Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Ok mkuu, vipi kuhusu mwamba Kizota?
Kizota na yeye alikuwa mzuri, kucheka na wavu kwake lilikuwa ni jambo la kawaida na pia kumnyang'anya mpira ilikuwa shughuli.
 
Kihistoria ila sio standard. Ukiweka accomplishments za Mohammed Ali na za Tyson utaona Tyson yupo juu ya Mohamed.

Ila nakupa tu 2pac nitafutie ambaye anaweza tengeza kazi za hip-hop za kiume size yake zama hizi.

Au Michael Jackson ntafutie pop artists anaemfikia hadi sasa kwa kazi zake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa mods hawana adabu wanatakiwa kuadhibiwa kwa makofi. Wanatoaje picha ya 2pac na Michael Jackson katika uzi wa ishma kama huu?! [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo kwa wacheza sinema wa Marekani kila mmoja alikuwa mkali kulingana na fan yake ya uchezaji.
Mfano Chuck Norris alikuwa mzuri kwa upiganaji, Rambo akishika mashine mkononi kwake basi hata vietnam M1 watakwisha tu kama njugu, mzee Anord huyu ni mzuri sana kwa upande wa movie za teknolojia kama vile Predator, Terminator nk.

Africa America kwa upande wang nawaona wawili wanachuana hapo chini
1) Samuel Jackson
2) Denzel Washinton

Bollywood unawekaje kijana mdogo kama Shahrukh Khan na kumuacha mkongwe Dharmendra ambaye hajawahi kupigwa ndan ya movie zake na pia hata watoto wake kina San Deo na Bob Deo walifuata utemi wa baba yao.
Bongo movie Kanumba umepatia maana kina vicent kigosi ambao wangevaa viatu vyake ndio hao wanaoshinda wanakunywa maji ili wawe weupe.

Mfalme wa soka miaka yote anajulikana, na hajawahi kumuachia mtu kiti chake cha ufalme huyu ni mchawi wa soka duniani ndugu Pele.
 
Ya ni kweli mkuu, hata mimi namkubali sana tena sana Tyson, ulimwengu wa masumbwi kamwe hauwezi kuja kumsahau abadani.
Ila ndio hivyo kwa vile Ali alitangulia kujijengea heshima yeye na mchezo mzima wa masumbwi basi acha heshima iendelee kubaki kwake tu japo hilo haliwezi kumuathiri wala kumpunguzia pia heshima na sifa Mike Tyson.
 
Ebuuu Mleta uzi chokoza mada watu watuletee List ya Wanasayansi bora dunian, Maana nishashindwa kumlinganisha Newton na Washkaj zake wa enzi hizo.
 
Weka hizo accomplishments tuone.
 
naongezea hii,aliwahi kutupa medali yake ya dhahabu mtoni aliyoipata kwenye mashindano ya Olympics baada ya kubaguliwa na muuza bidhaa kisa yeye NI black hivyo hakupaswa kuhudumiwa licha ya Ali kumuuliza muuzaji Kama alikuwa anamjua na alijibu kuwa anamtambua ila sio sababu Bado ya yeye kuhudumiwa..Alikasirika kwa sababu alipigana kwa ajili ya taifa na kila raia wa nchi yake lakini anabaguliwa kisa RANGI yake
 
Shukran na ubarikiwe sana mkuu. Tatizo baadhi ya watu hawakujishughulisha, na wala hawajishughulishi kumjua Ali vizuri. Huyu mwamba alikuwa ni bingwa wa aina yake kutokea katika ulimwengu wa Masumbwi.
Ali alikuwa na uwezo wa kumchezesha adui yake round hata mbili bila kupigwa ngumi hata 1.
 
Ebuuu Mleta uzi chokoza mada watu watuletee List ya Wanasayansi bora dunian, Maana nishashindwa kumlinganisha Newton na Washkaj zake wa enzi hizo.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mkuu hapa tu tayari kuna watu wameshapita wakaona ulichoandika.
Ngoja mwenye uelewa zaidi na ulichouliza atajitokeza atupe ufafanuzi wa unachotaka kujua.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu hapa tu tayari kuna watu wameshapita wakaona ulichoandika.
Ngoja mwenye uelewa zaidi na ulichouliza atajitokeza atupe ufafanuzi wa unachotaka kujua.
Yah nahtaj sana kujua hiyo kitu Mkuu, Maana wengine husema Henstain is the best.
 
Bila kanumba list irudiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…