Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Rais wa Urusi Vladimir Putin amehutubia Taifa lake kwa mara nyingine leo akitoa msimamo kuhusu shambulizi la kigaidi lililoua zaidi ya Watu 130 Crocus City Hall ambapo amesema ni kweli Waislamu wenye itikadi kali wamehusika na shambulio kama Marekani na Washirika wake wanavyosema lakini Putin amesema bado kuna maswali mengi ya kujiuliza ili kumjua aliyewatuma Wahalifu hao, moja ya swali hilo likiwa ‘inawezekanaje Waislamu wa kweli wakaua Watu ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani!!”.
Putin amenukuliwa akisema “Huu uhalifu umefanywa na Waislamu wenye msimamo mkali , Marekani wanatumia hii fursa kujaribu kwa makusudi kuficha ukweli kuhusu wanaohusika na shambulizi na wanasema ISIS ndio wanahusika moja kwa moja na shambulizi lakini tunajua ambaye amepanga na kutekeleza shambulizi lakini tunachotamani kwa sasa ni kumjua aliyewatuma na kutoa amri wafanye shambulizi”
“Vyombo vyetu vya uchunguzi na vya kisheria vinatakiwa kujiuliza na kupata majibu ya maswali mengi ikiwemo kwamba ‘inawezekanaje?, Waislamu wenye msimamo mkali ambao wanajinasibu kuwa ni Waislamu wa kweli wanawezaje kufanya dhambi kubwa kama ile ya kuua Watu ndani ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan!?’, swali hili na mengine ya kitaalamu yatasaidia kwenye uchunguzi wa shambulizi hili na tutapata majibu, tutajua nani ananufaika na shambulizi lile”
“Shambulizi hili linaweza kuwa lina mahusiano ya karibu kabisa na Mataifa/Watu ambao wanaipiga vita Urusi tangu kwaka 2014, maumivu ambayo wote tunayahisi na hamu tuliyonayo ya kumuadhibu kila aliyehusika tunatakiwa kuhakikisha uchunguzi unafanyika kwa viwango vya juu vya kitaalamu bila kumuonea Mtu au kuegemea upande wowote kwa sababu za kisiasa”
Huyu Putin🤣
Haya maneo ya kishogoa sijui hatimaye sijui kiana ni yenu eti unamuuliza maswali Putin nimecheka sana..