Waberoya
Platinum Member
- Aug 3, 2008
- 15,168
- 10,810
Tunasubiri Lissu aje na suluhisho!
ashajizika
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tunasubiri Lissu aje na suluhisho!
Nakubaliana na wewe watu wengi ni maimla sema hawana mamlaka lakini ni vyema kujitazama kwenye kioo ili kujiangalia vyema yale unayoyafanya.My point is i support mama sana, kwa mengi. Najaribu kukueleza kuwa kama ni dictatorship hata nyumbani ipo, kila mahali ipo, hata sometimes kazini kwako ipo, ila ni ile ya kubring changes
Katika yote aruhusu watu kusema aendelee kusimamia UHURU NA HAKI.Mama yupo vizuri and I wish her the very best ila ni swala la muda tu kabla hawajaanza kumpiga vitu. Sisi ndo wamatumbi tunakupenda mwanzo tu, usipotuletea ugali mezani tunaanza kukuchukia.
Ni kweli kabisa. Tutegemee mengi kubadilika. Inaonekana alikuwa hana namna ila alikuwa hakubaliani na Magufuli kwa mengi. Siyo yeye ila CCM ni wengi walikuwa wanaugulia kichinichini.Kama Tanzania ingekuwa ni simu tungesema mama kaonyeza command ya FACTORY RESET.
Yaani MAUJINGA yote Magufuli anayafukia kwa lugha laini bila chuki, husda wala matusi.
Sasa kama uliahidi kuleta ugali mezani na usilete mpaka mikono inakauka unadhani ni kwanini tusikuchukieMama yupo vizuri and I wish her the very best ila ni swala la muda tu kabla hawajaanza kumpiga vitu. Sisi ndo wamatumbi tunakupenda mwanzo tu, usipotuletea ugali mezani tunaanza kukuchukia.
Matagaaaa[emoji23][emoji23][emoji23]Tunasubiri Lissu aje na suluhisho!
Akifanya vizuri tunamuunga mkono akiharibu tunamshukia kama mwewe,yaani iko hivyoIla rais yoyote huanzaga vizuri sana. Ndio maana kina zitto wamejifunza kitu, hawakurupuki kusifia ila wanamcheki kwanza...
Huyu ni kumuombea ile timu isimuingilie...
Jambo hili namwomba Mungu ili ampe Hekima ya kukabiliana naloRais sasa ameonesha njia katika namna ya kukabiliana na tatizo la Covid 19 kisayansi akisisitiza kuwa Tanzania sio kisiwa, kwa hili tunamshukuru sana kwasababu ni wazi sasa tunaenda kubadili taswira yetu KIMATAIFA kwenye kukabiliana na changamoto hii inayoikabili Tanzania.
Suluhisho la nini. Alishatamka haya anayosema Mama Samia ila kwa sababu ya chuki mlidharau nq hata sasa unzkejeli. It is not fair. RAIS anawaumbuaTunasubiri Lissu aje na suluhisho!
Anamuumbua nani unavyoona!Suluhisho la nini. Alishatamka haya anayosema Mama Samia ila kwa sababu ya chuki mlidharau nq hata sasa unzkejeli. It is not fair. RAIS anawaumbua
Wa mbugani[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]Matagaaaa[emoji23][emoji23][emoji23]
Maneno yamekauka!ashajizika
Utajua mwenyewe!sipo
Akili yako utakuwa umeikabidhi kwa Zitto akicheka ndo na wewe utacheka sioIla rais yoyote huanzaga vizuri sana. Ndio maana kina zitto wamejifunza kitu, hawakurupuki kusifia ila wanamcheki kwanza...
Huyu ni kumuombea ile timu isimuingilie...
6 April 2021Wanajukwaa habari zenu,
Ni siku nyingine baada ya mapumziko marefu ya Pasaka, kama tunavyofahamu leo kulikuwa na zoezi la kuapishwa Makatibu na Manaibu Katibu wa wizara mbali mbali, pamoja na wakuu wa mashirika na taasisi mbalimbali.
Baada ya zoezi la uapisho zilifuata salamu kutoka kwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na baadae ikafuatia HOTUBA ya Mh. Rais, hotuba hii imekuwa ni kusimumua sana kwasababu imejikita katika kutoa dira ya Mh. Rais katika kutatua matatizo mbali mbali ikiwa ni:-
Kusisitiza matumizi ya AKILI badala ya "MISULI" nafikiri hapa Mh. Rais alimaanisha MIGUVU na hasa kwa kuendelea kuwasisitiza TRA kuhakikisha wanakusanya kodi bila ya kuwaumiza walipa kodi.
Rais sasa ameonesha njia katika namna ya kukabiliana na tatizo la Covid 19 kisayansi akisisitiza kuwa Tanzania sio kisiwa, kwa hili tunamshukuru sana kwasababu ni wazi sasa tunaenda kubadili taswira yetu KIMATAIFA kwenye kukabiliana na changamoto hii inayoikabili Tanzania.
Uwekezaji, hapa kwakweli amezungumza UKWELI mtupu na ni vyema watu wenye dhamana katika suala hili kuhakikisha wanafanyia kazi kwasababu hawa wawekezaji ndio ambao watasaidia katika kukuza ajira na kuipunguzia mzigo mzito serikali ya kuajiri. Hapa ni muhimu kuondoa urasimu ili kuweza kurudisha imani kwa wawekezaji si vizuri kusema Private sector haikupewa uzito inaostahili hapo nyuma lakini ni vyema kuanzia sasa tukawa na kiu ya kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.
Uhuru wa kwa vyombo vya habari, huu ni mwanzo mzuri kwasababu kukiwa na uhuru katika vyombo vya habari hii itampa nafasi ya kuweza kufahamu namna watendaji wake wanavyofanya kazi, wanasema Vyombo vya habari ni "Mhimili wa nne" katika serikali kwasababu ni wazi itakuwa ni rahisi kwake Rais kufahamu kwa uwazi mambo ambayo ingekuwa ni vigumu kwake kupata taarifa kwa wakati.
Kupitiwa upya kwa mitaala ya elimu, hapa ni kweli tunahitaji elimu ambayo itakuwa na msaada kwa vijana wengi wa Tanzania kwasababu elimu tuliyonayo sio siri hamuandai kijana kujiari bali kuwa muajiriwa ni kweli hapa tunahitaji mabadiliko ambayo yataenda kuleta suluhisho katika elimu ya Tanzania.
Kwakweli ni mambo mengi na ya umuhimu aliyoyaongelea kuweza kuayaandika hapa yote si rahisi sana ila ni hotuba yenye matumaini makubwa na kama watendaji watakuwa wamemsikiliza kwa umakini na kuyafanyia kazi basi tunaweza kuanza enzi mpya kwa mafanikio makubwa sana.
Niwatakie heri tunapoenda mapumziko ya Karume day.
Asanteni sana.