Unajifichia kwenye kichaka Cha uandishi wa heshima.
Huyo mzee Mwinyi sijatumia neno mzee pia nimetumia neno ALHAJ nayo ni neno ambalo humpa mtu "heshima"
Wewe kuwa mzee usitake kutufanya sisi vijana tuonekane si lolote si chochote na kwamba eti hatuna adabu Wala heshima. Hizo tabia za WAzee wapenda ubabe na kujikweza kwa mambo rahisi.
Mimi nitakuambia ukweli tu Sina haja kuongea kinafiki Wala kubembelezana. Ukiona unakejeli na jeuri Hilo ni tatioz lako binafsi, Mimi halinihusu. Ujumbe mujarabu niliokusudia niumefikisha.
Narudi Tena sambaza kampeni ya kuwaamhia waislamu wapeleke watoto shule Bora sio madrassa tu wapeleke watoto vyuo Bora sio kule M.U.M.
Halafu waje baadae waseme wanaonewa wakati hawafit demand iliyo kwenye skilled, semi-skilled, non-skilled labor.
Nakuheshu sana kwa umri wako wa miaka 60 ila nikuambie usitake kutumia kigezo Cha umri wako kulazimisha hoja zako zikubalike hata kama Zina UKAKASI.
Waambie wenzio katika Imani wapeleke watoto shule na vyuo Bora.
Huwezi ukawa unashikilia mambo ya kale sijui TULIONEWA hivi na vile. Why kwanini Sasa usipige kampeni kweli kweli Ili hii jamii Yako huko mbele iwe na dominance kubwa kwenye hayo mambo mnayoyataka. Fursa mnazo Sasa ila mnakalia mambo ya kale yatawasaidia Nini!?.
Mangungo...
Hapana sijajificha popote si hapa JF au penginepo.
Nafahamika kwa jina langu halisi na kwa picha na sauti.
Wewe ndiye uliyejificha.
Hakuna anaekujua kwa sura au kwa jina lako halisi na pengine haya ndiyo yanayokufanya ukawa ''jasiri'' kuandika kama hivi uandikavyo.
Kama kweli wewe ni hodari na shujaa jitokeze kama nilivyojitokeza mimi.
Kuhusu wewe kuniambia mimi ukweli.
Ukweli gani utakaokuwanao wewe ushindane na ukweli wangu?
Mimi nimeandika kitabu cha Abdul Sykes kimebadili historia nzima ya uhuru wa Tanganyika achilia mbali kubadili historia ya Julius Nyerere.
Kitabu kinakwenda tolea la tano sasa toka kitoke 1998.
Mimi kitabu changu kipo katika Cambridge Journal of African History na kimepitiwa na wasomi mabingwa wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan.
Nimekizungumza kitabu hiki Northwestern University, Chicago, USA.
Hawa ndiyo mabingwa wa African History ulimwenguni.
Mimi ni mmoja wa waandishi 500 ulimwenguni walioandika Dictionary of African Biography (DAB) mradi wa Harvard na Oxford University Press, New York (2011).
Ukweli gani utakuwanao wewe ambao utaandika uchapwe na kusomwa Vyuo Vikuu?
Niwaambie Waislam wapeleke watoto shule.
Mimi nikizungumza maneno hayo nitaonekana hamnazo.
Wewe utasamehewa kwa kuwa huna ulijualo.
Mwaka wa 1962 Sheikh Hassan bin Ameir aliitisha Muslim Congress na agenda ilikuwa elimu.
Azimio la mkutano huu ilikuwa EAMWS kujenga shule Tanganyika nzima na Chuo Kikuu.
Historia ya Chuo Kikuu sina haja ya kuirejea tena hapa.
Serikali iliipiga marufuku EAMWS na Sheikh Hassan bin Ameir akakamatwa na kufukuzwa Tanganyika BAKWATA ikaundwa.
Leo 2024 unasema niwaambie Waislam wapeleke watoto shule.
Unadhani hawajui faida ya elimu watu waliokuwa wanajenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968?
Unasema MUM si chuo cha maana.
Sikushangai.
Unazungumza kuhusu hoja.
Unajua nimeandika ''research papers'' na vitabu vingapi?
Unajua kwa siku ninaandika maneno mangapi?
Unajua nimechapa makala ngapi katika majarida ya kimataifa na hapa nyumbani?
Mambo ya kale yapi?
Waislam wamefanya maandamano dhidi ya dhulma za NECTA mwaka wa 2012 na baada ya maandamano yale haki ikapatikana.
Ushahidi uliofikishwa serikalini ulitosheleza.
Northwestern University, Evanston, Chicago