Hawa ndio wanawake wetu wasomi, bado hatuelewi nini wanataka

Hawa ndio wanawake wetu wasomi, bado hatuelewi nini wanataka

[emoji122][emoji122][emoji122]
Tatizo dada zetu siku hizi wameota mapembe, akili zao ni kutaka kupindua meza, wawe watawala katika nyumba na kichwa cha familia.
Wanataka waende kinyume na agano la Mungu mwisho wake wanaangukia kwenye agano la shetani.

Hao wanaume wenyewe vichwa vya familia unawaona?

Kama wapo ni wa kuhesabika[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Germany former chancellor, angela markel, ameolewa, alikuwa mkuu wa taifa lenye uchumi mkubwa europe, na alikaa madarakani miaka 16, na bado ako poa na mume wake, sasa hao wetu wa bongo na tujivisenti twao, wanajiona wakuu sana, hawana lolote,ni ujinga tu kufikiria hela tu ndio inahitajika, mtoto anataka kuwa na mama na baba,huyu nurse single mother aliwekwa mimba katupwa, sasa anamulisa wenzie poison, , naibu raisi wa marekali, kamalla harris ameolewa, hao wetu wa bongo ni upubavu tu
 
Maneno aliyoongea Mungu kwa hasira
Adamu - Utarudi mavumbini
Eva - Mumeo atakutawala

Haibadilishiki wala haikanushiki siku zote mwanaume ni kichwa cha familia na kiongozi wa mke wake na familia. Haijalishi kama huyo mke ni msomi au lah.

so beautiful.....
 
Kuna ticha mmoja ni rafiki wa mke wangu. Huyu ticha kaolewa ila wanaishi mikoa tofauti na mume wake. Jinsi wanavyopiga stori na mke wangu lengo la ticha ni kupata watoto wawili kisha aachane na mume wake.

Anachojivunia na kuona hana uhitaji na mume ni kwa vile tu ni muajiriwa huko serikalini, anasema ajira yake ndio mume wake.
Anamwambia mke wangu kwamba nyinyi msio na ajira ndio mynenyekee waume zenu,kwa hiyo mke wangu angekuwa na ajira huyu ticha angemshauri upumbavu wake anaowaza. Ipo siku huyu ticha inabidi nimchane.
Yani aje kupiga story kwangu kisha aanze kumshawishi mke wangu huo ijinga? Nisingesubiri chochote, namfukuza live kabisa "Toka kwangu nisikuone umekanyaga hapa" na mke wangu nakaa nae chini tunaongea vizuri kisha nampiga mkwara wa nguvu "nikikuona na huyo rafiki ako utahamia kwake"

Kama hauwezi kuwa mkavu hivyo, kuna njia nyingine ya kuwatenganisha. Mtongoze huyo mwalimu au onyesha nianya kumtaka kimapenzi kisha ruhusu mke wako ajue, hapo lazima urafiki ufe.
 
Wasaalam

Wakuu,

Leo asubuhi nilidamka mapema , wakati huu nilikuwa natoka kibaruani wakati najongea mdogo mdogo nyumbani nikapanda hewani nikampigia Mama, naam mama daVinci XV ,Nilimpgia asubuhi kwa sababu Mosi , ni Mila na Desturi zangu kumtaka hali kila uchao lakini pili nlitaka kuchota machache kuhusu siri nyingine zaidi na zaidi juu ya mwanamke ikiwemo yeye kuishi na Mzee wangu mpaka hivi sasa licha ya misuko suko ya ndoa na mahusiano.

Lakini Nikamuuliza pia kuhusu Mama mkubwa ambaye anaishi na Mzee wetu(bamkubwa) mpaka hivi sasa., nlimuuliza kuhusu mama mkubwa kwakuwa ni mwandani wa mama katika watoto wote wa Bibi yetu.

Kama ilivyo desturi ya Mama kuanza kunipa masomo kadhaa wa kadhaa juu ya mahusiano na maisha kwa ujumla huku Uvumilivu ikiwa silaha kubwa nayotakiwa kuishika mkononi na sio kuiweka mgongoni
Wakati wote Huu mama alikuwa na wasiwasi akidhani pengine nimekhitilafiana na mkamwanawe.(mpenzi wangu)

Baadaye nikarudi kulala nikijichekea nafsini mwangu kuhusu hii dunia yetu ya wanawake wasomi.

Ilikuwa hivi nilichukua uamuzi wa kumpandia hewani bi mkubwa kwanza hii ni desturi yangu kumtaka hali kila asubuhi kwakuwa tuko mikoa tofauti pili , ni kuongeza notes kidogo juu ya machache katika maisha hii ni desturi yake mama kutoa notes kila inapobidi.

Usiku wakati nipo shift ya Usiku , baada ya kumaliza majukumu yetu ya usiku , kwa kufanya medications na kufanya admission kadhaa na mengineyo yaliyotakiwa kufanywa., nlijongea taratibu kwenye kompyuta za Ofisi ili kupitia pitia kidogo yanayojiri katika ulimwengu wetu wa Urusi na Ukraine😅

Ni utaratibu wangu nikiwa night shift kusave bando langu na kutumia kompyuta za ofisi namaanisha simu itakaa kando kule.

WANAWAKE WASOMI
Pembeni kidogo walikuwa manesi (wote wanawake) ambao nlikuwa nao katika zamu ya usiku walishajitayarisha kwa ajili ya kupumzika, lakini walikuwa na stori chache kabla.

Mazungumzo yao yalikuwa ni matusi yanayofariji juu ya thamani ya wanaume kwa walezi huku wakisisitiza kuishi kama ma-single mothers .,huku mmoja akisimsititiza mwenzake zaidi.

Mie nikajifanya macho yangu yametaradadi na screen na nyoka EP ya jamal April lakini masikio na akili yangu bado vilikuwa juu ya maongezi ya wasomi hawa wawili., huu ni udodosaji ambao mwanaume sitakiwi kuufanya lakini masikio yaligoma kuisaliti mada hiyo iliyogusa vilivyo akili yangu.

Nikasema kutochukua notes chache kutoka hapo ingekuwa dhambi , dhambi nyeusi tii tii tii.

Huyu nesi mmoja ambaye alikuwa amezaa tayari alikuwa akimuelekeza mwenzie namna ya kuishi kama msomi (kwa mujibu wao)

Akawa anamuelimisha atafute mwanaume mwenye pesa tu azae nae kisha achukue mtoto wake,
yeye atulie tu na mtoto apambane naye hata akiachana nae iwe jukumu la mwanaume kama atahudumia au la asijishugulishe kuomba huduma ya mwanaume..lakini ni heri uzae na mwenye hela ili kama atakuwa na moyo wa kuhudumia mtoto wake basi mtoto apate huduma stahiki. Kuliko kuchagua hawa wanaume maskini wenzangu na mimi.

Akasisitiza mwanamke kutafuta pesa zake mwenyewe ili akomae kulea mtoto wake kuliko kufatisha Matakwa ya mwanaume., ambaye haeleweki mda wowote anaweza kukuacha hapa walisimamia wanaume wote ni sawa.,

Lakini hapa nikajiuliza kidogo mwanamke anataka nini zaidi?

hilo la kutafuta mwenyewe sawa tunalikubali , hatuhitaji mwanamke golikipa wa kusubiri kuletewa kila leo.

Lakini hili la kupigania usingle mother lilikuwa jambo jingine kwa hawa wasomi,

Ikanilazimu asubuhi kumuuliza bi mkubwa wangu kwa nini alidumu na mzee miaka yote. Akanimegea mengi. Kama ilivyo ada yake.

Lakini ukiachana na wanawake wa zamani kutokuwa na Elimu na kuwa wamama tu nyumbani nadhani kuna nyenzo nyingine iliyowafanya kudumu na waume zao hata sasa
Unadhani itakuwa nyenzo gani zaidi?
Hata hili naimani mama hakunichotea katika kile kitabu chake cha notes za siri za maisha.

Wanawake wetu wasomi wa sasa ambao pengine walitakiwa kuelimisha wengine juu ya namna ya kudumu na mwanaume ili kutoleta athari za mfarakano ambazo zinaweza kumjengea chuki mtoto juu ya mzazi wake mmoja.,ndiyo hao wanaopigania usingle mother. Wazae kisha wapambane na watoto wao wenyewe.

Huyu mtoto itamjengea picha gani kwa baba yake hapo badae CHUKI nyekundu isiyoweza kubadilika kuwa nyeupe kama ya mzee nasibu na yule dogo wa Tandale.

Maisha ya mahusiano na ndoa yana siri nyingi,, lakini kwanini wimbi la wanawake wengi hawa wasomi hivi sasa ndio wanapigania usingle mother ,PESA , au ELIMU?

Halafu cha ajabu hata wanaokwenda kwa wanasaikolojia kwa minajili ya kupata cancellin masingle mother wengi wasomi basi idadi yao ni Lukuki hivi sasa.

Elimu yao na kipato kidogo kinawafanya kuchagua kuwa masingle mother lakini hawana furaha na upendo kama wa mama zetu wa zamani ambao hawakuwa na Elimu wala vijisenti kama vya hawa wasomi wetu wa sasa.

Wanawake hawa ndio wanaongoza kuishi kwa visirani na sonona .

Wanawake wetu wanataka nini zaidi?
tafuta hrla ........
 
Every woman needs a man.
Usingo maza ni matokeo yasiopendeza. Hata huyo singo maza hakupenda kuwa hivyo. Mwanamke anafurahi sana mtoto akilelewa na baba yake, huku yeye (mwanamke) akiwa ndio mwangalizi mkuu wa mtoto.

They get stressed when they are not married.
 
Every woman needs a man.
Usingo maza ni matokeo yasiopendeza. Hata huyo singo maza hakupenda kuwa hivyo. Mwanamke anafurahi sana mtoto akilelewa na baba yake, huku yeye (mwanamke) akiwa ndio mwangalizi mkuu wa mtoto.

They get stressed when they are not married.
Kabisaaa
 
Acha ukuda, mchane sasa. Wa wapi we jamaa mbona unaonekana mshamba mshamba sana
Mimi anatokee mwanamke mpumbavu hivi kwenye tabia za kikuda kama huyo kuongea na mke wangu ujinga nimwangalie tu eti nitamchana baadae! Yule ni pale pale namchana! Utakuja kushitukia na mkeo ameshatafutiwa bwana mwingine! Maana tayari huyo mwanamke ni malaya kwa maongezi yake tu!
 
Huyo nesi aliyekua anamlisha sumu mwenzie..ni kwamba yeye aliingiaa chaka bovu..ss anajaribu kumdanganya na mwenzie asikubali kuolewa wakati ndoa haziko sawa...HIYO NI SUMU MBAYA SANA ANAMLISHA na kumpotosha...

Ila nikwambie deep down huyo nesi alitamani na yeye awekwe ndani..hakuna mwanamke hapendi kuhudumiwa kutunzwa au hata kupendwa...never....
Wengi wanaokimbilia kujizalia tu ni walishaktaaa tamaa anaona bora apaate watoto basi alee..maana ukute kwa tabia zake au sababu zingine zingine watu wanamkimbia......

Alichokua anamshauri mwenzie ni kumharibu na km ni bint mdogo basi anamshawishi adange mpk apate bwana mwenye hela amtegeshee mimba azae...haya atazaa na wangapi....stupid mind set

Usinglr mother unatakiwa uje tu automatically kwa mipango ya Mungu sababu sio kila mtu anapenda kutelekezwa

Ila huo usingle mother wakujitakia ni uboya...

Wazazi wetu wamedumu sababu walijua kuvumiliana ..kizaz chetu si wanaume wala wanawake wanaweza kuvumiliana..kosa kidgo kashaondoka kwao..kosa kidgo keshafukuza mke kaoa mwingine...

Ila wazaz qwtu walijikaza....angalia familia ambazo wazaz wamelea wawili..watoto angalau wanastawi...lkn familia nyingi ambazo zina talaka u akuta kidg ht malezi na tabia za watoto zinayumbA

Sasa nawaza sisi kizaz cha wasomi..miaka ijayo wToto wetu hawa sijui watakuaje..Mungu atusaidie

Mimi huwa namuomba Mungu anisaidie nilee watoto wangu kama nilivyolelewa mimi na wazaz wangu..angalau tu nitengeneze kiazaz chenye staha.na malezi mazuri (kifupi wanangu wawe kama mimi).
Nisingetaman wawe tofauti...kisa tu wazaz tuko busy ..kukosa upendo etc etc

Naandaa matiliobya kujengea sanamu lako dada[emoji1488][emoji1488]unataka likae wapi??
 
Back
Top Bottom