Wengi wamechoka, Mpira kipindi hicho haukuwa biashara kama sasa so wengi wapo mtaani Tu, Mimi nimekuwa mtaani Karibu kabisa na walipokuwa wanakaa Peter Tino, Gebo Peter na ndogo wao anaitwa Emma Peter, hii familia yote ilikuwa ina damu ya Mpira, Ila daaah, inasikitisha maana kuna wakati nilikutana na Emma Peter, kachoka kachakaa hata sijui wapo wapi sasa.
Kuna siku nilikutana na Kenneth Mkapa Arusha alikuwa poa kabisa tena tulikutana tizo asubuhi pale Sheikh Abeid, wapo wengine waliona mbali wakajiendeleza na ukocha, biashara kama Minziro,Jamhuri Kiwelu, Jamhuri alikuwa na mdogo wake anaitwa Mtwa Kiwelo sijui yupo wapi sasa, Ila ipo haja iandaliwe documentary moja kuhusu kile kizazi, nafikiri itakuwa poa Sana.