Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Hawa ni watu maarufu duniani ambao viatu vyao vimekosa mvaaji

Mkuu unaota ndoto za mchana. Tafuta rekodi zao, angalia kila mmoja alipigana na nani ndio uwafananishe.
Shukran mkuu kwa kunisaidia kujibu.
Jamaa nilikuwa nishamjibu maana inaonekana yey anayachukulia haya mambo jujuu.
 
Alejandro Pele wa Brazil naye Ni level nyingine kbsa.Naamini mpaka Dunia inaisha Hakuna mchezaji wa Sola atakaye kuja kufikia viwango vya Pele.

Duru zinasema katika kipindi chake Cha uchezaji jamaa alifunga mabao zaidi ya 1,500
Mkuu nashukur sana kwa kunisaidia baadhi ya data za huyu mchawi wa soka. Kuna mwamba fulan eti anamlinganisha Messi na Pele.
Kwamba eti Messi ndo anastahili kuwa king wa mpira wa miguu. Mwamba amesahau kwamb kabla ya Messi kulikuwa na wachezaji hodari na wenye uwezo zaidi ya alionao Messi.
Wachezaji kama Ronaldo de Lima, Bebeto, Rivaldo, Ronaldinho, Zinedine Zidane na mkongwe Maradonna. Hao niliowataja walikuwa hatari kuliko Messi lkn walikubali tu kwamba Pele ni level nyingine isiyotakiwa kujadiliwa.
 
Uzi wako umekosa maana kwa kukosa jina la mfalme wa Pop, Michael Jackson hapo ndipo ulichemka. Tena alitakiwa kuwa namba moja hapo. Hawa umewataja kuna watu wameweka rekodi za kuwafunika.

Mfano, Mohamed ali ukimuweka na Tyson, hivi nani katika ujana wake ameweka rekodi kali?!

Bruce lee ni mkali wa karate moves miaka hiyo ila ukitazama kuna mtu kama Don Yen,Jet Lee, ana moves kali balaa brucelee anasubiri.

Bob Marley raggae yake siwezi kusemea maana ni ya tofauti na reggae za sasa sababu yake ilikuwa politically motivated. Wenzake ni kama akina 2pac kwenye hip-hop hakuna wa kumlinganisha nae tokana na mistari yake na style ya delivery. So kwa bob Marley nitakupa pass.

Michael Jordan pia ukitazama League ya NBA kuna madogo wanapiga kikapu hadi unaogopa yeye mwenyewe Jordan ana appreciate uwezo wao na kukiri angekuwapo kwenye court miaka hii angetolewa jasho.

Ila nionyeshe msanii anayeweza match legacy ya Michael Jackson hadi leo hii tokea jamaa amefariki au hata alipokuwa hai! Huyo mtu hayupo.

Ntafutie mtu anayeweza kufunika legacy ya 2pac kwenye hip-hop?

Nitafutie mtu wa kufunika legacy ya Anold Schwarzenegger kwenye cyborg figure?

Nani anamfunika Kenny G katika uimbaji kwa kutumia tarumbeta?!




Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nashukur kwa kuongeza baadhi ya legendary kwenye list, ila ukweli ni kwamba Michael Jackson yupo kwenye list ni namb 4 pia niliweka na picha zake nashangaa moods walizitoa bila taarifa na ukisoma comment kuna sehem pia nimewakumbusha warudishe picha za Jackson na 2pac lkn hadi sasa hawajafanya hivyo wamekausha tu. Afu picha zenyewe ni za kawaida wala sio mbaya nitaziweka hapa kwa post hii uzione kama zilifaa kutolewa.

Kuhusu 2Pac na yeye nilimuweka namb 5 au 6 hivi, lkn pia moods wakafuta kama walivyofanya kwa Jackson japo majina na historia kidogo waliviacha, so inakuwa ngumu mtu kuwaona kama wapo kwa list.
Picha hizo hapo waliziondoa mkuu.
 

Attachments

  • Screenshot_20220821-143452.jpg
    Screenshot_20220821-143452.jpg
    57.7 KB · Views: 19
  • Screenshot_20220821-143311.jpg
    Screenshot_20220821-143311.jpg
    39.4 KB · Views: 19
  • images (13).jpeg
    images (13).jpeg
    21.8 KB · Views: 15
Lionel Messi ni mtoto sana kwa Pelle
Hakika na ww umeliona hilo mkuu.
Inaonekana mwamba ameanza kuangalia mpira miaka hii.
Kwangu mimi Messi hawezi kufikia hata viwango vya kina Zidane wa 1998 to 2006, Ronaldo de Lima wa 1994 hadi 2005, Ronaldinho, Bebeto na wengine wengi tu wa enzi hizo waliokuwa wanalichapa kabumbu sawa sawa.
 
Tumkumbuke Mzee Small na Mzee Majuto. Msiwasahau kwa Tanzania These guys were best comedians
 
Mwamba Issack Newton na Robert Einstein hawashikiki hao kwenye Science na Teknolojia. Viatu vyao havijapata mpinzani
 
Hakika umeandika maneno mazuri sana mkuu. Muziki wetu ulianza kumezwa baada ya ujio wa kina Mr 11 (sugu) mnamo mwanzoni mwa miaka ya 90.
Jamaa alikuwa anasikiliza nyimbo za kina 2Pac afu anazibadilisha kwa kiswahili, vijana wanafurahi wanaona ujanja. Ikaenda ikaenda mwisho vijana wengi wakaingia kwenye mkumbo huo wa muziki wa wenzetu, na kuuendeleza hadi leo. Wanachofanya ni kubadili majina tu ili uonekane ni mziki wa nyumban.
Mara hip hop bongo, mara bongo fleva nk.
Wengine waliotuingiza chaka japo sio ile kivile ni hawa sijui twanga pepeta ya kina marehemu banza, ali choki, muumin mwinjuma nk.
Nao hiyo singeli ndo afadhali kidogo imesimama ktk nafasi ya mnanda au mchiriku kama wengi tulivyokuwa tunaita miaka hiyo. Mziki huu ulionekana wa kihuni, japo baadae baada ya wale vijana wa garikubwa kule mw/nyamala kuja na vibao vya akili kama vile raisi wetu hodari Ali Mwinyi, uko wapi mama nk.
Dah mziki wetu ushaondoka na ma legend wetu.
Kwani hao kina Mbaraka mwishehe si walicopy nyimbo za Kongo
 
Yani mimi mkuu toka huyu mzee alipoondoka ktk nafasi yake kama manager na kocha wetu basi mpira wenyew nimepunguza speed ya kuupenda maana nimeona unaweza kuniletea ugonjwa wa moyo bure.
Hakuna atakaekuja kuziba pengo la yule mzee kwa sasa, hakuna kabisa.
Itabaki kuwa pengo, haitatokea wa kuvaa viatu vyake
 
Ya hakika hawa ma legendary wawili Mike Tyson na Lucky Dube walijitahidi kuwa na miguu iliyokaribia kuenea viatu vya wafalme wao, pia hata kwa upande wa Bruce Lee wanasema legendary mungine ni Jackie Chan nae ni moto wa kuotea mbali, ila ndo hivyo walikuwa na vidole vifupi kwahiyo viatu havikuwatosha vizuri.
Mkuu japo me kwa upande wangu naona Mike Tyson na Lucky Dube viatu wamevivaa vizuri kabisa na vimewatosha mnoo. Ila kwa Jackie Chan viatu vya Bluce Lee vimempwaya.
 
ningependa kujua rekodi ambazo Mohammed Ali aliziacha na hazijafikiwa ama kuvunjwa mpaka leo!?
Ali Hana rekodi za kutisha kuliko wengine woote. Lakini ulingoni alikua na mbinu za kipekee alipowapiga wapinzani wake .
Tofauti na Hilo Ali ( Calsius Clay) alikuwa socialite was kipindi hicho
Pia mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa Rangi.
Mwanaharakati dhidi ya Vita hasa Vietnam. Ali alikataa kwenda Vietnam akachagua kwenda jela.. anasema Kwamba haikua vyema kuwapiga watu walio maelfu ya km kutoka nyumbani (Marekani) bila sababu ya msingi.
Hili likapelekea Ali kuanza kukubali a Duniani kote kwa kitendo hiki.
Mbinu za upiganaji.
Ali alikua mpiganaji mwenye mbinu za kuchekesha kuburudisha Sana.
Ali alikua mzungumzaji mwenye ushawishi na hasa vituko anapojigamba dhidi ya mpinzani wake.
Duh Ali ana mengi Sana.
 
Tumkumbuke Mzee Small na Mzee Majuto. Msiwasahau kwa Tanzania These guys were best comedians
Dah shukran mkuu, aisee nimehisi kutaka kutokwa na machozi baada ya kuyaona haya majina.
Hakika udongo unakula binadam badala ya kula kisamvu au viazi.
Hawa ni ma legend wakubwa sana kwa nchi yetu, ukanda wetu, bara letu na dunia yetu kwa ujumla.
 
Kushinda pambano dakika ya 1, 2 au ya 3 ndio kunakufanya kuwa bondia bora? Mkuu unajua boxing au unaisikia tu?
Umeuliza swali zuri sana mkuu. Atakaewahi kuona jibu lake amtag mwenzake.
 
Mwamba Issack Newton na Robert Einstein hawashikiki hao kwenye Science na Teknolojia. Viatu vyao havijapata mpinzani
Kweli mkuu hawa legendary nilifanya kosa kutokuwaweka.
 
Kwani hao kina Mbaraka mwishehe si walicopy nyimbo za Kongo
Hawa ku copy nyimbo za Kongo, isipokuwa hiyo ndio ilikuwa asili ya nyimbo za kiafrika. Ukibahatika kusikia nyimbo za Zimbabwe, Malawi, Kenya na kwengine mwendo na style ya mziki wao wa zaman ilikuwa ni hii hii ya Tanzania, Congo, Burundi nk.
 
Back
Top Bottom