Hawa Feminist walipofikia ni pabaya sasa

Hawa Feminist walipofikia ni pabaya sasa

Kinyonga01

Member
Joined
May 22, 2023
Posts
85
Reaction score
295
"Moja ya ukatili ambao wanawake wanafanyiwa ni kufanyishwa kazi majumbani bila kulipwa, kiuhalisia mwanamke anapofanya kazi za nyumbani lazima alipwe, kwasababu hujamuoa awe house girl wako, yule ni mke wako ambaye umemuoa kwa malengo maalumu na siyo ya kufanya kazi za nyumbani."

"Sisi kama wanaharakati tupo kwenye mchakato kuhakikisha ule muda ambao mwanamke anautumia kufanya kazi za nyumbani uwe na manufaa kwake, alipwe na mume wake."- Shamira Mshangama, Mwanaharakati.

Wamefikia stage mbaya sana aloo.
[emoji174][emoji23][emoji23]
1691657674404.jpg
 
Hapo zamani mambo hayakuwa hivi ila kuiga western culture imefanya yawe hivi. Ukitaka ku prove hilo angalia role za wenzi ambao wapo kwenye ndoa kongwe mtaani kwako.
ilibaki kidogo yale mambo yaanze kushikiwa bango kama haya ya haki sawa ila naona yamekutana na resistance ya maana.
 
Wengi hamjaelewa hapo kuna hali kadhaa zinatokea.

Mwanamke aliyeolewa akiwa hana kazi kabisa ,huyu kufanya kazi hata yeye ataona ni sawa kwa vile hawezi kukaa tu bila ya kazi utakuta anajishughulisha wengine kufua kila baada ya siku kadhaa ,mara kupika,kufagia uwanja yaani binafsi ni asili ya binadamu kujishughulisha ili mwili ukae sawa.

Tuje fungu la utandawazi hawa wale wanaofanya kazi kwa wale walioa watumishi ,mke anatoka nyumba saa 2 asubuhi anarudi jioni hapo nyumbani nan atapika ,atafagia asubuhi na mchana? huoni hapa kiuhalisia unatafuta mfanyakazi ili umlipe kwa shughuli hizo ambazo angefanya mke....Sasa mnakataa maneno hayo wakati ndo yale yale tu kawaida.
 
Back
Top Bottom