Hawa ni watanzania 10 chini ya umri wa miaka 50 walioleta mabadiliko chanya kwenye jamii kupitia vipaji na vipawa vyao walivyojaliwa

A. Hawa Watoke

4.Samia Suluhu - Kawapa waarabu Ngorongoro kawatimua wamasai, DP World walitaka kupewa bandari milele na hata huu mkataba wa sasa haijulikani.

7.Ruth Zaipuna, Hapa muweke Charles Kimei, ndie kaleta mapinduzi makubwa

8.George Waitara ( Ana mchango lakini golf ni mchezo wa watanzania wachache tena wale wanaoijiweza mno kiuchumi, mchango wake ni mkubwa lakini umegusa wachache)

9.John Joseph Pombe Magufuli (Huyu alianza kuleta ukabila na Ukanda kuipendelea kupita maelezo Chato, Aliminya sana uhuru wa kuongea yani hata kumiliki channel youtube uwe na milioni 2, Hakuweza kabisa kuvumilia wapinzani kama kina Tundu Lisu)

B. Hawa waingizwe

DIAMOND PLATNUMZ - Kafanya mapinduzi makubwa ya kimuziki, Kaleta chachu kwa wasanii kuwekeza na kufanya biashara, kaleta uhuru kwenye Media, Zamani ukikorofishana na Mtemi wa Clouds fm nyimbo hazisikiki redioni ila siku hizi kuna media nyingi

MAXENCE MELO - Kuanzisha jamii forums apongezwe lakini kuifanya iendelee kuwepo apewe maua yake, Kuna kipindi serikali ilikuwa inataka ip adress za watu wanaokosoa vuiongozi wakubwa ili waend tcra wajue namba za simu zinazotumika wakamate wahusika, Max aliwagomea kwamba ni privacy lakini haikua rahisi, aliwekewa kesi nyingi alinyanyaswa na polisi, n.k. Kuna kipindi ilibaki kidogo hii jamiiforums ifungwe, Kwa msaada wa wadau, vyama vya haki na balozi za nchi za nje aliweza kulinda privacy za watu humu ndani, Bila hivyo watu wangekamatwa sana humu ndani wangefungwa jela, kuteswa, na mambo kadhaa tuliyoona wakosoaji wakifanyiwa awamu ya tano. pia ni moja wa waasisi wakubwa wa mabadiliko yaliyofanyika kwenye muswada uliopitishwa bungeni wa Privacy za watanania mitandaoni.
 
Mkuu hadi Mo dewji?...tukatae tukubali huyu mtu ameleta evolution sana katika mpira wa kitanzania. Tukisema tuangalie kwa fields basi kama umemtambua samatta huna budi kumtambua mwakinyo kwenye boxing japo nidhamu yake sio kubwa
Hao ni mwendelezo Mo kaleta mabadiliko ila sio makubwa kiasi Cha kuathiri maisha ya watz kimsingi vibe la mpira lilikuwepo hapa nasemea zaidi wale walio pave the way eg Waitara kaifanya golf kuwa ya Kila mtu wengine wanashuka kwenye daladala na kuingia lugalo na kaiweka hadi kwa juniors hii siku za usoni itajenga national team
Rwakatare alianzisha shule za private kipindi ambacho watu hawaamini kama kusoma private ni big deal wengi waliamini private school ni kwa failure
 
namba 1,4 na 10 hapana,

diamond aingie anamuwakilisha kanumba kwenye tasnia ya burudani,mapinduzi ya media kafanya bakhresa group huyo mwengine hayupo,politics ya ubepari /uwekezaji ni mkapa huyo kikwete na samia wote waomba misaada nje.
Samia ni Rais wa kwanza mwanamke amejitahidi kiasi chake na anastahili pongezi
Kachukua nchi ikiwa imetoka kwenye kipindi kigumu ambacho kama nchi hatukuwahi kupitia (kupoteza rais akiwa madarakani)
Kulikuwa na madhara ya covid
Vita Ukraine n.k lakini kaweza angalau kidogo kutoa ajira kupandisha madaraja
Karuhusu siasa huru n.k amejitahidi angalau kaondoa Ile dhana kuwa mwanamke hawezi kuwa Rais
 
Hawa watoke

4.Samia Suluhu - Kawapa waarabu Ngorongoro kawatimua wamasai, DP World walitaka kupewa bandari milele na hata huu mkataba wa sasa haijulikani.

7.Ruth Zaipuna, Hapa muweke Charles Kimei, ndie kaleta mapinduzi makubwa

8.George Waitara ( Ana mchango lakini sio wa kuingizwa hii list)

9.John Joseph Pombe Magufuli (Huyu alianza kuleta ukabila na Ukanda kuipendelea kupita maelezo Chato, Aliminya sana uhuru wa kuongea yani hata kumiliki channel youtube uwe na milioni 2, Hakuweza kabisa kuvumilia wapinzani kama kina Tundu Lisu)
Kwa Waitara anachokifanya pale lugalo golf ni kikubwa sana
Zaipuna nimerekebisha na kumuweka Kimei
Magufuli tumuondoe akae nani ambae jamii inapaswa kuenzi mchango wake kwa mabadiliko
 
Samia ni Rais wa kwanza mwanamke amejitahidi kiasi chake na anastahili pongezi
Kachukua nchi ikiwa imetoka kwenye kipindi kigumu ambacho kama nchi hatukuwahi kupitia (kupoteza rais akiwa madarakani)
Kulikuwa na madhara ya covid
Vita Ukraine n.k lakini kaweza angalau kidogo kutoa ajira kupandisha madaraja
Karuhusu siasa huru n.k amejitahidi angalau kaondoa Ile dhana kuwa mwanamke hawezi kuwa Rais
kwani unapima kupitia jinsia au nafasi/hadhi yake?

mkapa aliipokea nchi kutoka kwa mwinyi kukiwa na wasomi wachache,viwanda vingi vimetelekezwa,na barabara mbovu.n.k
 
Nimemuweka Mkapa alijitahidi sana
Yah kwa Samia nimezingatia Gender hasa mabinti na jamii itamuangalia na kuona kuwa tunaweza mchagua mwanamke na akaongoza vizuri
 
Ni kweli kabisa kama no 4.
1. Kubinafsisha bandari kwa dp Woldi.

2.kuweka makato ya tozo kwa kila mtz kwa mitandao ya simu.

3.kununua kila goli la yanga na simba kwenye champions league kama motisha.

4. Kushiriki kwenye uzinduzi wa album ya msanii harmonize maarufu kwa jina la jeshi.

5 kuzindua kundi dogo almaarufu kama chawa kama motisha ya kazi kwa viongozi mbalimabali .

6. Kutoa movie inayohamasisha utalii kwa muongozaji maarufu wa movie duniani aitwae pita🥰.
 
Kwa Waitara anachokifanya pale lugalo golf ni kikubwa sana
Zaipuna nimerekebisha na kumuweka Kimei
Magufuli tumuondoe akae nani ambae jamii inapaswa kuenzi mchango wake kwa mabadiliko
Ni kweli Waitara anafanya makubwa lakini Golf ni mchezo wa watanzania wachache hasa wanaojiweza kiuchumi,

Heshima kwake mzee Waitara
 
Hapa kwenye wanaojiweza ndipo anapojitahidi kuondoa hiyo dhana kwa Sasa ukienda pale utakuta watoto wadogo wanaotoka familia za kawaida Wana train
Kwa muendelezo ule huenda miaka kadhaa mbeleni tukawa na golfers mashuhuri afrika
 
Hii ni orodha tukufu ya watanzania wenye umri chini ya miaka 50 walioweza kufanya mapinduzi makubwa kupitia jinsi walivyojaliwa na muumba.

1. ZITTO KABWE
Haina ubishi Zitto ndo aliamsha wengi kuona inawezekana kuwa mwanasiasa mkubwa mwenye umri mdogo tena kupitia upinzani. Zitto aliingia bungeni akiwa na miaka 29 kama mbunge wa kuchaguliwa kupitia CHADEMA mwaka 2005. Baada ya yeye vijana wengi waliingia kwenye siasa wakiwa wadogo na kufanya makubwa.

2. MBWANA SAMATTA
Huyu kijana hadi sasa ndo anashikilia rekodi ya mwanasoka aliyefanya makubwa zaidi kuwahi kutokea Tanzania. Ni namba moja karibu kwenye kila kitu. Kupitia yeye vijana wengi wamejua kila kitu kinawezekana hata kucheza EPL ukiwa mzaliwa wa Mbagala.

3. NASEEB ABDUL (DIAMOND PLATINUMZ)
Kama vile Samatta anavyoshikilia rekodi za kuwa mwanasoka aliyepambana na kuweka rekodi ambazo hazikuwahi kuwepo basi Diamond naye kafanya hivyo kwenye muziki. Kaamsha wengi sana.

4. MILLARD AYO
Huyu chalii wa Ara hakuna mtu atamwambia kitu oote kwenye biashara ya media. Mapinduzi aliyofanya kwenye media imesababisha kuwa na online media nyingi sana. Ni role model hado kwa wakongwe wa hiyo tasnia.

5. FRED NGAJILO (VUNJABEI)
Kimsingi Fred na mwenzie Frank Knows ndo kioo cha wajasiriamali wapya karibu wote. Ufanyaji wao wa biashara umeleta mapinduzi makubwa kwenye namna ya kufanya biashara hasa kwenye kipengele cha upangaji bei. Fred kabadili fikra za wajasiriamali wengi.

6. MamaSamia2025
Nikiwa kijana mdogo wa miaka 38 ninaweza kutamka wazi nina mchango mkubwa hasa hapa JF kupitia nyuzi na comments zangu. Nyuzi na comments nyingi hutumika kama mwongozo wa mambo mbalimbali.

7. LAUREL KIVUYO
Huyu binti ni mwanaharakati wa mambo ya mazingira. Ni graduate wa MUHAS. Katika umri mdogo sana wa chininya miaka 25 tayari kashashiriki mikutano mikubwa ya kimataifa ndani na nje ya nchi. Halafu ni wa kutoka Arusha na sio Chato.

8. JOKATE MWEGELO
Hakuna asiyemfahamu kidoti ambaye kwa sasa ni boss wa UVCCM. Kina Laurel wanafanya makubwa sana baada ya dada Jokate kuonyesha mfano.

9. JORAM MKUMBI
Huyu mzee wa ulumbi kaonyesha sio lazima iwe msanii au mwanasiasa ili kuleta impact kwenye jamii. Kupitia tu lugha ya kiswahili kaweza kuhamasisha raia kujifunza zaidi lugha yao. Joram ni mfano wa kuigwa.

10. LUCAS MWASHAMBWA
Huyu jomba anapigwa vita sana hapa JF ila wanaompiga vita ndo haohao wanamkubali mbaya mbovu. Kila akishusha uzi lazima nzi wajae.. Lucas katuonyesha wazi kuwa unaweza kuwa mwanaCCM na ukajenga hoja za kukubaliwa na pande zote.
Nonsense
 
img_1_1714763390384.jpg
 
Mwaashambwa huyo no 6 siyo Mtanzania acha kunidanya. Hana hata kitambulisho cha taifa la Tanzania na hatokuja kuwa nacho.
 
Wewe na Lucas Mwashambwa dugu moya! Akili zenu mnazijua wenyewe! MamaSamia2025 umesahau rekodi yako moja ile niliyokutatua marinda ukiwa binti mdogo!
 
Back
Top Bottom