Hatimaye tapeli sugu wa viwanja nchini atiwa nguvuni

Hatimaye tapeli sugu wa viwanja nchini atiwa nguvuni

Kivipi wakati kuna legal document kupitia wanasheria na anafanya kwa miongozo ya usajili wa makampuni plus miongozo ya wizara ya Ardhi ambayo hizi private company ni agency na zipo regulated na wizara.
Criminality hapo ipo wap? Kuwa na legal document siyo justification kosa ni la jina kosa ninaloliona hapo ni CIVIL CASE, mkataba una makubaliano

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Isijekuwa huyo ndiyo kaiuza bandari yetu wa Waarabu?

Maana nasikia hawa matapeli wa udalali walishamuuzia Mmasai Msikiti huko Morogoro, mahodhi ya kutwadhia wakamwabia unaona eroo, hapa unaogesgea dawa ng'ombe zako wakati wowote...
Foxy unatetea wizi Mtoto wa Kiislamu!!
 
Msimpakazie bandari mmeuza wenyewe maccm, ndio maana mmekomaa hili ni swala la chama na ilani, ilani ya ujambazi.

Pale Kunduchi kwa Kondo kina ya kwenda kaburi la Sharrif Ras Kilomoni kuna mkondo wa bahari maji kupwa maji kujaa, kuna mmasai alipigwa kweli hapo kiwanja wakati wa maji kupwa, kesho aliporudi palepale alipouziwa akaikuta bahari hamna kiwanja.
Story za Abunuasi hizo! Thibitisha!!??
 
Kampuni ya uwakili iliyotumika kutapeli ni Eagle Laws Chamber ,Bank ni NMB,na TIN ni wakili ni
Baadhi ya Ma Wakili ni Wana tamaa sana na wako tayari kutetea uwongo kwa hali na Mali popote pale kisa pesa, utu wanauacha nyuma!!
 
Kuna tapeli mwingine anakesi mahakamani na ameshinda kesi hiyo.

Huyu tapeli mtusi anaconnection mahakamani ila hata balozi hamtambui na wenyeviti hata waliopita serikali za mitaa hawamtambui ...cha ajabu eti ameshinda keshi .... Hamuwezi kuamini lkn ni kweli...
Nchi hii imamaajabu Sana
Kama una vielelezo nenda kwa Msajili wa Mahakama ataku shauri bila Malipo na utakuja nishukhkuru!!
 
Wasalamu, kupitia msaada wa mitandao ya jamii imefanikisha kulikamata tapeli sugu na maarufu nchini jina Yonah Kittah pichani chini.

Kwa miaka mingi amekuwa akifungia kampuni halali za kuuza viwanja na mashamba kwa kulipia kidogo kidogo kwa awamu.

Kisha ukishamaliza kulipa mkopo wako anaanza danadana ya kukupa kiwanja au shamba lako.

Alifungua ofisi Mbezi beach kwa jina la Yared investment akawatapeli watu viwanja walipomzonga kutaka viwanja au pesa zao akawambia.

Akaenda Ilala Mwalimu House akafungua kampuni inaitwa VKP youth development akiuza viwanja na mashamba ikiwemo kukopesha pikipiki na bajaji akatepeli zaidi ya bilioni moja Mimi ni mmoja wa mhanga kanipiga milioni 60, kwa kampuni pekee ya vkp tumepigwa jumla ya watu 250 kwa idadi ya walipoandikisha kesi mwaka 2020 kwa mikoa ya Arusha, Dodoma,Mwanza na Dar es salaam.

Alikaa ndani akatoka kwa dhamana kesi ikiendelea akakimbia dhamana ya shilingi bilioni moja.
Akaenda fungua kampuni nyingine ya kutapeli viwanja ofisi ikiwa Manzese Darajani akapiga hela, kafungua makampuni mengi tu ya kupiga Hela.

Kama wewe ni muhanga wa hizo kampuni kutapeli viwanja za mmiliki jina Yonah Kittah jongea central Dar ofisi ya upelelezi waone wahusika ukiwa na ushahidi wa documents zako zote wakutolee shimoni mtu wako ili uongezwe kwenye list ya watu waliotapeliwa na Yonah Kittah.

Kwa taarifa alienda Nigeria kujifunza jinsi ya kutapeli watu kitaalamu na jinsi ya kula na wakubwa na jinsi ya kudili na kesi.

Pana mtu kapigwa milion 60 na Yonah kwa ishu za viwanja na ndoa imevunjika mume haelewi somo.

Anachofanya huyu tapeli anaenda kwenye mashamba ya watu Usiku anapima code net kisha anachora ramani nzuri anavipa viwanja plot number anasajili mchoro ardhi kisha anatangaza anauza viwanja mnapelekwa site mnaonyeshwa viwanja pori mkiuliza mbona pori anasema greda lipo njiani kuchonga barabara za mitaa unaingia kingi unasaini mkataba unapewa account ya kampuni unalipia unakuwa unapewa risiti, kimbembe umemaliza unataka hati kiswahili kinaanza, ukienda eneo husika kumtafuta mmiliki anakwambia Mimi simjui Yona wengine wanasema tulifanya nae mapatano ya kununua shamba hakurudi Tena.

Mkiwa wengi mnamsumbua anafunga ofisi anatoroka wasiojua wao wanaendelea kurejesha pesa kwenye account siku unaenda na risiti zako za miezi labda 3 unakuta hakuna ofisi.

Ujinga wake pesa zote hizi anamalizia kwenye starehe hana hata Hela kwenye account zote anaponda raha kila mwanamke mzuri mjini hampiti.

So kama wewe ,ndugu yako au jamaa yako ni mhanga wahi central Dar.

Wahanga ni wengi wakiwemo hadi viongozi, watumishi ndio wa kada zote wakubwa kwa wadogo ni wahanga.

View attachment 2694136
Hana jina?!
 
Kama hjna hoja ya kuchangia ni heri ungekaa kimya tu.

Akili kubwa huongelea maendeleo.
Akili ya kawaida huongelea matukio
Akili mbovu huongelea watu.
Mwenzako ameleta hoja ya maana,watu wametapeliwa pesa mingi wwe unaleta porojo zako za Bandari sijui na Wamasai wamefanya nini, au kwa kua hujatapeliwa wwe!? Subiri siku wajanja wa town wakupige ndiyo utajua machungu ya kuibiwa haki yako!!
 
Mwenzako ameleta hoja ya maana,watu wametapeliwa pesa mingi wwe unaleta porojo zako za Bandari sijui na Wamasai wamefanya nini, au kwa kua hujatapeliwa wwe!? Subiri siku wajanja wa town wakupige ndiyo utajua machungu ya kuibiwa haki yako!!
Ukisikia kuna Mtanzania hajawahi kutapeliwa elewa kuwa huyo si Mtanzania. Hususan kwa wat wa Dar Es Salaam.

Unafikri jina la "bongo" lilichipuwa tu kama majani?
 

Attachments

  • Screenshot_20230512_082131.jpg
    Screenshot_20230512_082131.jpg
    29.4 KB · Views: 9
Utapeli unathibitishwa na mahakama tu.
Hawa organized criminal gang wanacheza na mahakama na mda.
Watu wapo bize watapigwa kalenda miaka wanapungua mmoja mmoja then hakimu anafuta kesi,mtu aache mishe zake atoke Arusha dodoma au Mikoani aje dar ipigwe tarehe anakata tamaa.Kesi ya awali ilikua hivyo hivyo ana kesi kisutu tayari process yake imesuasua.
Huyu aogopi kesi huu utapeli wa kucheza na kesi Kama walivyokuwa mapapaa ya mjini.
Matapeli dawa zao Huwa ni plan B na Sio kesi mtasumbuana sana.
 
Niwape pole sana kwa yaliyowakuta.

Ki ukweli sasa hivi utapeli umekua advanced sana. Hata uwe mjanja au msomi bado unaweza kuokotwa kirahisi kabisa ukiingia kwenye 18 zao, especially uwe muajiriwa maana hata muda wa kufuatilia vitu kwa ukaribu huna.

Kuna mwanangu juzi juzi tu hapa nusu apigwe laki 7 kuhusu haya mambo ya ajira za mchongo serikalini. Ogopa sana mtu kakutanishwa hadi na afisa utumishi na afisa tawala wa serikali wenye vitambulisho kabisa. Kumbe ni ma afisa wa mchongo na IDs pia ni za mchongo!

Jamaa ananiambia kwanza ni watu wazima kabisa halafu kila kitu kuhusu mambo ya ajira na serikali wanajua mpaka nafasi za kazi zote zinazotangazwa wanazijua na idadi ya watu wanaohitaji na mahali zinapofanyika...kila kitu! (Watu wako serious na kazi zao!)

Kilichomuokoa hakuwa na hela kamili. Kwaiyo ikabidi amshirikishe Broh wake yupo gvt pia ili amuongezee hapo hela kidgo mchongo ukamilike. Ndio Broh akachezwa na machale akamwambia amtumie hayo majina aliyoyaona kwenye IDs zao amuulize mtu chap amuangalizie kama ni kweli hao watu ni wa serikalini. Aisee... kumbe hawapo!

Wakaishia kutukanana na ndio ikawa pona yake..!

Kwaiyo saivi matapeli wako very organized yani kupona kwako ni mpaka uwe makini sana au uwe na bahati kama Jamaa maana kama angekua na hela yote waliyotaka angeshapigwa zamani sana!
 
Back
Top Bottom