KERO Hatuelewi nauli rasmi ya usafiri wa umma Arusha - Moshi ni sh ngapi? LATRA toeni ufafanuzi

KERO Hatuelewi nauli rasmi ya usafiri wa umma Arusha - Moshi ni sh ngapi? LATRA toeni ufafanuzi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Baadhi ya wasafiri wanaotumia usafiri wa umma katika njia ya Arusha – Moshi – Arusha tumekuwa tukikumbana na changamoto kuhusu utofauti wa bei ya nauli inayotozwa na watoa huduma.

Katika nyakati mbalimbali, imeonekana kuwa baadhi ya abiria hutozwa nauli tofauti, huku viwango vikibadilika kati ya Shilingi 4,000 hadi 6,000 kwa safari hiyo.

Kutokana na hali hiyo, tunaomba ufafanuzi kutoka kwa LATRA kuhusu nauli rasmi iliyopangwa kwa njia ya Arusha – Moshi – Arusha.

Ni muhimu kuwepo kwa uwazi kuhusu viwango halali vya nauli ili abiria wajue haki zao na kuhakikisha watoa huduma wanatoza bei inayokubalika kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa.
 
Back
Top Bottom