Hatimaye Uingereza imemaliza kutoa raia wake Tanzania leo

Hatimaye Uingereza imemaliza kutoa raia wake Tanzania leo

Wanaenda wapi wakati corona tanzania imeisha? Jumapili kesho kutwa ni party all day and all night. Yani badala ya waingereza wajaze ndege za watalii wao waje Tanzania, na sie mipaka iko wazi bin shee, wao wanafanya yao mbadala na kinyume chake kabisa, na kuwarudisha wageni UK? Itakuwa ni mabeberu tu hao 😉😉😉😀😀😀
 
Sisi tunafunguliwa wao wanakimbia...hawa nao ni mabeberu tu kama walivyo mabeberu wengine..na wasirudi!!
 
Umefarijika na nini mkuu? Mimi hakuna kitu kinachonikasirisha kama serikali kufanya usanii wakati watakaoumia ni walala hoi. Tusijidanganye, bado tunawahitaji sana mabeberu

Wewe ndiye umefarajika kwa kuona Wazungu wameondoka ili dua la kutaka Serikali iliyoko madarakani ikwame, litimie.

Ni kweli bado tunawahitaji kama wao wanavyotuhitaji la wasingeweka balozi zao hapa nchini. Ni maisha ya "Nipe Nikupe". Km sisi ni soko la bidhaa zao na mitaji yao. Wao wanatugemea kwa mali ghafi ya viwanda vyso, nk. Na isotoshe katika maisha "changamoto" ni "fursa". Mfano ufuatao unadhibitisha hili.

Kama ulikuwa mtu mzima wakati nchini kulikuwa na uhaba wa bidhaa muhimu, tukawa tunajipanga foleni kwenye maduka ya kaya, utajua nina maana gani. Wakati huo viwanda vidogo viliibuka vya kutengeneza baadhi ya bidhaa km sabuni, japo mwanzo zilikuwa zinachubua, ziliboreshwa kadri ya muda ulivyokwenda. Viwanda hivi vilikufa kifo cha mende tulipoanza utegemezi wa bidhaa kutuka nje ya nchi.

Hivyo usije kushangaa COVID-19 ikafufua na kukuza uvumbuzi wa ndani km sasa kumeibuka viwanda vya kutengeneza "takasa mikono", barakoa, mashine za kutakasa, nk. Viwanda vikubwa vimeongeza uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ambazo haziji tena kutoka nchi zilizofunga mipaka au zenye " lockdown".

Niamini kuwa G Sam una akili ya kujitegemea ila umeandika hivyo kufurahisha jukwaa.
 
Sasa Maghembe nchi zinazosaidia raia wake kwenye majanga kwanini zisibarikiwe ? Halafu kupuuza waliokumbwa na mafuriko Lindi , kudhulumu korosho , kudhulumu hela ya tetemeko , kuteka watu , kuvunja nyumba za raia bila fidia ila wa kwenu hawavunjiwi , kuficha taarifa za corona nk . hizi ndio positive issues unazozizungumzia ?
Nina heshimu sana michango yako kuna kitu ambacho wewe unakiona, lakini watu wengi huchelewa kukiona.

Lakini mfumo wa maisha au muunganiko wa jamii huwa unafanya kazi sawa sawa pale ambapo watu wote wanapo kuwa kinyume na wewe, mama yako, kaka zako, dada zako na ndugu wa damu hufa na wakwao.

Na hali hii huendelea mpaka kwenye nchi sababu matokeo yote chanya utafaidika na matokeo yote hasi yatakudhuru bila kujali upo upande gani. Wazungu wanaita collateral damage/benefit.
Watu watakuchukulia serious pale tuu utakapo weza kutofautisha matokeo ya madhara ya jumla au matokeo ya faida ya jumla.

Na hivyo ndio upinzani wenye kuheshimiwa, kinyume chake hata mazuri utakayo ya highlight watu watafanyia dharau. Na sidhani kama unapenda michango yako ichukuliwe hivyo.
 
‪Ubalozi wa Uingereza imewaondoa nchini raia wake na kuwarudisha nchini kwao ili kuungana na familia zao ‬.

Wakati sisi tunatarajiwa kufungua shughuli zetu jumatatu kwa vifijo na nderemo ya kufa mutu!
Screenshot_20200520-155147.jpeg


In God we Trust
 
Siku wakirudi tupate majina na idadi ile ile isiyopungufu ili tujue walikoelekea kama kuna usalama zaidi ya hapa Bongo!
 
Hapa hoja ni kuwa Uingereza imewaondoa raia wake hapa kwetu....
Siku wakirudi tupate majina na idadi ile ile ili tujue walikoelekea kama kuna usalama zaidi ya hapa Bongo!

In God we Trust
 
Back
Top Bottom