Hawa ndio Wabunge waliopita bila kupingwa (2020) ambao Mahakama imesema ni batili

Hawa ndio Wabunge waliopita bila kupingwa (2020) ambao Mahakama imesema ni batili

Pole zao waje mtaani Mambo yalishabadilika unga Bei juu mchele Bei juu mafuta kupikia bei juu
 
Wabunge waliopita bila kupingwa
Wataalamu wa sheria wanasema the law is not retrospective sijui hapa itakuwaje, ngoja waje. Pascal Mayalla

Pia soma > Mahakama Kuu: Kutangaza Washindi wa Uchaguzi waliopita bila kupingwa ni Kinyume cha Katiba
Sheria yetu ya uchaguzi sio tuu ni sheria mbovu bali pia ni sheria batili!. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!

Maadam Mama kakubali kuifumua, yaliyopita sii ndwele, tugange yajayo ya 2025!.
P
 
covid ni malaya wa
Heshima kitu cha bure!. Usitukane watu malay. Unless una uthibitisho wanafanya ile biashara!.
nduli magufuli
Shujaa wetu usimuite nduli!, nduli ni mmoja tuu, Iddi Amini Dada!.
na yule mwenye ukimwi
Huu ni unyanyapaa!.
na mental disorder ndugai.
Huu ni ugonjwa kama magonjwa mengine yoyote!, sio busara kuwatukana violence wetu!.
P
 
Wabunge waliopita bila kupingwa (2020) na majimbo yao kwenye mabano.

1. Hamis Kigwangalla (Nzega Vijijini)
2. Kassim Majaliwa (Ruangwa)
3. Nape Nnauye (Mtama)
4. Vita Kawawa (Namtumbo)
5. Sagini Abdallah (Butiama)
6. Alexander Mnyeti (Misungwi)
7. January Makamba (Bumbuli)
8. Elias Kwandikwa (Ushetu)
9. Job Ndugai (Kongwa)
10. Ahmed Shabiby (Gairo)
11. Palamagamba Kabudi (Kilosa)
12. Jonas Van Zeeland (Mvomero)
13. Kalogereris Innocent (Morogoro Kusini)
14. Taletale Hamis Shabani (Morogoro Mashariki)
15. Eng. Isaack Kamwelwe (Mlele)
16. Geofrey Pinda (Kavuu)
17. Philipo Mulugo (Songwe)
18. Zedi Jumanne (Bukene).

Wataalamu wa sheria wanasema the law is not retrospective sijui hapa itakuwaje, ngoja waje. Pascal Mayalla

Pia soma > Mahakama Kuu: Kutangaza Washindi wa Uchaguzi waliopita bila kupingwa ni Kinyume cha Katiba
Kwanza, kwenye hiyo list, umemsahau Deo Mwanyika - jimbo la Njomve mjini.

Mimi siyo mwanasheria, lakini inaposemwa kuwa sheria siyo retrospective inamaanisha kuwa leo ikitungwa sheria mpya ambayo kabla ya sheria hiyo mpya tendo fulani halikuwa kosa, na sheria mpya sasa imelitaja tendo hilo ni kosa, basi wale waliolitenda tendo hilo wakati siyo hatia, hawatakuwa na hatia.

Lakini hiyo ni tofauti na mtu kutenda kosa, na kwa sheria zilizokuwepo wakati anatenda kosa lilikuwa ni kosa ila tu tafsiri haikuwa bayana, hapo lile zuio la kwamba sheria siyo retrospective haliwezi kufanya kazi.

Hivyo baada ya tafsiri na hukumu hii ya mahakama, wabunge hawa wote ambao hawakuchaguliwa na mtu yeyote, ni batili, siyo wabunge tena. Baada ya hapa, inatakiwa Tume ya uchaguzi kwa kushirikiana na Bunge, iandae utaratibu wa namna ya kuwaondoa wabunge hawa batili na kuwapata wabunge wengine walio halali kwa mujibu wa sheria.
 
Ilikuwaje wakati mwenyekiti wa nec ni jaji? Au yeye ni tofauti na majaji wa mahakama kuu waliotoa hukumu hiyo?!
Kuwa jaji au mwanasheria ni sawa tu na fani nyingine:

Kuna madaktari wazuri na wabaya

Kuna walimu wazuri na wabaya

Kuna madereva wazuri na wabaya

Kuna wahandisi wazuri na wabaya

Kuna wanasheria wazuri na wabaya, na wapo waliopewa ujaji ambao ni majaji michongo.
 
Back
Top Bottom