Hawa jamaa wa Iringa chini ya Producer Ambha walitisha sana

Hawa jamaa wa Iringa chini ya Producer Ambha walitisha sana

kwa-muda

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
2,097
Reaction score
5,348
Ambha anadai kwamba alifanya production lakini hakutoboa akawa ameamua kufunga studio aachane na muziki maana nyimbo zilikuwa hazipigwi na hapati fedha. Sasa akiwa ashaamua kufunga studio, asubuhi kalala kaja yaki anamgongea dirishani anamwita ambha aamke kuwa kaja na faridah anataka wakarekodi. Kama mnakumbuka zama hizo faridah alikuwa ni msanii wa kike ambaye nyimbo zake kama pesa zilikuwa ikipigwa sana RFA ambayo ilikuwa kwenye peak zama hizo.
Basi ambha kusikia farida akaamuka na kwenda studio na yaki na farida ndipo wa karekodi wimbo unaitwa we ni wangu ulikuwa na beat ya crank na crank ndiyo ilikuwa mainstream.
Baada ya hapo akarekodi hits kibao hadi wasanii wakaanza kutoka dar wanamfuata iringa. Moja ya msanii aliyefanya ngoma naye ambazo mpaka leo nazikubali ni Rama Dee ambapo alifanya naye ngoma inaitwa kikao cha family na ngoma nyingine. Ambha anadai ngoma za rama dee zilikuwa zimejaa back vocal zake mwenyewe na rama dee alimkubali jamaa jinsi alivyokuwa anapika nyimbo zake.
Ila kati ya vijana ambao alifanya nao ngoma zikahit kutokea iringa ni yaki, roho saba, na vijana wengine.

View: https://www.youtube.com/watch?v=H6MWWxMkDhM&list=RDH6MWWxMkDhM&start_radio=1

View: https://www.youtube.com/watch?v=PihvQOA_gxo

View: https://www.youtube.com/watch?v=chdP7c91Qs4
Lakni my favorite ni yaki ya tonight.
 
Hata zingepigwa sana bado studio isingemlipa. Producer huwezi kupata pesa bongo sababu wengi wanarekodi bure

Kaza fuvu uanze kulipisha uone kama utamaliza hata mwaka kama hujafunga hiyo studio.
yeye alitaka ngoma zipigwe asikike kuwa ni mtayarishaji atengeneze hata pesa kidogo kitu ambacho alikuwa amekosa. Ila baada ya hapo wakaanza mfuata, na mwisho alitengeneza almost nusu ya album ya ambwene ile ya gospel ya nguvu ya msamaha
 
Back
Top Bottom