Ukweli usemwe;
Mimi nilikuwa Muislam ila baadae niliamua kuokoka,kwahiyo nitazungumza vyema sana kuhusu Uislam na Elimu kama ifuatavyo;
Uislam unaichukulia Elimu Dunia kama elimu ya kikaffir bali wanawekeza nguvu kubwa sana kwenye elimu akhera.......Nakumbuka Baba yangu alikuwa akitoka kazini swali la kwanza ni kuwa "Ulienda chuo (Madrasa)?" Na kama sikwenda basi atanichapa sana ila kama sikwenda skuli basi huchukulia kawaida tu..........na wazazi wengi wa kiislam wanataka wana wao wakalili Alif,Bee,Tee badala ya A,B,C.......wakati huo watoto wa kikristo wanapoteza muda wao mwingi kwenye Tuition na ata kama ni dini hujifunza Sunday school,tofauti kabisa na uislam ambao kila siku ni Kuhudhuria madras
Waislamu wao kwa wao mtu akisoma sana wanaanza kumuonea wivu kuwa kakengeuka na anataka kuwa kaffir.......Mimi Kuna dada yangu alisoma mpaka chuo sasa ule mtaa mzima hakuna binti wa Rika lake ambaye aliwahi kusoma vile na wengi wao waliposwa mapema sana kwa kisingizio cha dini......walianza kumuandama eti kwanini haolewi na umri amefikisha wa kuolewa,Kuna imaam wa msikiti akataka amuowe kama mke mdogo,dada akagoma aiseeh!!! Kilinuka ikabidi atoke zenj aje bara na mpaka anamaliza chuo hakuwahi kurudi........Aliolewa na Muikristo.
Waislamu hawataki kutoa nguvu zao kwenye mambo ya elimu kama wafanyavyo kwenye Dini pamoja na ndoa.........Unaweza ukafaulu kwenda vidato vya juu kielimu lakini watakao kuunga mkono kimawazo au kiuchumi ni wachache lakini ukitaka kuoa au kuolewa utaungwa mkono na Jamii nzima..........Waislamu wenyewe hawataki kujenga Skuli au Hospitali zao wenyewe kama wafanyavyo Wakristo,lakini ukipitishwa mchango wa kujenga Msikiti au kumlipa mwalimu wa madras pesa uwa yapatikana muda huo huo
Elimu ndio kila kitu ndugu zangu Waislamu .....Jamii ya wajinga ni rahisi sana kuwadanganya na kuwatawala, ndio maana tulishindwa kumtoa Sultan wenyewe mpaka tukasaidiwa na John Okello(Muikristo mmoja anawaongoza wazenj milioni 3 kudai kupigana vita)..... .....leo hii mikoa maskini ya Waislam ndio maskini sana kuliko ata ya Wakristo