Hatimaye picha kutoka James Web telescope zimetolewa rasmi kwa umma

4.5 billion light years ni parefu sana swali kwako ni je wamewezaje kuona huo mwanga wake? Na je hiyo teknolojia haiwezi kuongezwa zaidi ili kuzoom kilichopo ndani yake?
Ndio mana kila baada ya tafiti wanaobuni technolojia mpya ili kugundua vitu vipya, thats why watu dunia nzima wamefurahi kua mwanzo mzuri kama hizo galaxy za mbali hivo zimeweza kuonekana, sasa watajitahidi wabuni kifaa kitakachokua na uwezo zaidi kuliko kilichotumika sasa.
 
Nithibishie ya kuwa jua ninalo liona muda huu ni la dakika 8 zilizo pita.
unaweza hata kuthibitisha mwenyewe, jioni wakati jua linakaribia kuzama dakika 8 kabla, chukua darubini angalia hilo jua unaloliona, wala hutoliona zaidi ya mwanga sababu lishahama
 
Asante sana mike2k ila naomba kukurekebisha kidogo hapo nilipo-bold.

Light Years maana yake ni umbali mrefu sana. Kisayansi, ni umbali ambao mwanga (light) huweza kuchukua mwaka mzima kuufikia.
 
Yote kwa Yote science ni mchanganyiko WA religion. MISSION Yao yoote Ni kwenda ulimwengu WA pili... Ile gateway ndo inatafutwa... Ndo maana wanajaribu kuplay around na Time. Wanaweza fanikiwa maana CERN wameshaufungua upya mtambo wao. Time travel etc etc....
 
Asante sana mike2k ila naomba kukurekebisha kidogo hapo nilipo-bold.

Light Years maana yake ni umbali mrefu sana. Kisayansi, ni umbali ambao mwanga (light) huweza kuchukua mwaka mzima kuufikia.

Asante Lizzy kwa kunirekebisha

Naomba unitajie "Assumptions" hata tatu katika ile safari ya Mtume kwenda mbingu ya saba. Kingine uonyeshe ya kuwa lile tujio siyo uhalisia.

Pili, ushawahi kuhoji kuhusu habari za mwanga kwa mujibu wa Sayansi ?

Tatu, kwenye hili unatakiwa ujipange kuhadiliana na mimi. Kama huna hoja fanya shughuli nyingine.
 
Ndiyo maana tuna hoji, sasa kama nyinyi hamna uwezo wa kuhoji, ni tatizo lenu.

Mimi sina haja ya kwenda huko unakosema wewe, bali natumia elimu yangu na akili niliyopewa kung'amua mambo.
 
unaweza hata kuthibitisha mwenyewe, jioni wakati jua linakaribia kuzama dakika 8 kabla, chukua darubini angalia hilo jua unaloliona, wala hutoliona zaidi ya mwanga sababu lishahama
Soma ulichokiandika hapa na hicho cha kabla kikichofanya nikuombe uthibitisho. Maana naona unaruka ruka na kuchanganya mambo. Sasa umerukia katika darubini. Jikite katika msingi. Ukitaka turudi kwenye kujadili Darubini tutarudi tu sababu hiki ni kifaa na tunajua mipaka yake na madhumuni ya chenyewe kutengenezwa kwa ajili gani.
 
"Katika picha hii unaweza kuona maelfu ya galaxy yakiwa umbali wa 4.5 billion light years away. Yaani tunaona leo hizo galaxy jinsi zilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita."

Mkuu hayo maelezo hapo yana kiuchachu fulani hivi.
Aisee hii Ni balaa. Hapa nashindwa kuelewa Kama mwanga unasafiri kwa muda huo uliotajwa. Ina maana hii picha ilipigwa lini? Au mwanzisha uzi kujichanganya.
 
Nachanganyikiwa hapa. Je, hizi picha zilipigwa lini!?
 
Nimeanza kuelewa. Ina maana mtu akiwa huko kwenye hizo galaxies Kisha akawasha tochi yenye uwezo mkubwa kumulika duniani kwetu, huo mwanga utatufikia kwa huo muda uliotajwa.
 
"Katika picha hii unaweza kuona maelfu ya galaxy yakiwa umbali wa 4.5 billion light years away. Yaani tunaona leo hizo galaxy jinsi zilivyokuwa miaka billion 4.5 iliyopita."

Mkuu hayo maelezo hapo yana kiuchachu fulani hivi.
Jamaa yuko good..ingawa kwa hapa nafikiri alitakiwa kusema "hizo galaxy zipo umbali wa ambao mwanga unatakiwa kusafiri miaka Bilioni 4.5 ili kufika huko."
 
Jamaa yuko good..ingawa kwa hapa nafikiri alitakiwa kusema "hizo galaxy zipo umbali wa ambao mwanga unatakiwa kusafiri miaka Bilioni 4.5 ili kufika huko."
Light year ndo SI unit ya distance katika cosmology na Astrophysics.

Nimejitahidi kuieleza distance ya zilipokuwa hizo galaxies katika lugha ya kueleweka.
Pia asante ulivyoeleza wewe pia ni sahihi na ni lugha nyepesi zaidi kwa msomaji kuweza kuelewa.

Tazama hii video kuweza kuelea ukubwa wa ulimwengu huu
https://www.facebook.com/
 
Mimi huwa najiuliza hivi mnawezaje kutofautisha hizi picha na picha za kutengeneza ? Yaani mnajuaje kama hizi ni picha halisi na siyo za kutengeneza ? Au huwa mnapenda kuona kuliko kujadili ?
Na mimi nimejiuliza hili suala wamarekani wajanjawajanja sana sio wa kuwaamini
 
Binadamu tumefikia mahali pa kubwa saana yaani bado tuu kuzuia kifo
Hatujui kitu ndugu yangu. Hizo zote ni salakasi, tunaongopewa mpaka tukome.

Hadi sasa hakuna binadamu anayeweza kukuelezea kwa ufasaha pyramid za Kemet zilijengwaje.

Hapo Mali kuna kabila linaitwa dogons. Hao jamaa wanaujua ulimwengu hakuna mchezo.

Hizo habari za wazungu ni movies tuu, hakuna chochote ni propaganda zao hata hazina maana.
 
Kwanini wakudanganye ili wapate faida ghani?
Haya project nasa artemis hiyo iko katika majaribio kabla ya kwenda mwezini..

https://www.facebook.com/
Unaalikwa kwenda kushuhudia live

https://www.facebook.com/
Marekani waliwahi kutudanganya wameenda mwezini na wakaexpose mapicha kama hayo kabla ya mwishi wa siku Russia kuja kuwaumbua kuwa ni waongo..lengo lao la kudanganya si lingine bali wapewe sifa tu na kuogopwa
 
Asante sana mike2k ila naomba kukurekebisha kidogo hapo nilipo-bold.

Light Years maana yake ni umbali mrefu sana. Kisayansi, ni umbali ambao mwanga (light) huweza kuchukua mwaka mzima kuufikia.
Hakukosea. Wewe ndiye hukumwelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…