Hatimaye ujenzi wa stendi ya mabasi (Mbezi Luis) yaendayo mikoani yaanza kujengwa

Hatimaye ujenzi wa stendi ya mabasi (Mbezi Luis) yaendayo mikoani yaanza kujengwa

Stendi inaonekana ni ndogo mno kwa jiji kubwa kama Dar. Stend hii ni saizi ya kibaha town sio Dar. Tutajenga nyingine tena baada ya miaka 5.
Design huwa ina-consider idadi ya watu watakayoitumia na pia huwa kunakuwa na provision for expansion, yaan endapo idadi ya watu itaongezeka, basi jengo linatanuliwa. Ni kama mlimani city ilivyotanuliwa baada ya matumizi kuzidi uwezo
 
Naombeni msaada wa kuchambuliwa kazi za hawa watu, zinanichanganya kidogo. Architects, structure engineers, quantity surveyors, main contractors,service engineers na sub contractors. Wote wapo kwenye huu mradi majukumu yao ni nini?

Je haiwezekani akawepo architectures na contractors peke yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
Architect - Ndio anabuni lile jengo kwa ujumla wake, na ndio anaweza akapewa jukumu la u-project manager hadi jengo kuisha.
Structural engineer - Ndie ana-design zege na nondo pamoja na vitu vingine vinavyohusiana na ubora na uimara wa jengo.
Quantity surveyor - Yeye ndio anakadiria gharama ya ujenzi wa jengo husika, maana serikali haiwezi kulipa bila kujua kiasi gani kinatakiwa kilipwe.

Main contractor - Huyu ndie mjenzi mwenyewe (Civil engineer), yeye ndio anaubadilisha mchoro kutoka kwenye karatasi na kuuleta kwenye uhalisia, kiufupi ndie anajenga.

Service engineers (Sub-contractors) - Mfano ni mechanical engineers ambao wanafunga Lift, escalators, Air conditioners, mabomba ya maji nk.; kuna electrical engineers wanaofanya wiring ya umeme kwenye jengo, kuna IT engineers wanaofunga mitambo ya mawasiliano, kuna enviromental engineers watakaoshughulika na mifumo ya maji taka nk.
 
safi sanaaa kodi zetu tunaziona zinavyotumika heko JPM heko CCM
 
Jambo jema lakini kwa hawa machinga kuwaluhusu kufanya biashara ndani ya stand ndio tatizo,angalia kwa mfano pale morogoro wanaharibu kabisa show ya stand,fukuzia mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom