Marekani waliwahi kutudanganya wameenda mwezini na wakaexpose mapicha kama hayo kabla ya mwishi wa siku Russia kuja kuwaumbua kuwa ni waongo..lengo lao la kudanganya si lingine bali wapewe sifa tu na kuogopwa
United State of America ni taifa lenye muunganiko wa nchi 52. taifa lenye raia zaidi ya million 352. Taifa hili lina umri wa zaidi ya miaka 300 kasoro. kila mwaka wanazalisha Wataalam wa masomo ya science, mathematics, technology zaidi ya 600k kwa mwaka mmoja tu. Wakati wewe mtanzania bado serikali imeshindwa kutatua tatizo la madawati ilhali miti iko hapahapa nchini. Hawa Tayari wana shirika linalojihusisha na anga exploration na mwaka huu wamelitengea 24$ billions ambayo kibongobongo ni 53 Trillion shillings.
Kwa maana hiyo wamekuzidi wewe mtanzania kila kitu na itakuhitaji wewe mtanzania na serikali yako 1000 light years kufika waliko leo hii.
Kwa hiyo kukaa na kuamini kuwa walikaa chini kukudanganya inakuhitaji uwe mvivu wa kusoma pro max ili uweze kuihifadhi hiyo conspiracy katika ubongo wako.
Sitaki tuanze kubishana kuhusu NASA apollo 1 mission coz ndo next thread yangu. NASA and her partners (blue moon,space x, toyota,lookhead Martin space etc) tarehe 29 agoust 2022 wataanza mission ya kwanza kabisa NASA artemis 1 kwa hiyo itakuwa ni wakati muafaka kabisa wakuweza ku observe na ku discuss moon missions kwa mapana yake.
Hii project ya JWST ili waweze kukudanganya ingebidi waanze kuwadanganya space agencies wa NASA,CANADA NA EUROPEAN AGENCIES kwani project nzima imefanywa na zaidi ya watu 20000 kwa kipindi cha miaka 10.
Na usifikiri labda ni NASA wana fedha? hapana. Hizi fedha zinatolewa na serikali kupitia ruhusa ya Baraza la Seneti kwa maana hiyo ni lazima wafanye presentation katika bunge la Seneti na senate wapige kura kuridhika kuwekeza hicho kiasi huko kisha ipelekwe Congress na congress watunge sheria za kusimamia project nzima.. Ndo hivyohivyo pia Bunge la Canada liliridhia na bunge la Ulaya pia.
Kwa hiyo hakuna sababu yoyote ile ya watu 20000 astrophysics, cosmologist, Scientists🥼 makampuni mbalimbali ya binafsi kuwekeza fedha na mida wao ili wakudanganye.
Kitu ambacho unatakiwa ufahamu NASA project zao nyingi huwa wanashirikisha public kwa lengo la kujifunza, Vyuo vikuu mbalimbali huhusika kwa ukaribu kabisa katika Research and Development.
Upe ubongo wako nafasi ya kujifunza.
ukuta wa imani usikufanye uwe kipofu.