Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Hata mimi nilikuelewa sana, lakini hawa bado huwezi kuweka boxi moja na Bob, yule Rasta amekua kama nabii na si tu umaarufu kama hawa wengine, yule anachukuliwa kama prophet, alikua na maneno mazito kama ya manabii wa MUNGU wa kale na si tu kuimba kiasi umlinganishe na mcheza ngumi, mcheza mpira na mwanamuziki anayeimba mambo ya kawaida ya Dunia, Bob ni level tofauti na ndiyo maana unaona uliowataja wengine wanapotea, lakini Marley anaishi toka ameondoka
Ya ni kweli mkuu, heshima ya Bob Marley hapa Afrika, Asia na duniani kwa ujumla ni kubwa mara kumi zaidi ya hayati George Washington (baba wa taifa la Marekani)
I feel ya bra.
 
We jamaa bhana umenikumbusha mbali hao wa mnanda walikuwa wanaitwa Hisani gari kubwa ndio waliimba hizo nyimbo...kumbe zao manzese ccm na mburahati huko....miaka ya 90...we kweli mwamba.
Mkuu Dadii Toka mwanzoni mwa miaka ya 90 mimi nilikuwa mfuatiliaji mkubwa wa miziki, michezo na mambo mbali mbali yaliokuwa yanafanyika nchini na duniani kwa ujumla. Japo nilikuwa na umri mdogo, lkn nilikuwa na akili au uwezo wa kutambua kila kinachoendelea ktk nchi yetu na dunia yetu kwa ujumla. So naielewa historia ya hawa hisani vizuri.
Hisani au gari kubwa hili ni kundi la mnanda lililoundwa na vijana kutoka maeneo ya mw/nyamala koma koma kama sijasahau. Afu kwa upande wa Mburahati, Manzese, Mabibo na Kigogo wao walikuwa na makundi yao mengine ambayo majina nimeyasahau.
Hawa Hisani waliweza kujijengea umaarufu kutokana na umahiri wa tungo zao zenye akili, zilizojaa ujumbe unaoeleweka kama vile Ally Mwinyi, Mola, Uko wapi mama na nyinginezo nyingi.
Wimbo huu wa Ally Mwinyi ndio uliosababisha mzee Rukhsa atoe marufuku iliyokuwa imewekwa na serikali (chini ya wizara ya mambo ya ndani) Kabla ya hapo mziki huu ulionekana kama vile ni mziki wa kihuni uliokuwa unavunja maadili ya mtanzania. Hata wazee wengi walikuwa wanapingana na mziki huu, polisi nao haikuwa nyuma ktk kamata kamata ya waimbaji wa mziki ule.
Ila Mwinyi alipotoa ruhusa ndo hapo ulipoanza kusambaa na wengi wakaja gundua kuwa mziki huo pia ulikuwa na ujumbe unaofunza na kuelimisha kama zilivyo nyimbo nyingine za miziki ya dansi nk.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] hakuna king wawili kwenye tasnia. Hapo kwenye mpira tayari kaishabana mzee Pele wa brazil toka miaka hiyo. Hata waliotaka na Maradonna aongezwe walichemsha, sembuse ije kuwa bwana mdogo Mesi??
Hapo umesahau jon bocco tupende vya kwetu ,,[emoji2][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hapo umesahau jon bocco tupende vya kwetu ,,[emoji2][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ya kweli mkuu, mkataa kwao mtumwa.
Ngoja nijipange kuja na list ya nyumbani.
 
madaraka selemani hata kwa kibadeni haingii...mpaka mtu kaitwa King Mputa sio jambo dogo...hata kwa Zamaoyoni Mogella Golden Boy haingii. Alafu Madaraka National Team hajafanya kazi ilee na Simba kama alikuja malizia mpira tu...Madaraka alikuwa wa moto Majimaji ya songea kisha akaenda zake uarabuni ndio kaja Simba.
Ok mkuu, vipi kuhusu mwamba Kizota?
 
Tumchukue nani hapa?
Chuck Noris
Sylvester Stalone( Rambo)
Shwarznegger

Kuna yule mzee aliyecheza Movie ya 10 Commandments

Kwa African Americans tukchukue nani?
Sidney Poitier
Denzel Washington?

Kwenye Bollywood tumchukue nani?
Amita Bhachan au
Shahrukh Khan

Kwenye Bongo Movie
kanumba hana mpinzani

Kwenye Soccer
Messi
Maradona
Pele
 
Ndugu, Bob Marley ni level tofauti sana na hawa,ukivuta kumbukizi na kufatilia hata kama ni binadamu kama hawa lakini yeye alikua na kitu special zaidi, elewa ya kwamba Peter Tosh alikua mwamba wake sana ktk tunzi za muziki lakini Marley alitunukiwa kivingine kuleta ushawishi duniani

Ukimuondoa Yesu na Mohammed ni huyu Bob Marley anayefuata kwa kua na watu wengi zaidi duniani kama wafuasi na wwaliofatilia maisha yake, toka amefariki 1981,kuanzia hapo mpaka leo kaburi lake na makao yake ni eneo linalotembelewa na tu karibu kila siku ama kila wiki toka kipindi hicho mpaka leo hii

Hii inamfanya kua tofauti na hawa kina Alli, maana kidogo kidogo wanaanza kupotea lakini si Bob,fatilia utajua
Aisee upo sahihi sana
 
Ali kapigwa Mara kadhaa eg na Smokin Joe Frazier
Ali katika mapambano matatu na Joe Frazier kashinda mawili na yeye kapoteza moja.
Tena alipoteza pambano kipindi kile alichokataa kwenda kupigana Vietnam, kwahiyo kitendo kile kilimtengenezea mizengwe serikalini. Baadhi ya mizengwe hiyo ni (a) kufunguliwa kesi kumbuka kitendo cha kukataa kwenda vitani kupigania taifa lake miaka ile ilikuwa ni kosa kisheria, (b) kupigwa marufuku ya kupigana nchini kwao Marekani, (c) kuanza kuwekwa ktk list ya wanaharakati ambao walionekana ni maadui wa ndani wa Marekani kipindi hicho.
I mean kulikuwa na mambo mengi ambayo yalimchanganya na kumfanya ashindwe baadhi ya mapambano. Fikiria mtu ukiwa ktk situation aliyokuwa nayo yeye dhidi ya serikali yake na nchi yake mwenyewe.
Hata ingekuwa ww ungejiweka ktk hali gani mkuu. Hapo chini baadhi ya picha ya mapambano tofauti Mohammad Ali akimuadhibu Joe Frazier kama mtoto wake.

Unaweza kumchukulia Ali poa kama haujipi muda wa kumjua vizuri huyu mwamba, na sababu za kushindwa kwake zilitokana na nini.
 

Attachments

  • Screenshot_20220827-145232.jpg
    Screenshot_20220827-145232.jpg
    41.8 KB · Views: 12
  • images (35).jpeg
    images (35).jpeg
    19.2 KB · Views: 13
  • images (36).jpeg
    images (36).jpeg
    19.8 KB · Views: 11
  • images (34).jpeg
    images (34).jpeg
    26.8 KB · Views: 12
Back
Top Bottom