Hawa ndo watu wenye bahati duniani

Hawa ndo watu wenye bahati duniani

Hiyo ya kwanza ungefafanua zaidi.hiyo inategeme na ajira.kunawengine walichelewa kupata ajira Hadi wakaamua kujiajiri Hadi kuwazidi kimaendeleo waliomtangulia kuajiriwa.Mfano kwa ajira hizi ndogondogo kama mwalimu,polisi wanajeshi hawa wa vyeo vya kawaida hata akitangulia miaka kumi lakini ukaamua kujiajiri kwenye ufugaji na kilimo unawazidi kimaendeleo Kwa muda mfupi.Hii nimeiona Kwa watu wengi sana
True kabisa me naona kilimo hasa cha tumbaku watu wanapiga pesa mbaya.
 
Hii ndo list ya watu wenye bahati dunia:
1) Mtu aliyepata ajira mara tu baada ya kumaliza chuo/masomo
2) Mtu aliyezaliwa kwenye familia tajiri
3) Mtu aliyepata mpenzi/ mke/ mume sahihi kwenye mahusiano yake ya kwanza tu
4) Mtu ambae yupo carefree
5)... ongezea
Mtu aliye hai mpaka kufikisha miaka walau 85 ana bahati. Hao wengine wote ulioorodhesha kuna wengi wanafariki wakiwa vijana kabisa.
 
Dah yote hayo unanisema mimi kabisa japo kwenye upande wa familia sio matajiri kihivyoo..


Kingine mimi handsome boy mtoto wa kinyaturu /ki Ethiopia
Mnyaturu kweli unajisifia kuwa ww n Mnyaturu asee Miaka imekimbia sana šŸ˜€šŸ˜€šŸ˜€
 
sema watu waliopata mbeleko maishani

bahati ya pekee ni kua na afya njema dogo
 
Waebrania 10
Warumi 2:12-14

Soma :
Wakolosai 2:16-23

16 Kwa hiyo, basi, msikubali kupewa masharti na mtu yeyote kuhusu vyakula au vinywaji, siku za sherehe, sikukuu ya mwezi mpya au Sabato.

17 Mambo ya aina hiyo ni kivuli tu cha yale yatakayokuja; ukweli wenyewe ndiye Kristo.

18 Msikubali kuhukumiwa na mtu yeyote anayejitakia kuwa wa maana kwa sababu ya maono ya pekee na ambaye anasisitiza juu ya unyenyekevu wa uongo na ibada kwa malaika. Mtu wa namna hiyo amepumbazika kwa fikira danganyifu za kidunia

19 na amejitenga na Kristo aliye kichwa cha huo mwili. Chini ya uongozi wa Kristo, mwili wote unalishwa na kuunganishwa pamoja kwa viungo na mishipa yake, nao hukua kama atakavyo Mungu.

20 Nyinyi mmekufa pamoja na Kristo na kukombolewa katika nguvu za pepo watawala wa ulimwengu. Kwa nini, basi, kuishi tena kama vile mngekuwa wa ulimwengu huu? Ya nini kuwekewa masharti:

21 ā€œMsishike hiki,ā€ ā€œMsionje kile,ā€ ā€œMsiguse kile!ā€

22 Mambo hayo yote yanahusika na vitu vyenye kuharibika mara tu vinapotumiwa; hayo ni maagizo na mafundisho ya kibinadamu tu.

23 Kweli, masharti hayo yaonekana kuwa ya hekima kwa namna ya ibada wanayojishurutishia, unyenyekevu, na kuutendea mwili kwa ukali; lakini hayafai chochote kuzuia tamaa za mwili.
 
Hii ndo list ya watu wenye bahati dunia:
1) Mtu aliyepata ajira mara tu baada ya kumaliza chuo/masomo
2) Mtu aliyezaliwa kwenye familia tajiri
3) Mtu aliyepata mpenzi/ mke/ mume sahihi kwenye mahusiano yake ya kwanza tu
4) Mtu ambae yupo carefree
5)... ongezea
Number three (3) ukiikosa hata upate hizo nyingine Ni bure tu.
 
Kwenye mke sahihi Nina uhakika soon nakuwa na wife na mwenyewe mzuri.. Tatizo nataka nipate mshindo wa maana yaani hela kama ya Madini ile Vito nipewe million 140 Kwa Mara moja hapo ndo nitajiona nimepata BAHATI KUU
Duh
 
Nimekonda sana mkuu? Ndo mwili wangu mzee
Uko poa mbona mkuu kama mimi tuu sema macho ndio yanaonesha ni mla vyombo, mwanzo na mimi nilikua nakula vikali kila siku, watu wakaribu wakaanza kuniambia nimeanza kua na sura ya ulevi, nikaamua kupunguza vikali nakula mara chache tuu nikiwa na hela nakunywa bia basi.
 
Hii ndo list ya watu wenye bahati dunia:
1) Mtu aliyepata ajira mara tu baada ya kumaliza chuo/masomo
2) Mtu aliyezaliwa kwenye familia tajiri
3) Mtu aliyepata mpenzi/ mke/ mume sahihi kwenye mahusiano yake ya kwanza tu
4) Mtu ambae yupo carefree
5)... ongezea
Mtu anayepata hela ya Kubet
 
True kabisa me naona kilimo hasa cha tumbaku watu wanapiga pesa mbaya.
Mkuu acha kabisa, mwezi uliopita nilikua kahama tunakusanya tumbaku kwa wakulima vijijini huko aisee vijana wadogo wanapiga hela balaa, mind you tumbaku inanunuliwa kwa dollar.
 
Back
Top Bottom