Nashindwa kuelewa Kwanini linapokuja swala la kuthibitisha uwepo wa Mungu inakuwa ni vigumu sana na mwisho wa siku watu kukimbilia kusema mtalaanika na mambo kama hayo
Miongoni kwa majibu mepesi kabisa ya kuthibitisha kuwa Mungu yupo ni kama haya, mtu atakuuliza we umetokea wapi? Nani kaumba dunia au dunia imetokea wapi? Na utaskia Kila kitu kina mwanzo wake
Sasa linapokuja swala la mie nimetokea wapi, au dunia imetokea wapi hivi ndo kweli uthibitisho wa uwepo wa Mungu? Inajulikana kuwa maandiko yanasema Mungu hakuumbwa Wala hajazaliwa, ila hapo hapo tumetoka kuambiwa Kila kitu kina mwanzo wake kwahiyo mwanzo wa Mungu ni upi?
Kama unaambiwa kuwa Mungu hakuumbwa na wala hakuzaliwa kwahiyo maana yake alitokea tu from no where na unaamini Kwanini ila kwa nini ukiambiwa kuwa dunia pia imetokea tu na yenyewe from no where hutaki? Kwanini namie nikisema nimetokea tu from no where hutaki kuamini ilihali unaamini Mungu ametokea tu from no where?
Huwezi kuthibitisha ulikotokea wewe pamoja na dunia uliyopo ila unataka kutetea na kupambaba kuthibitisha uwepo wa aliekuumba wewe na dunia uliyopo kwa kigezo cha Imani, hapo ndio shida inapokuja, acheni tuendelee tu kuishi na kuabudu tu hakuna namna labda kuna siku majibu ya kuridhisha yatakuja