Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 9,548
- 28,817
"Inaonekana tumeipoteza India na Urusi katika sehemu kubwa zaidi, yenye giza zaidi, China. Wawe na mustakabali mrefu na wenye mafanikio pamoja!"
— Donald Trump
— Donald Trump
Hivi karibuni Trump aliongeza ushuru kwa bidhaa za India hadi kufikia 50% kama adhabu kwa sababu ya India kuendelea kununua mafuta kutoka Urusi.
Kitendo hicho kimeifanya India ijikite zaidi kurekebisha uhusiano wake wa kidiplomasia na China na kuimarisha uhusiano wake na Russia.
Na hilo limeonekana kwa Modi kuhudhuria mkutano wa Shanghai Cooperation Organization (SCO) uliofanyika Tianjin, China. Ilipita miaka saba tangu mara ya mwisho Modi kuwa na mkutano wa mazungumzo na Xi.
Xi na Modi walikuwa na mazungumzo ya pamoja wakikubaliana kuimarisha umoja na kutatua mgogoro wa mipaka kati ya mataifa hayo.
Modi na Putin walionekana ndani ya Limo ya Putin wakizungumza mawili matatu. Na baadaye wakiwa na mazungumzo ya kina kwenye mkutano maalumu kati ya marais hao wawili wakiwa China.
Na kama inavyojulikana Urusi imezidi kuwa na ukaribu na China tangu ilipoanzisha Special Operation nchini Ukraine.
Na kama haitoshi Putin alikuwepo kwenye gwaride la jeshi la China kuadhimisha miaka 80 ya ushindi wa China dhidi ya uvamizi wa Japan.
Viongozi hawa watatu walionekana kuwa na ukaribu sana katika matukio hayo mawili. Nafikiri hii ni sababu kwa nini Trump ameamua kuondoa ukimya na kukiri.
Kwa kumalizia Trump aliyatakia mataifa hayo matatu mustakabali mrefu na mafanikio makubwa.
Trump amezipush India, Russia ziwe closer na China, sasa mataifa yenye watu bilioni 3 na nguvu kubwa za kijeshi duniani stand strong.

"The supreme art of war is to subdue the enemy without fighting."
— Sun Tzu (Chinese general and strategist)

So much winning kwa China!