Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ungemalizia tu;1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966. Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.
2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)
Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.
3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)
Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema "Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute" Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.
4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC
Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu hawezi kuizamisha" Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.
5. BON SCOTT (MUIMBAJI)
Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya "Don't stop me; I'm going down all the way, down the highway to hell'. Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.
6.
Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake.
Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti la gari". Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.
7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)
Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia" Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.
8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)
Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema "Simuhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu
hakuna kama Mungu.
Follow me on twiiter as LegalGentleman
Kwani weye unaamini Mungu yupo?Wasiomdhihaki Mungu hawafi?
Hawapati shida?
Mungu hayupo, ndiyo maana hii habari ni ujinga mtupu.K
Kwani weye unaamini Mungu yupo?
Mama Lwakatre siyo, full stop. TB Joshua alisema nitakufa kabla ya birthday, baada ya muumini wake mmoja kumtakia HBD wiki mbili kabla na siku hiyo ndiyo aliyotabiri vita Urusi na kutengwa kwa Putin. Fuatilia vitu vizuri na ujue undani wa mtu kabla ya ku-judge kuwa yuko hivi au vile.Nakupa list ya wachungaji na masheikh ambao hawakumdhihaki Mungu na walipata shida na kufariki
1. TB JOSHUA
2. MAMA LWAKATALE
3. STEPHEN AKNOLA
4. ISSA TURAY
5. WILSON BADEJO
Sheikh nooren mohammed hakumdhihaki Mungu lakini alikufa kwa ajali mbaya sana.
Sheikh Saeed bin nahynan huyu kafa siku nne zilizopita naye kwa ajali mbaya sana na hakumdhihaki Allah
Rashid bin Mohammed naye alikufa kwa shambulio la moyo na hakuwahi mdhihaki Mungu.
Na sio tu hao wapo wengi sana wamekufa na wengine wakipata shida pasipo hata kumdhihaki Mungu.
Kinachokufanya uone hao watu uliowataja kua wamepatwa na shida kutokana na wao kumdhihaki Mungu ni kipi? Nani asiyepata tabu hapa ulimwenguni?
Huyo Mungu wako historia ya dini inaonesha yeye ndio alikua muanzilishi wa kupata tabu baada ya vita yake na shetani ambapo shetani alizua utata huko juu mpaka akafanikisha kusepa na robo tatu ya malaika unafikiri tabu aliyoipata huyo Mungu ilikua ndogo?
Kwa hiyo nayeye tuseme alimdhihaki nani mpaka ikamfika hiyo tabu?
Thibitisha wewe upo kwanzaThibitisha Mungu yupo, na kwamba habari za kusema Mungu yupo si hadithi za mapokeo tu.
Unataka Mungu awe kama wewe unavyotaka ndo ujue yupo ?unavyoonekana kuna kitu ulikua unamtegemea kikaenda tofauti ndo maana una vita nae .Unaamini unachoamini au umethibitisha?
Unaelewa kuwa kuamini si kuthibitisha?
Hata nikishindwa kuthibitisha mimi nipo, hilo halithibitishi Mungu yupo.Thibitisha wewe upo kwanza
Hapana,Unataka Mungu awe kama wewe unavyotaka ndo ujue yupo ?unavyoonekana kuna kitu ulikua unamtegemea kikaenda tofauti ndo maana una vita nae .
Kamwe hawapatwi na shida!!! Mara nyingi kuliko zote wanatwaliwa tu!! km Musa hakuna kaburi lake hapa Duniani, alipanda Mlimani hakurudi ni wazi alitwaliwa!!Kwani wasiomdhihaki Mungu hawapati shida?
Achana nae huyo Mzee hana jipya anaona ignore List ndo kitu cha maana!! hasa akisha shindwa hoja!!! hajui kwamba hata shetani alimuhasi Mungu lkn bado anaishi!Aliyekuloga amekufa.Tutapata shida sana kukuagua kwa mitishamba.