Tunaweza kuwalaumu sana hawa ^watoto wa mamdogo,^ lakini ukichunguza kwa kina utagundua kwamba tabia yao hii ya kueneza, kuimarisha na kulinda imani yao kwa upanga walijifunza kwa Wakotoliki.
Nani asiyejua kwamba Ukatoliki ndio ilikuwa dini ya dunia nzima enzi za Mfalme Konstantini wa Dola ya Rumi?
Baada ya kuweka mamlaka ya ufalme chini ya mikono yao, Ukatoliki ukaanzisha harakati za kujitanua kidini na kueneza imani yake kwa watu wote kwa lazima.
Wakristo wa kweli na wapagani—wote walishurutika ama kuupokea ushirikina wa Kikatoliki au kuuawa.
Nani asiyejua ukatili wa kutisha uliofanywa na Ukatoliki katika zama za giza?
Nani asiyejua jinsi ambavyo Ukatoliki uliwateketeza kwa moto na upanga na mateso mamilioni ya wale waliokuwa wakifuata mafundisho halisi ya Kristu kwa mujibu wa Biblia?
Nani asiyejua kwamba Papa John Paulo II aliomba radhi dunia kwa ajili ya mauaji na ukatili uliofanywa na Ukatoliki enzi hizo?
Nani asiyejua jinsi ambavyo Ukatoliki ulipiga marufuku Biblia isisomwe wala kufundishwa, isipokuwa kwa idhini yake, huku ikiweka mwongozo kuhusu masomo gani yafundishwe na kwa namna gani?
Kwa kisingizio cha kumtetea Kristu, Ukatoliki ulikuwa ukiwaangamiza wafuasi wa Kristu!
Ni wapi ambapo Bwana Yesu alifundisha kwamba imani ienezwe kwa njia ya upanga? Au ushurutishaji?
Angalia namna Yesu alivyofundishwa:
^Bwana… akawatuma… kwenda kila mji na kila mahali… [Akawaambia,] Enendeni, angalieni, nawatuma kama wanakondoo kati ya mbwamwitu….
Na nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwemo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu…
Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha,… waponyeni wagonjwa waliomo, waambieni, Ufalme wa Mungu umewakaribia.
Na mji wowote mtakaouingia, nao hawawakaribishi, tokeni humo.^ Luka 10:1-10.
Ni wazi kwamba mfumo wa uenezaji imani ya Ukatoliki hautokani na Biblia kama alivyofundisha Kristu, bali hutokana na yule muuaji wa roho za watu—Ibilisi mwenyewe!
Si ajabu historia inaonesha kwamba kuna uhusiano wa karibu kati ya Ukatoliki na Uislamu. Kimsingi, Uislamu ni zao la Ukatoliki!