Nebula unveils the earliest, rapid phases of star formation that were previously hidden. Looking at this star-forming region in the southern constellation Carina, as well as others like it, Webb can see newly forming stars and study the gas and dust that made them.
View attachment 2288416
Carina Nebula hapa ndipo ambapo nyota huumbwa. Webbs imeweza kutupatia picha kutoka katika eneo hili umbali wa miaka 7200 ya speed ya mwanga.
Kupitia ujifunzaji wa eneo hili tutaweza kufahamu namna ambavyo nyota zinavyokuwa formed.

Mada nyingine zilizoandaliwa na mwandishi mimi ni
James Web Telescope: Darubini kali kwa ajili ya kutazama anga la mbali yaondoka rasmi duniani | JamiiForums James Web Telescope: Darubini kali kwa ajili ya kutazama anga la mbali yaondoka rasmi duniani

Ina mashaka na upishi wao
 
Miaka 4.5 iliyopita.
According to bing bang theory
Ulimwengu unatanuka kwa speed kali kuliko ya mwanga.

Ili uweze kuelewa vizuri hebu jifunze hapa
Nini kilitokea katika " Big Bang " ? | JamiiForums Nini kilitokea katika " Big Bang " ?
Ukishaelewa kuhusu bingbang theory sasa utakuwa unaelewa ni namna gani ulimwengu ulivyo na unavyofanya kazi.

Kwa sababu ulimwengu unatanuka kwa speed kubwa kuliko mwanga basi utakpokuwa umeamua kutazama katika anga hata kwa macho tu zile nyota unaziona ni vile zilivyokuwa mamilion ya miaka iliyopita kwa ziko mbali.


Kwa lugha nyingine iko hivi

Mwezi unazunguka dunia
Dunia inazunguka jua
Jua nalo linazunguka kitovu cha milk way galaxy,
Na milk way galaxy nayo inazunguka,
Yaani kila kitu katika ulimwengu kiko katika mwendo kasi,
Ulimwengu unatanuka kwa speed kali sana.
Kwa maana hiyo unapoona mwanga wa jua ina maana umesafiri kutoka katika jua mpaka duniani. Umbali kutoka juani mpaka duniani ni kilometers 150 million kwa maana hiyo mwanga wa jua hutumia dakika nane kufika duniani kwani mwanga unasafiri kwa speed ya km 300000 kwa second.
Kwa maana nyingine ni kwamba jua unaloliona siyo live ila ni lilivyokuwa dakika nane zilizopita.

Mwezi unaouona mwanga wake unatumia 1.3 seconds kufika duniani kwa maana nyingine mwezi unaouona sivyo ulivyo sasa ila ni 1.3 seconds zilizopita.

Kwa sababu ulimwengu unatanuka matukio ya miaka billion iliyopita mwanga wake ndo JWST imeweza kuyanasa wakati huu.
Tunaposema mwaka mmoja wa speed ya mwanga ni 300000km x 60 second x 60 minutes x 24 hours x 30 days x 12 months =trillion 9 km jibu lake ndo km hizo.
Yaani mwanga kufika hapa duniani utachukua mwaka mmoja. Yaani ukibahatika kuona hiyo nyota 🌟 basi sivyo ilivyo sasa ila ni mwaka mmoja uliopita.

Nakupa mfano huu lets say kuna aliens yupo katika nyota ya karibu kbx na solar system inaitwa proxima Centaurus iko umbali wa 4.5 light years away akachukua telescope 🔭 akatazama duniani hapa. Basi ataiona dunia ilivyo mwaka 2018. Yaani ataiona TANZANIA YA MAGUFULI.

Macho yako ni time machine kwani utazamapo angani na ukaziona nyota basi unazipna zilivyo mamilion ya miaka iliyopita.
Gud info
 
Mimi na nyinyi tunatofautiana sehemu moja, mimi nataka kujua kwanini hizo namba zimekuwa hivyo vilivyo, na nyinyi mnafurahia hesabu mnazowekewa.

Mimi kwanza kabisa unatakiwa uthibitishe ukweli usio na shaka juu ya "Big Bang Theory" au "Big Bang Models"

Aliens ni nani ? Na kwanini Aliens ? Kwanini usiandike chukulia wewe ndiyo upo katila hiyo Nyota fulani ?

Nachotaka mimi unipe hesabu zako pasi na kuwepo "Assumptions" yoyote katika hesabu husika, huo mwendo kasi wa mwanga umepatikana vipi ?
Boss hii sio business adminstration ....ukaelewa unavyotaka wew ndo maana 1+1=2 na sio 11 was science ndo ilivyoo
 
Asante mkuu kwa kunielewa

Albert Einstein "l anasema kwamba "If you can't explain it to a six year old, you don't understand it yourself." Concept ya light year ni very complicated.
 
Nazijua vizuri mno, kwani hakuna mzunguko katika Ellipse ? Jibu upo. Sasa hoja yako iko wapi hapo ?
? naona ntapoteza muda. Unajua hesabu za ellipse. Orbit sio circual but elliptical na kupata hizi facts na mathematical proven ni simple Google mathematics explanation ya hizo distance utagundua tuu
Maana yake katika Orbit hakuna starting point ? Sijaona hoja yako iko

Hakun aMathematical Proven kwenye sehemu ambayo ndani yake kuna "Assumptions" zaidi ya makubaliano ya Wanamahesabu.

Jitahidini haya mnayo yasoma muyajue na mtupe majibu, siyo kutuambie twende google, elimu ni ile ambayo ipo kifuani mwako.
 
Boss hii sio business adminstration ....ukaelewa unavyotaka wew ndo maana 1+1=2 na sio 11 was science ndo ilivyoo
Hoja yako iko wapi hapo sasa. 1+1=2 huu ni uhalisia na haiwezi kuwa 11. Sasa hesabu za Anga zinaleta 1+1=11 na siyo 2 tena, yaani zina assumptions nyingi, sababu nyinyi bado watoto katika kuhoji na kufikiri na kuujua ukweli wa Sayansi hasa ya anga, siku mkijua kwanini kuna "Assumptions" katika nadharia zao na hesabu zao, mtajiona wajinga msio faa hata kupigiwa mfano.
 
Hoja yako iko wapi hapo sasa. 1+1=2 huu ni uhalisia na haiwezi kuwa 11. Sasa hesabu za Anga zinaleta 1+1=11 na siyo 2 tena, yaani zina assumptions nyingi, sababu nyinyi bado watoto katika kuhoji na kufikiri na kuujua ukweli wa Sayansi hasa ya anga, siku mkijua kwanini kuna "Assumptions" katika nadharia zao na hesabu zao, mtajiona wajinga msio faa hata kupigiwa mfano.
Assumptions kama za yule mtu aliyeenda mbingu ya saba kwa farasi mweny mabawa na ukaamini ni kweli. Kama hili unaliamini bila uhalisia wowote tena bila kuhoji ni umbali gani hadi huko mbingu ya saba while unapinga umbali unaosafiri mwanga wa jua hadi duniani huku ukidai uthibitisho kabisa
Unaweza kuwa ndio mtu mjinga kabisa ambae umewahi kutokea humu
 
Hii tarifa nilikuwa naangalia live sky news walikuwa live kwenye NASA HQ daah nimevutiwa sana na lecture iliyokuwa inatolewa pale gafla na mimi nikatamani kuwa astronomer [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Pale kuna wamama wawili walikuwa wanaeleza hadi raha sana. Akaja na Chairman wa NASA naye yuko simple ukimuona na anavyoongea
 
Shida ya Sayansi ipo katika kukufanya uujue ukweli au kukupeleka katika kuujua ukweli, hapa ndipo kuna mauza uza ya Sayansi.

Maana imewasilishwa, sijaona hata mmoja akihoji kuhusu au juu ya ukweli wa hizo habari. Lakini kwa maendeleo ya sasa katika usawirishaji wa mambo watu kutengeneza picha kama hizo wanaweza sana. Sasa tunapoletewa habari kama hizi watu wanatakiwa waumize akili na kufikiri na kuhoji, kinyume na hapo tutishi miaka yote tukiamini mambo ya uongo na uzandiki tu.
na kwa nini uamini ni uongo wakati NASA na mashirika mengine yapo unaweza kwenda kujiridhisha, acheni ushamba basi fatilieni mambo, hao watu unaosema huwaamini ndio wamekutengenezea hadi hio simu ambayo haina wire wala connector na unaweza mpigia mtu hata alieko China na Marekani
 
Kwanza kabla ya ufafanuzi na kukujibu swali lako unatakiwa akili yako ui switch iwe kama ya mtoto ili uwe egoless kuweza kuruhusu ubongo wako kupokea maarifa mapya.

Hii field inahitaji akili kubwa ndo maana huwezi ikuta kwenye vijiwe vya kahawa.

Sasa narudi kwenye swali lako.

Kwanza unapaswa kufahamu kuwa binadamu anaona sehemu ndogo sana ya waves za electromagnetic spectrum inaitwa visible light.

Sasa nikufahamishe kuwa binadamu anapna sehemu ndogo sana ya kilichoko kwenye universe.
Mfano mdogo ni internet mawimbi ya radio huwa hatuyaoni ila yanasafiri from 1 point to another point.
Tukiongea kwenye simu mawimbi yanasafiri hivyo hivyo lakini macho yetu hayana uwezo wa kuyaona.

Matukio yaliyokwisha kupita hatuwezi kuyaona kwa macho coz ni mid infrared katika electromagnetic spectrum. Kwa sababu hiyo JWST hutumia camera ambayo ina uwezo wa kunasa picha katika mid infrared light na yanapotumwa duniani kuna program hutumika kuweza kuzi coloring ili ziweze kuwa visible kwa binadamu kwani binadamu ana uwezo wa ku detect rangi tatu tu ambazo ni red, green, and blue.


Je kwa faida ya wasomaji ni aina gani ya technology hutumika kuweza kufanya photo colorize?
Naomba uitazame vizuri hii video imeeleza vizuri na kwa mifano halisi!.



Nasa wanaelezea hapa namna ambavyo hufanya photo colorize

Nakufatilia sana mkuu
 
Back
Top Bottom