Hawa ndo watanzania Elimu yao haijaleta Impact yoyote katika nchi wala katika taasisi walizoziongoza

Hawa ndo watanzania Elimu yao haijaleta Impact yoyote katika nchi wala katika taasisi walizoziongoza

Uprofesa wa majalalani kaole sana, ndo maana msukuma huwa anawaponda sana lakini anaonekana ana wivu kwavile hajasoma lakn si kweli.
 
Unafahamu Prof Kabudi ana Publications ngapi? citations ngapi? Supervisions za Masters na PhD ngapi? Consultations ndani na nje ya nchi ngapi? Fanya utafiti ndipo uje kuandika kitu, vinginevyo usilete usela gogo kwenye ulimwengu wa ki intellectual.
 
Elimu ya bongo ni intimidation ,mtu akikosa teuzi anaanza kulia ..Yule T.O kutokea kusini ,kelele zote mtandaoni ,umotivational speaker kumbe anataka ubunge ....Jamani ,jamani elimu hii ukisikiza wanavyongelea neno '' elimu '' utachekw
 
Elimu ya Tanzania kimeo sana kuna jamaa kasoma SUA sijui diploma au degree sijui lakini kaja mtaani tukijuasasa sisi wakulima na wafugaji tutapata auheni yaani ushauri wa kitalaamu. Badala yake akaanza moja kujifunza kunyoa baada ya muda akafungua saloon yake na sasa ananyoa vichwa ukimwambia kuhusu kilimo hakuna anachojua hadi a google!!

Mwingine aliletwa na mzee wangu shambani kwangu tena huyu ni bwana shamba wa kata kabisa analipwa na ana pikipiki alichonishauri nilishangaa mno na mara ya kuondoka nilimwambia mzee usimlete tena huyu wala msimtumie kwenye mashamba yenu.
 
Ikiwa huna taarifa za kutosha kuhusu wasifu wa mtu, si vyema kutoa shutuma au kuwachafua hadharani kwenye jukwaa hili.
 
Unafahamu Prof Kabudi ana Publications ngapi? citations ngapi? Supervisions za Masters na PhD ngapi? Consultations ndani na nje ya nchi ngapi? Fanya utafiti ndipo uje kuandika kitu, vinginevyo usilete usela gogo kwenye ulimwengu wa ki intellectual.
Hakuna cha maana hapo Kenya maprofesa wao wanafundisha University za USA wanavuta na Michongo kuleta Kenya unafanisha hizi takataka zinazovizia TEUZI mtu anafika level ni Profesa wa Uchumi hana hata kibabda cha kuuza mkaa hajawai kugundua Chochote hao ni kenge tu
 
Prof -Lipumba huyu nilianza kumfatilia mwaka 2005 huyo hana alichoisaidia nchi wala taasisi yake ya CUF.

Prof -Muhongo , huyu anaingia katika kundi hili ukiachana na Scandal Kama Escrow n.k sijaona Kama kuna kitu kafanya jimbo lake ni moja ya majimbo masikini Sana Tanzania .

Prof Tibaijuka , huyu ukiacha Ku-brag n.k Elimu yake haina impact yoyote kuanzia kule kwao Muleba ambako wale wadada wauza stake wanatoka kashindwa hata kubadilisha mindset zao ili waache kuuza stake.

The list is endless Ila nikiwasikiliza wasomi wa Tz huwa nacheka Sana ukiachana uwezo wa kukariri madesa sijui Kama kuna kitu wanaweza.


Kuna mzungu mmmoja alimwambia mtanzania kuwa nyie ni mabingwa wa kukariri Ila kufikiri hilo swala hamliwezi hata kidogo.

Hii ndo maana watanzania baadhi wakienda kusoma ulaya wanafanikiwa kupata good marks ila kufikiri kitofauti hawawezi.
Katika wote hao umemuonea Prof Anna.
Prof Lipumba hana impact anapotoka hata katika jamii pana aliyopo au ndani ya chama chake; amekua mchumi wa kwanza duniani kung'ang'ania uenyekiti badala ya kutumia elimu yake kuisaidia jamii.

Kwa upande wa Muhongo kule Musoma kijijin bado hali ni ngumu; Anajitapa yeye ni mwanageologia lakin basi angewasaidia hata wananchi wa kanda yake kupata taarifa za kijiogolijia ili waweze kuchimba madini katika maeneo ya Bunda( kinyambwiga), Serengeti, na Tarime maeneo ya kewanja, genkuru nk.
Prof Tibaijuka: sijajua kwa upande wa huko Kagera alichokifanya lakin kwa ufaham wangu mdogo amejenga shule maeneo ya Kibamba ambayo inawasaidia watoto wanaotoka familia ngumu na za juu wanaopitia mazingira magumu...! Licha ya hayo amekua mkosoaji bila kusita au kuogopa ukilinganisha na hizo karabsha za juu.
Mimi namkubali na kama siku itatokea nitatamani awe mjukuu wake nipate madini zaidi.
Kuhusu hoja ya wadada wauza stake hata ww unaweza kuwabadilisha; kuuza stake ni mindset ya watu sio kabila kwan river side na viunga vyake wamejaa mpaka wachaga, waarabu na wazaramo nk ni kisu chako kukata stake.
 
Siasa Tanzania imetawala inaharibu kabisa elimu yetu, wanasiasa wanashirikiana na vilaza walioishia std 7 kudidimiza taaluma na elimu kwa ujumla

Kama elimu haifai tujaribuni ujinga tuone matokeo yake halafu turudi tukae mezani tupange tena
 
Hakuna cha maana hapo Kenya maprofesa wao wanafundisha University za USA wanavuta na Michongo kuleta Kenya unafanisha hizi takataka zinazovizia TEUZI mtu anafika level ni Profesa wa Uchumi hana hata kibabda cha kuuza mkaa hajawai kugundua Chochote hao ni kenge tu
Kwa kifupi,wewe hujui kitu. Hebu nitajie Andiko hata moja la Prof Kabudi, kama kweli unaona Hana impact. Hivi unajua kutoka Dr Hadi Prof unatakiwa uwe umefanyaje?
Kuhusu kugundua kitu si lazima uwe na PhD, hata level ya Masters inaweza kukufanya kuwa Scholar ..huwezi kugundua kitu pasipo kufanya utafiti (research) kwahiyo kuanzia Masters unapewa go ahead ya ku fill a research gap. Amka kutoka usingizini
Nchi yetu Ina tafiti za kutosha, lakini hazifanyiwi kazi pia wanasiasa wana channel pesa nyingi kwenye utawala badala ya kwenye tafiti.
 
Unafahamu Prof Kabudi ana Publications ngapi? citations ngapi? Supervisions za Masters na PhD ngapi? Consultations ndani na nje ya nchi ngapi? Fanya utafiti ndipo uje kuandika kitu, vinginevyo usilete usela gogo kwenye ulimwengu wa ki intellectual.
Hivyo vyote vinamsaidia nini maskini wa pale kilosa au tandale
Tofautisha personal achievement na impact uliyoleta kwenye jamii kwa ujumla
 
Back
Top Bottom