Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 18,069
- 25,172
Siyo hao tu; mawaziri wake karibu wote ni watu wa pumba tupu.Kuna hawa vichaa wawili:
Marco Rubio ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani
Na Pete Hegseth Waziri wa Ulinzi wa Marekani
Hawa jamaa kwenye masuala ya diplomasia sijawahi kuwaelewa kabisa
Wana kauli za hovyo sana ndio maana kwa namna fulani Marekani inapoteza sana ushawishi
Raisi ana mdomo mchafu na mawaziri nao ni hovyo lazima wapoteze
- Tulsi Gabard Director wa NSA ni wa hovyo kabisa hajui analofanya bali andhani kazi yake ni kumfurahisha Trump tu, kwa mfano kutoa siri za NSA zinazofurahisha Trump na hivyo kuvuruga utaratibu mzima wa utendaji kazi ndani ya NSA bila mwenye kujua.
- Kash Patel Director wa FBI, analojua ni kuwaandama "maadui" wa Trump tu na kusahahu kuzuia uharifu halisa kwa nchi.
- Pam Bond Mwanasheria mkuu wa serikali, anachofanya ni kuwa mwanasheria wa Trump, siyo mwanasheria anayetumikia katiba ya marekani.
- Krist Noem waziri wa Mambo ya ndani hajui kabisa sheria inayoongoza mambo ya ndani, anachojua yeye ni kuvamia sehemu za kazi kutafuta wanaoitwa illegals na kuacha kazi halisi ya wizara yake
- Scott Bessent Waziri wa fedha hajui kuwa fedha za serikali ni tofauti na fedha za mtu binafsi kama ilivyo kwa Trump mwenyewe. Anachojua ni jinsi ya kukamua nchi nyingine kusudi serikali yake ipate pesa bila kujua madhara yake kidplomasia.
- Robert Francis Kennedy Jr. waziri wa afya, anachojua ni kupunguza matumizi ya serikali kwa kuondoa huduma za afya bila kujua madhara ya kuwa na taifa la watu wenye afya dhaifu. Hajui madhara ya magonjwa ya kuambukiza na umuhimu wa kuyazuia mapema kabla hayasambaa. Kuindoa US kwenye WHO ulikuwa ni upumbavu wa hali ya juu sana kwani magonjwa yanayoanza nchi moja husambaa dunia nzima hadi ndani ya Marekani.
- List ni ndefu sana