Hatimaye tapeli sugu wa viwanja nchini atiwa nguvuni

Hatimaye tapeli sugu wa viwanja nchini atiwa nguvuni

Isijekuwa huyo ndiyo kaiuza bandari yetu wa Waarabu?

Maana nasikia hawa matapeli wa udalali walishamuuzia Mmasai Msikiti huko Morogoro, mahodhi ya kutwadhia wakamwabia unaona eroo, hapa unaogesgea dawa ng'ombe zako wakati wowote.

Mmasai si awapeleke ng'ombe zake usiku usiku msikitini, kishalipa hela dalali kasepa.

Muadhin anakwenda kuadhin alfajiri anakuta ng'ombe kibao msikitini, hapaingiliki.

Kimbembe.
Msimpakazie bandari mmeuza wenyewe maccm, ndio maana mmekomaa hili ni swala la chama na ilani, ilani ya ujambazi.

Pale Kunduchi kwa Kondo kina ya kwenda kaburi la Sharrif Ras Kilomoni kuna mkondo wa bahari maji kupwa maji kujaa, kuna mmasai alipigwa kweli hapo kiwanja wakati wa maji kupwa, kesho aliporudi palepale alipouziwa akaikuta bahari hamna kiwanja.
 
Lipo lockup limenenepeana kwa utapeli,baada ya kutengeneza chain kila ya kuuza viwanja hewa kila siku Hela zinaingia Benki ye ni kudraw na kufanyia ngono tu.
Utapeli huu wa kiofisi na kusuka kampuni za kitapeli alienda Nigeria kujifunzia
 
Wizara ya Ardhi,Brella,mabenki,TRA,Leseni jiji wekeni stop list huyu mtu kumpatia huduma za vibali.
Kampuni moja tu ya VKP kapiga zaidi ya bilioni moja toka kwa watza 250.
Kiwango Cha Chini kupigwa ni milioni 6.Wengine milion 15,17,32,60,21,
 
Kampuni ya uwakili iliyotumika kutapeli ni Eagle Laws Chamber ,Bank ni NMB,na TIN ni wakili ni
 

Attachments

  • Screenshot_20230720-213816.png
    Screenshot_20230720-213816.png
    219.4 KB · Views: 13
  • IMG_20230720_213406_991.jpg
    IMG_20230720_213406_991.jpg
    998.6 KB · Views: 12
  • IMG_20230720_213102_995.jpg
    IMG_20230720_213102_995.jpg
    710.7 KB · Views: 13
  • IMG_20230720_213235_786.jpg
    IMG_20230720_213235_786.jpg
    737.1 KB · Views: 12
  • IMG_20230720_213251_244.jpg
    IMG_20230720_213251_244.jpg
    635.5 KB · Views: 12
Poleni mliotapeliwa jamani
Ukisikia kampuni inauza viwanja,au online business sijui unalipa pesa wanakuagizia mzigo China kwa Bei rahisi usiingie na mguu wa kulia.
Hata Kama Wana ofisi hakikisha kwanza usalama wa pesa zako au try at your own risks.
Watz Sasa hivi wanafundishwa utapeli wa organized group na Wanigeria wanafungua legal office Kama mzionazo sampuli ya hizi DECI wengine ujifichia hadi kwa viongozi,Huwa wanaanza vizur tu mwanzon ili kuvutia wengi wakishapata market kubwa pesa ikaingia kwa wingi hapa ndipo wanapokuja achwa watu.
Hata online business hivyo hivyo mtaenda vizur ndani ya mwaka watajenga uaminifu wakishapata mzunguko mkubwa tu wanapiga.
Kisha wanacheza na kesi madai mahakamani miaka huku wanafungua kampuni nyingine kwa jina lingine kuendelea kupiga.
Mamlaka imelala na aina hii ya utapeli nchini.

Kampuni zote zinazodili na watu kutrust na kushawishi watu kuweka pesa zao ili wapate bidhaa au huduma ni za kumulikwa sana.
 
Wasalamu, kupitia msaada wa mitandao ya jamii imefanikisha kulikamata tapeli sugu na maarufu nchini jina Yonah Kittah pichani chini.

Kwa miaka mingi amekuwa akifungia kampuni halali za kuuza viwanja na mashamba kwa kulipia kidogo kidogo kwa awamu.

Kisha ukishamaliza kulipa mkopo wako anaanza danadana ya kukupa kiwanja au shamba lako.

Alifungua ofisi Mbezi beach kwa jina la Yared investment akawatapeli watu viwanja walipomzonga kutaka viwanja au pesa zao akawambia.

Akaenda Ilala Mwalimu House akafungua kampuni inaitwa VKP youth development akiuza viwanja na mashamba ikiwemo kukopesha pikipiki na bajaji akatepeli zaidi ya bilioni moja Mimi ni mmoja wa mhanga kanipiga milioni 60, kwa kampuni pekee ya vkp tumepigwa jumla ya watu 250 kwa idadi ya walipoandikisha kesi mwaka 2020 kwa mikoa ya Arusha, Dodoma,Mwanza na Dar es salaam.

Alikaa ndani akatoka kwa dhamana kesi ikiendelea akakimbia dhamana ya shilingi bilioni moja.
Akaenda fungua kampuni nyingine ya kutapeli viwanja ofisi ikiwa Manzese Darajani akapiga hela, kafungua makampuni mengi tu ya kupiga Hela.

Kama wewe ni muhanga wa hizo kampuni kutapeli viwanja za mmiliki jina Yonah Kittah jongea central Dar ofisi ya upelelezi waone wahusika ukiwa na ushahidi wa documents zako zote wakutolee shimoni mtu wako ili uongezwe kwenye list ya watu waliotapeliwa na Yonah Kittah.

Kwa taarifa alienda Nigeria kujifunza jinsi ya kutapeli watu kitaalamu na jinsi ya kula na wakubwa na jinsi ya kudili na kesi.

Pana mtu kapigwa milion 60 na Yonah kwa ishu za viwanja na ndoa imevunjika mume haelewi somo.

Anachofanya huyu tapeli anaenda kwenye mashamba ya watu Usiku anapima code net kisha anachora ramani nzuri anavipa viwanja plot number anasajili mchoro ardhi kisha anatangaza anauza viwanja mnapelekwa site mnaonyeshwa viwanja pori mkiuliza mbona pori anasema greda lipo njiani kuchonga barabara za mitaa unaingia kingi unasaini mkataba unapewa account ya kampuni unalipia unakuwa unapewa risiti, kimbembe umemaliza unataka hati kiswahili kinaanza, ukienda eneo husika kumtafuta mmiliki anakwambia Mimi simjui Yona wengine wanasema tulifanya nae mapatano ya kununua shamba hakurudi Tena.

Mkiwa wengi mnamsumbua anafunga ofisi anatoroka wasiojua wao wanaendelea kurejesha pesa kwenye account siku unaenda na risiti zako za miezi labda 3 unakuta hakuna ofisi.

Ujinga wake pesa zote hizi anamalizia kwenye starehe hana hata Hela kwenye account zote anaponda raha kila mwanamke mzuri mjini hampiti.

So kama wewe ,ndugu yako au jamaa yako ni mhanga wahi central Dar.

Wahanga ni wengi wakiwemo hadi viongozi, watumishi ndio wa kada zote wakubwa kwa wadogo ni wahanga.

View attachment 2694136
Kuna tapeli mwingine anakesi mahakamani na ameshinda kesi hiyo.

Huyu tapeli mtusi anaconnection mahakamani ila hata balozi hamtambui na wenyeviti hata waliopita serikali za mitaa hawamtambui ...cha ajabu eti ameshinda keshi .... Hamuwezi kuamini lkn ni kweli...
Nchi hii imamaajabu Sana
 
Una tapeli mwingine anakesi mahakamani na ameshinda kesi.

Huyu tapeli mtusi anaconnection mahakamani ila hats balozi hamtambui na wenyeviti hats waliopita serikali za mitaa hawamtambui ...cha ajabu eti ameshimda keshi .... Hanuwezi kuamini kkn ni kweli
Sidhani Kama kesi ni solution zaidi ya Plan B
 
Usikubali kuuziwa viwanja na hizi kampuni binafsi kwa kujiridhisha na ofisi nzuri location nzuri full documents za usajili ukutani bila kujiridhisha sana hakikisha wamiliki wa kwanza wa shamba Hilo unawajua pili usikubali kutoa pesa yako kwa kuonyeshwa code net au Raman kwa shamba pori eti mtasafishiwa kwa pamoja mkimaliza malipo.
Pana mama analiaa milion 36 imeliwa na Yona na ndoa chali kisa viwanja.
Huyu takataka hajali maumivu ya watu,na Serikali inacheka nae tu.
Watumishi tu mshahara kidogo anajinyima kapata unafuu wa kiwanja alipe kidogo kidogo baada ya mwaka awe na kiwanja aanze kujenga kumbe mwaka mzima unampa pesa mwanaume mwenzio anaenda kuzifanyia ngono,wewe unakula dagaa.
Yupo Moja Arusha huitwa David Kambele ni tapeli hafai. Anachukua sehemu za watu anaziuza kwa mtundo huo wa kulipa kidogokidogo, Kisha anahonga mabaraza ya kata na watendaji anaanza kuzungusha wamiliki halisi... Serikali imfatilie huko muriet na Terat ameliza watu sana

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Yupo Moja Arusha huitwa David Kambele ni tapeli hafai. Anachukua sehemu za watu anaziuza kwa mtundo huo wa kulipa kidogokidogo, Kisha anahonga mabaraza ya kata na watendaji anaanza kuzungusha wamiliki halisi... Serikali imfatilie huko muriet na Terat ameliza watu sana

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
Hahaa yule mmeru mbna fala tu...mimi ardhi zangu zote nanunua kupitia kwa wakili wng,kiwanja mpka nilipe nimeshaongea na ukoo wenu mzima bila wewe kujua
 
Hahaa yule mmeru mbna fala tu...mimi ardhi zangu zote nanunua kupitia kwa wakili wng,kiwanja mpka nilipe nimeshaongea na ukoo wenu mzima bila wewe kujua
Mi nilijua muaru, kumbe mmeru, yani yule ni fala kinyama, ameuza ardhi za watu sana, halafu yeye anacheza na mabaraza

Sent from my TECNO CI6 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom