Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kihistoria ila sio standard. Ukiweka accomplishments za Mohammed Ali na za Tyson utaona Tyson yupo juu ya Mohamed.Mkuu haya mambo nimeshayatolea ufafanuzi kwa baadhi ya post huko juu.
Iwe mpira, masumbwi, mziki nk tayari kuna wale ambao washapewa heshima ya ufalme na wahusika wa hiyo michezo. Haijalishi hawa vijana wa sasa au baadae wanaweza kufikia au kuzidisha rekord za hawa ma legends au not. Soma post namb 34 na 36 mkuu naambatanisha na picha hapo chini.
Kama chama cha ndondi duniani kimeamua kuwa Mohammad Ali ndio mfalme wa masumbwi wa miaka yote, mimi na ww ni kina nani mpaka tupingane na wajuzi hao.
Si waliwaona kina Lewis, Tyson na wengine wengi waliokuwepo kabla na baada ya Mohammad Ali?
Hawa mods hawana adabu wanatakiwa kuadhibiwa kwa makofi. Wanatoaje picha ya 2pac na Michael Jackson katika uzi wa ishma kama huu?! [emoji23]Mkuu nashukur kwa kuongeza baadhi ya legendary kwenye list, ila ukweli ni kwamba Michael Jackson yupo kwenye list ni namb 4 pia niliweka na picha zake nashangaa moods walizitoa bila taarifa na ukisoma comment kuna sehem pia nimewakumbusha warudishe picha za Jackson na 2pac lkn hadi sasa hawajafanya hivyo wamekausha tu. Afu picha zenyewe ni za kawaida wala sio mbaya nitaziweka hapa kwa post hii uzione kama zilifaa kutolewa.
Kuhusu 2Pac na yeye nilimuweka namb 5 au 6 hivi, lkn pia moods wakafuta kama walivyofanya kwa Jackson japo majina na historia kidogo waliviacha, so inakuwa ngumu mtu kuwaona kama wapo kwa list.
Picha hizo hapo waliziondoa mkuu.
Hapo kwa wacheza sinema wa Marekani kila mmoja alikuwa mkali kulingana na fan yake ya uchezaji.Tumchukue nani hapa?
Chuck Noris
Sylvester Stalone( Rambo)
Shwarznegger
Kuna yule mzee aliyecheza Movie ya 10 Commandments
Kwa African Americans tukchukue nani? Au
Sidney Poitier
Denzel Washington?
Kwenye Bollywood tumchukue nani?
Amita Bhachan au
Shahrukh Khan
Kwenye Bongo Movie
kanumba hana mpinzani
Kwenye Soccer
Messi
Maradona
Pele
Ya ni kweli mkuu, hata mimi namkubali sana tena sana Tyson, ulimwengu wa masumbwi kamwe hauwezi kuja kumsahau abadani.Kihistoria ila sio standard. Ukiweka accomplishments za Mohammed Ali na za Tyson utaona Tyson yupo juu ya Mohamed.
Ila nakupa tu 2pac nitafutie ambaye anaweza tengeza kazi za hip-hop za kiume size yake zama hizi.
Au Michael Jackson ntafutie pop artists anaemfikia hadi sasa kwa kazi zake?
Sent using Jamii Forums mobile app
Yan hata mimi nilishangaa mkuu, labda wana beef nao la kimya kimya 😂😂😂😂Hawa mods hawana adabu wanatakiwa kuadhibiwa kwa makofi. Wanatoaje picha ya 2pac na Michael Jackson katika uzi wa ishma kama huu?! [emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkonoJiandae kuja kuongeza jina la Lione MESSI.
Kwani Tyson hakupigwa? Tena kapigwa hadi na bums kama James Buster Douglas na Kenneth MacBride.Ali kapigwa Mara kadhaa eg na Smokin Joe Frazier
Weka hizo accomplishments tuone.Kihistoria ila sio standard. Ukiweka accomplishments za Mohammed Ali na za Tyson utaona Tyson yupo juu ya Mohamed.
Ila nakupa tu 2pac nitafutie ambaye anaweza tengeza kazi za hip-hop za kiume size yake zama hizi.
Au Michael Jackson ntafutie pop artists anaemfikia hadi sasa kwa kazi zake?
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante. Nilikuwa sijaiona hiyo.Pele nimemuweka kwa post ya katikati mkuu.
naongezea hii,aliwahi kutupa medali yake ya dhahabu mtoni aliyoipata kwenye mashindano ya Olympics baada ya kubaguliwa na muuza bidhaa kisa yeye NI black hivyo hakupaswa kuhudumiwa licha ya Ali kumuuliza muuzaji Kama alikuwa anamjua na alijibu kuwa anamtambua ila sio sababu Bado ya yeye kuhudumiwa..Alikasirika kwa sababu alipigana kwa ajili ya taifa na kila raia wa nchi yake lakini anabaguliwa kisa RANGI yakeAli katika mapambano matatu na Joe Frazier kashinda mawili na yeye kapoteza moja.
Tena alipoteza pambano kipindi kile alichokataa kwenda kupigana Vietnam, kwahiyo kitendo kile kilimtengenezea mizengwe serikalini. Baadhi ya mizengwe hiyo ni (a) kufunguliwa kesi kumbuka kitendo cha kukataa kwenda vitani kupigania taifa lake miaka ile ilikuwa ni kosa kisheria, (b) kupigwa marufuku ya kupigana nchini kwao Marekani, (c) kuanza kuwekwa ktk list ya wanaharakati ambao walionekana ni maadui wa ndani wa Marekani kipindi hicho.
I mean kulikuwa na mambo mengi ambayo yalimchanganya na kumfanya ashindwe baadhi ya mapambano. Fikiria mtu ukiwa ktk situation aliyokuwa nayo yeye dhidi ya serikali yake na nchi yake mwenyewe.
Hata ingekuwa ww ungejiweka ktk hali gani mkuu. Hapo chini baadhi ya picha ya mapambano tofauti Mohammad Ali akimuadhibu Joe Frazier kama mtoto wake.
Unaweza kumchukulia Ali poa kama haujipi muda wa kumjua vizuri huyu mwamba, na sababu za kushindwa kwake zilitokana na nini.
Shukran na ubarikiwe sana mkuu. Tatizo baadhi ya watu hawakujishughulisha, na wala hawajishughulishi kumjua Ali vizuri. Huyu mwamba alikuwa ni bingwa wa aina yake kutokea katika ulimwengu wa Masumbwi.naongezea hii,aliwahi kutupa medali yake ya dhahabu mtoni aliyoipata kwenye mashindano ya Olympics baada ya kubaguliwa na muuza bidhaa kisa yeye NI black hivyo hakupaswa kuhudumiwa licha ya Ali kumuuliza muuzaji Kama alikuwa anamjua na alijibu kuwa anamtambua ila sio sababu Bado ya yeye kuhudumiwa..Alikasirika kwa sababu alipigana kwa ajili ya taifa na kila raia wa nchi yake lakini anabaguliwa kisa RANGI yake
😂😂😂 mkuu hapa tu tayari kuna watu wameshapita wakaona ulichoandika.Ebuuu Mleta uzi chokoza mada watu watuletee List ya Wanasayansi bora dunian, Maana nishashindwa kumlinganisha Newton na Washkaj zake wa enzi hizo.
Yah nahtaj sana kujua hiyo kitu Mkuu, Maana wengine husema Henstain is the best.[emoji23][emoji23][emoji23] mkuu hapa tu tayari kuna watu wameshapita wakaona ulichoandika.
Ngoja mwenye uelewa zaidi na ulichouliza atajitokeza atupe ufafanuzi wa unachotaka kujua.
Bila kanumba list irudiweZa asubuhi wakuu, leo nakuja na makala ya watu maarufu duniani, ambao wameacha alama kubwa katika tasnia zao na mpaka leo hakuna alietokea kuziba mapengo yao.
1) Mohammedi Ali
Huyu ni bingwa, mbabe na mtemi wa masumbwi ulimwenguni kote. Mohammed Ali ambae alizaliwa 17 January 1942, huko Louisville, Kentucky Marekani na kufariki 3 June 2016, huko Scottsdale, Arizona Marekani. Alikuwa ni bondia wa pekee kuufanya mchezo huo uwe na wapenzi na waangaliaji wengi ulimwenguni.
Licha ya kwamba mchezo huo ulikuwepo maelfu ya miaka kabla ya ujio wake Ali, lkn ni yeye ndio aliefanya watu waanze kuupenda zaidi mchezo huo na kuchukua nafasi ya pili kwa kupendwa duniani baada ya mchezo wa mpira wa miguu. Ali ambae alikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki ulingo, kukwepa ngumi, na mwepesi wa kupiga ngumi za haraka haraka. Lakini pia alikuwa na mbinu nyingi za kuweza kumchosha na kummaliza kbs mpinzani wake wakati wowote alioutaka yeye ulingoni.
Ali alikuwa na uwezo wa kumsogezea mpinzani sura, lkn utashangaa hadi round nzima inaisha bila mpinzan wake kufanikiwa kumpiga ngumi hata 1 tu usoni (kama tuonavyo pichani) sometimes unakuta mpinzani wake anarusha ngumi (kota) na kuanguka mwenyewe, huku Ali akimtizama kwa dharau 😂😂🤣🤣
Pamoja na yote lkn kama ilivyo michezo mingine na yey kuna muda alikuwa anapoteza baadhi ya mapambano pia, aidha kwa kutokana na mchoko wa mazoezi makali anayokuwa amefanya kabla ya pambano nk. Toka Ali alipostaafu ngumi mpaka kifo chake, hakuna bondia ambae ashawahi kufikia rekodi ya upiganaji wake na vituko vyake awapo ulingoni na nje ya ulingo.
Mabondia wengi kama kina Mike Tyson, Evander, Lenox Lewis na wengineo walikuwa wanakwenda kumuona na kupata mbinu mbali mbali za kupigana ulingoni kupitia mfalme huyo wa ngumi ulimwenguni. Huyu ndio Mohammed Ali alieacha alama kubwa ktk mchezo huo maarufu wa ngumi duniani. Hakuna na hatotokea Mohammed Ali mungine, Never.
Mungu ailaze roho ya huyu Legend mahali pema peponi.
View attachment 2335340
2) Bob Marley
Bob Marley alizaliwa 6 Feb 1945, huko Nine Mile, Jamaica, na kufariki 11 May 1981, huko Florida Marekani.
Alipozaliwa aliukuta mzikiwa reggae ukiwa ulimwenguni miaka na miaka. Lkn kwa kipaji chake na uwezo wake akaanza kuleta mabadiliko makubwa katika mziki huo, hadi kufikia hatua ya kusikilizwa na viongozi wakubwa wa nchi mbali mbali. Japo kulikuwa na waimbaji wengine wakubwa kama kina Peter Tosh, Burn Spear nk, lkn ni yeye Bob Marley ndio aliefanya reggae ipendwe na walio wengi. Hadi anakufa Bob Marley aliacha muziki huo ukiwa na mamilioni ya wasikilizaji ulimwenguni.
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
View attachment 2335341
3) Bruce Lee
Bruce Lee alizaliwa 27 Nov 1940, huko San Francisco, California Marekani na kufariki 20 July 1973 huko Kow loon Tong, Hong Kong.
Bruce alizaliwa na kuukuta mchezo wa kung fu au karate ulimwenguni. Lakini kwa kipaji alichozaliwa nacho, alianza kuleta mabadiliko makubwa kwenye mchezo huo hadi kushawishi mamilioni ya watu ulimwenguni kuupenda na kuanza kuufuatilia mchezo huu. Bruce alikuwa na uwezo mkubwa wa kucheza na hisia za adui na kujua ni wapi atapopiga lazima adui atakaa tu hata awe na mwili kama jumba.
Ikafika kipindi watu wakamshauri ajiunge kwenye tasnia ya uigizaji ili kuwavutia watu zaidi kuupenda mchezo huo, lkn pia kujifunza baadhi ya mbinu za upambanaji kupitia movie zake. Mpaka toka Bruce afariki mpaka leo bado anapewa heshima kubwa na magwiji wa mchezo huo wakiwemo wacheza sinema kama vile Jackie Chan, Jet Lee nk. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
View attachment 2335338
Wanaofuatia ni 👇
4) Michael Jackson king wa Pop na mitelezo.
5) 2pac Shakur king wa Hip hop aliekuwa haiogopi serikali ktk kuwatetea wamarekani weusi wenzake na jamii nyingine zilizobaguliwa nchini Marekani, pia alipambana sana na polisi kuhusu unyanyasaji wowote uliofanywa na jeshi hilo kwa vijana mbali mbali hadi alipouwawa. Aliwahi kuwa na kesi ya kuwashambulia polisi wawili na bunduki, baada ya 2pac kupita sehem na gari aliwakuta polisi wakiwa wamemfunga pingu mtu mweusi huku wanampiga, kitendo kile kilimuuzi 2pac ndipo alipoamua kutoa bastola yake na kuwashambulia polisi, japo baadae polisi wale waliwahishwa hospital na kupona.
Katika kesi ile 2pac hakuhukumiwa baada ya kuonekana kuwa wale polisi walikuwa na makosa ya kiutendaji kwa mtuhumiwa waliekuwa wamemkamata.
Mungu awalaze roho zao mahali pema peponi.
6) Michael Jordan
Mzee wa kudumbukiza kikapuni. Huyu alikuwa na uwezo wa kuruka juu zaidi na kuonekana kama ameganda kwa sekunde kadhaa hewani kabla ya kutia mpira kapuni na kushuka chini. Toka astaafu bado hajapatikana Jordan mungine, japo bwana mdogo hayati Kobe Bryant alijitahidi kwa namna fulan, lkn bado hakufikia kule alipofikia mzee wa kazi.
View attachment 2335342
Hawa ni baadhi ya watu ambae mpaka leo viatu vyao viko wazi, havijapata wa kuvivaa vikawatosha.