::::::
Serikali ya Tanzania kupitia kwa Waziri wake wa Mipango na Uwekezaji Prof Kitila Mkumbo imeliambia Taifa hilo kuwa Ujenzi na Uendeshaji wa Bandari ya Bagamoyo bado haujaanza na kama utaanza basi Serikali hiyo itaufanya mradi huo kwa sharti la Ubia kati yake na Sekta binafsi yaani PPP kupitia kituo cha Ubia PPPC.
Mbali na Ujenzi wa Bandari hiyo Waziri Kitila amesema miradi mingine itakayoangukia PPP ni pamoja na Ujenzi wa Kituo cha Reli ambapo Waziri huyo amesisitiza kuwa kila hatua za Ujenzi huo Wananchi kupitia PPPC watashirikishwa kikamilifu ili Tanzania na Watanzania waweze kunufaika na rasilimali zao walizopewa na Mungu wao.
Wachambuzi wa maswala ya Kiuchumi na kisiasa toka nchini Tanzania walipohojiwa na chombo hiki walionesha kuwa na imani na kituo cha Ubia kama msimamizi mkuu wa Mali za Umma kwakuwa kituo hicho Kiko chini ya Kiongozi wake David Kafulila ambaye kwa umri na rekodi zake zote anasifika kama mtu anayechukia rushwa na Ufisadi.
Ikumbukwe na ifahamike kuwa Ubia PPP sio Ubinafshaji bali ni Uendeshaji wa miradi | mradi wa pamoja kati ya Serikali na Sekta binafsi na wakati wote baada ya ukomo wa mkataba husika Mali zote zitasalia kuwa ni Mali za Wananchi wa Jamuhuri ya Tanzania.
:::::::