Wengi hamjaelewa hapo kuna hali kadhaa zinatokea.
Mwanamke aliyeolewa akiwa hana kazi kabisa ,huyu kufanya kazi hata yeye ataona ni sawa kwa vile hawezi kukaa tu bila ya kazi utakuta anajishughulisha wengine kufua kila baada ya siku kadhaa ,mara kupika,kufagia uwanja yaani binafsi ni asili ya binadamu kujishughulisha ili mwili ukae sawa.
Tuje fungu la utandawazi hawa wale wanaofanya kazi kwa wale walioa watumishi ,mke anatoka nyumba saa 2 asubuhi anarudi jioni hapo nyumbani nan atapika ,atafagia asubuhi na mchana? huoni hapa kiuhalisia unatafuta mfanyakazi ili umlipe kwa shughuli hizo ambazo angefanya mke....Sasa mnakataa maneno hayo wakati ndo yale yale tu kawaida.