Hatimaye BBC wameokoteza habari kuonesha kwamba hata bara la Afrika lilishawahi kutoa papa. Hii inaua hoja kwamba, safari hii Papa atoke Afrika. Ikiibuka hoja ya kutaka Papa Mweusi, tutasema huo ni ubaguzi wa rangi katika dini!
Habari kamili;
Afrika Kaskazini ambayo wengi wao ni Waislamu, wakati mmoja ilikuwa nchi ya dini ya Kikristo, ikitoa mapapa wa Kikatoliki ambao waliacha alama zao kwenye Kanisa hadi leo.
Upapa wao ulikuwa katika enzi ya Ufalme wa Kirumi, ambao ulienea katika Tunisia ya kisasa, kaskazini-mashariki mwa Algeria na pwani ya magharibi mwa Libya.
"Afrika Kaskazini ilikuwa Ukanda wa Biblia wa Ukristo wa kale," anasema Prof Christopher Bellitto, mwanahistoria katika Chuo Kikuu cha Kean nchini Marekani.
Wakatoliki wengi barani Afrika wanatumai kuwa upapa utarejea barani humo kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 1,500, huku mrithi wa Papa Francis akichaguliwa.
Chanzo; BBC Swahili