Hawa ni watu waliomdhihaki Mungu na kupatwa na shida

Joined
Oct 26, 2021
Posts
99
Reaction score
294
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966. Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)
Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)
Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute" Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC
Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi kuizamisha" Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)
Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya "Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'. Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6.
Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake.
Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti la gari". Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)
Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia" Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)
Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simuhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu
hakuna kama Mungu.

Follow me on twiiter as LegalGentleman
 
Namba 6 hapo ilikuaje kuaje yaani?

2F65C5CC-3671-436B-82FA-C3E5372E1399.jpeg
 
Nakupa list ya wachungaji na masheikh ambao hawakumdhihaki Mungu na walipata shida na kufariki

1. TB JOSHUA
2. MAMA LWAKATALE
3. STEPHEN AKNOLA
4. ISSA TURAY
5. WILSON BADEJO

Sheikh nooren mohammed hakumdhihaki Mungu lakini alikufa kwa ajali mbaya sana.

Sheikh Saeed bin nahynan huyu kafa siku nne zilizopita naye kwa ajali mbaya sana na hakumdhihaki Allah

Rashid bin Mohammed naye alikufa kwa shambulio la moyo na hakuwahi mdhihaki Mungu.

Na sio tu hao wapo wengi sana wamekufa na wengine wakipata shida pasipo hata kumdhihaki Mungu.

Kinachokufanya uone hao watu uliowataja kua wamepatwa na shida kutokana na wao kumdhihaki Mungu ni kipi? Nani asiyepata tabu hapa ulimwenguni?

Huyo Mungu wako historia ya dini inaonesha yeye ndio alikua muanzilishi wa kupata tabu baada ya vita yake na shetani ambapo shetani alizua utata huko juu mpaka akafanikisha kusepa na robo tatu ya malaika unafikiri tabu aliyoipata huyo Mungu ilikua ndogo?

Kwa hiyo nayeye tuseme alimdhihaki nani mpaka ikamfika hiyo tabu?
 
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi

Una uhakika gani kwamba Mungu ndiye aliyewaua, na sio hao wanaotetea walivyo vikosoa hao watu?

Mpaka leo bado hujajua kuna watu wana masilahi ya moja kwa moja na dini!
 
Nakupa list ya wachungaji na masheikh ambao hawakumdhihaki Mungu na walipata shida na kufariki

1. TB JOSHUA
2. MAMA LWAKATALE
3. STEPHEN AKNOLA
4. ISSA TURAY
5. WILSON BADEJO

Sheikh nooren mohammed hakumdhihaki Mungu lakini alikufa kwa ajali mbaya sana.

Sheikh Saeed bin nahynan huyu kafa siku nne zilizopita naye kwa ajali mbaya sana na hakumdhihaki Allah

Rashid bin Mohammed naye alikufa kwa shambulio la moyo na hakuwahi mdhihaki Mungu.

Na sio tu hao wapo wengi sana wamekufa na wengine wakipata shida pasipo hata kumdhihaki Mungu.

Kinachokufanya uone hao watu uliowataja kua wamepatwa na shida kutokana na wao kumdhihaki Mungu ni kipi? Nani asiyepata tabu hapa ulimwenguni?

Huyo Mungu wako historia ya dini inaonesha yeye ndio alikua muanzilishi wa kupata tabu baada ya vita yake na shetani ambapo shetani alizua utata huko juu mpaka akafanikisha kusepa na robo tatu ya malaika unafikiri tabu aliyoipata huyo Mungu ilikua ndogo?

Kwa hiyo nayeye tuseme alimdhihaki nani mpaka ikamfika hiyo tabu?
Duhhh! Taratibu basi jamaa!...
 
Sijui kama umesoma na kuelewa kilichodhamiriwa kuwa funzo!Au kuna maudhui ya habari haukupenda yawemo?Hata hivyo,yote kheri tupu!
 
Hakuna funzo lolote kwenye hiyo habari zaidi ya kufanya association ya vitu visivyoendana. Kwahiyo mleta mada anataka kutuaminisha kwamba Mwenyezi Mungu ndio aliwaua hao watu? Mbona kama ni kufa vifo vibaya wamekufa watu wengi maarufu na hatukuwahi kusikia eti waliwahi kumdhihaki Mungu? Kina Lucky Dube, Bob Marley, Paul Walker, Aaliyah, Tupac, Biggie, Sharo milionea, Rais Kennedy, Steve Jobs, Nyerere, nk. Wote hao walikufa kwa ajali, kansa, kupigwa risasi nk sawa tu na hao aliotaja mleta mada..
 
Binafsi nakubali Mungu yupo na anatenda.

Ila naona vifo vya hao waliotajwa inawezekana ni Coincidences tu watu wakaunganisha matukio ya mwisho walisems vipi au ni vifo kutokana na wale wanaoilinda dini ili izidi kuwa imara na kubrainwash binadamu juu ya ubora wa dini.

Umechangia vyema sana, na ambao hawakumdhihaki Mungu ndio asilimia kubwa sana na wanakufa vifo vibaya mno.
 
Sijui kama umesoma na kuelewa kilichodhamiriwa kuwa funzo!Au kuna maudhui ya habari haukupenda yawemo?Hata hivyo,yote kheri tupu!
Ukiweka list ya watu waliomdhihaki Mungu wakapata shida, wakati kuna watu hawajamdhihaki Mungu na wamepata shida hizo hizo, na hata zaidi, list yako ni pointless.

Ni list ya ujuha mtupu.
 
Hakuna funzo lolote kwenye hiyo habari zaidi ya kufanya association ya vitu visivyoendana. Kwahiyo mleta mada anataka kutuaminisha kwamba Mwenyezi Mungu ndio aliwaua hao watu? Mbona kama ni kufa vifo vibaya wamekufa watu wengi maarufu na hatukuwahi kusikia eti waliwahi kumdhihaki Mungu? Kina Lucky Dube, Bob Marley, Paul Walker, Aaliyah, Tupac, Biggie, Sharo milionea, Rais Kennedy, Steve Jobs, Nyerere, nk. Wote hao walikufa kwa ajali, kansa, kupigwa risasi nk sawa tu na hao aliotaja mleta mada..
Bado uko mumo kwa pale.Haukusikia kwa hao wengine kwa sababu hawakukufuru.Haingewezekana kiwepo kitu ambacho hakikuwepo.
 
Kama Mungu angekuwepo, asingekufa mtu yeyote, popote, wakati wowote, kwa sababu yoyote.
 
Ukiweka list ya watu waliomdhihaki Mungu wakapata shida, wakati kuna watu hawajamdhihaki Mungu na wamepata shida hizo hizo, na hata zaidi, list yako ni pointless.

Ni list ya ujuha mtupu.
Sasa,weye hata Mungu tu hutaki,hupendi na umeng'ang'ana kwamba hajawahi kuwepo.Ukiandikiwa hayo utaacha kuona ni u-hopulesi?
 
Bado uko mumo kwa pale.Haukusikia kwa hao wengine kwa sababu hawakukufuru.Haingewezekana kiwepo kitu ambacho hakikuwepo.
Sasa kama hawakukufuru na walipata matatizo hayohayo iweje uwa isolate wachache useme hawa walipata kwasababu walimkufuru Mungu?
 
Sasa,weye hata Mungu tu hutaki,hupendi na umeng'ang'ana kwamba hajawahi kuwepo.Ukiandikiwa hayo utaacha kuona ni u-hopulesi?
Tafadhali acha kuzungumzia watu, zungumzia hoja.

Nimekwambia hivi, ukiniambia hawa wamepata shida kwa sababu wamemdhihaki Mungu, wakatu kuna wengine hawajamdhihaki Mungu na wamepata shida hizohizo na zaidi, list yako ni ujuha mtupu.

Unabisha?

Kama unabisha bishia mantiki ya nilichokiandika. Kwa hoja.

Usinishambulie mimi kwa ad hominem attack.

Kunishambulia mimi ni ishara ya kukosa hoja.
 
Hakuna aliyekushambulia.Nimekueleza kile ulichoning'iniza kichwani mwako.Na si kosa.Umeletewa hoja(kumbuka sijaanzisha uzi mimi) ambapo una haki ya kukataa au kukubali.Maana unapoelekea utauliza huyo Mungu wakati anawaua hao watu nani alithibitisha!
 
Hoja ukiiona utaijua?

Maana nimekuletea hoja, hujaijadili hoja, unanijadili mimi.

Una uwezo wa kujadili hoja wewe?
 
Back
Top Bottom