Iran hakufanya shambulizi la uoga la kushtukiza kama afanyavyo Israel huko Lebanon, Syria nk.
Kwanza kwa kujiamini walitoa taarifa mapema huku wakijua fika taarifa hizo zitawapa nafasi Israel na washirika wake wajipange kulizuia.
Pili baada ya kuona Israel na washirika wake wameshajipanga kuzuia akafungulia bomba ili aone panapovuja. Na kweli ikabainika kuwa vifaa vyao vyote vya kuzuia vinavuja. Maana Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ujeruman, Jordan, Saudi Arabia na Israel yenyewe walianza kuzuia kuanzia Iraq, Saudi Arabia, Syria, Jordan nk, lakini mzigo umepita kilometres zaidi ya elf 2000 hadi katika nchi husika.
Sasa jiulize kama Iran isingetoa taarifa au Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Jordan wasingeisaidia kuzuia hali ingekuaje.