Sasa ulishindwa nini kuandika hoja zako kama hivi mpaka uanze akili zangu zina majipu? Nimekudharau sana.Hakuna mipasho.
Akisimama tena CDF akasema mafisadi wanaimaliza nchi halafu watu wakaanza kuwataja mafisadi.
Utakuja na swali hilo hilo mlikuwa wapi kuwataja? CAG anakula hela za serikali kwa kutoa ripoti zinazotupwa kapuni.
Vyombo vya usalama vinalipwa kwa kazi gani kama wameshindwa kung'amua hadi aje ataje madeleka?
Katibiwe bana. Tutakuchangia gharama za matibabu
Alikuwa wapiSasa ulishindwa nini kuandika hoja zako kama hivi mpaka uanze akili zangu zina majipu? Nimekudharau sana.
Jifunze zaidi kuhusu CDFWewe ni Nchi gani CDF anafanya kazi ya Home Affairs? Au na wewe umesha zezeteshwa?
Pambana.Alikuwa wapi
Ulishindwa nini
Huwezi kuwa unawaza sahihi si bure.
Sitafuti kutukuzwa ndugu. Mimi sijakupuuza lakini nakuangalia kwa tahadhari kubwa
Mkimbizi yeye au wazee wake walikuwa wakimbizi?Mmezoea siri siri kibaao hafi wakimbizi mnateuana.
Sasa kiranga komo kimesajili
Hili nalo nendeni mkalitizame
Hata "makamu" iliandikwa sana kuwa kwao ni Burundi...lakini ikapotezewaHii nchi imekuwa shamba la bibi kwa kila namna, kuanzia kutoa hovyo rasilimali zetu, kupokea na kuwapa vyeo wakimbizi, tumegeuka kama wanyama tusiojua thamani ya ardhi tuliyopewa na Mungu.
Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Sheria zifatwe wasionewe watu.
do your own research, enquiry!Akitajwa unitag mkuu nije nimuone walau jinale!
Joseèe kabila alumni wa Sangu sekoNani huyo?
Bashiru ni mtusi? Inawezekana maana ni wa KyakaMtu wa kwanza kubana mbavu ni Bashiru atweleze aliwaingiza watusi wangapi TISS
Umenena vyema ila tatizo sio PK tu bali huo ukanda wote wa Burundi, Rwanda na DRC una watu wapumbavu sana wenye roho za kinyama. Mikoa mingine ya pembezoni ina wahamiaji wengi lakini si unaona hata CDF hajaitaja? Sumbawanga pale pamejaa wazambia lakini fresh tu maisha yanasonga.Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi tu wanmesoma hadi shule kenya, wana ndugu zao kenya na Tanzania, ila hawana shida. ukienda Mtwara, wamakonde na wayao wapo pande zote mbili za msumbiji na Tanzania, ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na wazambia na wamalawi,wameoleana mno, in fact wafanyabiashara wazuri wengi wa Lusaka kwa wale waliofika kule, ni wakinga na wanyakusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule zambia. ukienda kwa ndugu zangu wachagga, na wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili, kama wameru ndio hadi kenya kuna eneo na kabila la wameru, ukienda Tanga ndio usiseme wanaingiliana na makabila, hivyo ukienda kigoma, bukoba na Rukwa, usishangae kuona kuna wanyarwanda, warundi na wacongo wengi tu ila ni watanzania. mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote.shida nadhani ni PK na sio makabila ya nchi hizo, watu hawampendi PK, kitu ambacho hata mimi huwa simkubali kabisa kabisa kwa ukatili wake. asingekuwepo PK hao wote wangeishi bongo kwa amani tu na suala hili lisingejitokeza.
hata hivyo, serikali ina mkono mrefu, kama wapo wanaoishi hapa kiitellijensia hao hawana nia nzuri, serikali ikamate mmoja mmoja kimya kimya uone kama wote wenye nia mbaya hawajakimbia kimya kimya. wataambizana kwamba mwenzetu kakamatwa na watasepa, ila wale wema hawana haja ya kufukuzwa. wengine ni wake za watu na waume za watu wanaprovide kwa dada zenu hapahapa tz.
Mimi siyo Mtanzania, mimi Mtanganyika. Kumbuka hilo.Ngoja tukupige vetting hadi wewe
Wengi wanao comment humu wengine sio wa TZ
Tunatosana baharini tu
Umenena vyema ila kiukweli hao Burundi, DRC na Rwanda wana roho mbaya. Hakuna nchi watakayoenda wasisumbuliwe. Hapo Zambia wananyanyasika sana wakati kuna watanzania wengi hata vibali hawana lakini wanaishi fresh bila usumbufu.Nilichojifunza baada ya kutembea nchi kadhaa hasa za watu wenye uelewa wa dunia, katika maisha unachotakiwa kujali ni namna gani unaingiza kipato chako na usalama wa familia yako na nchi yako tu, otherwise, unaweza kuishi popote na ukapaita nyumbani. ndio maana nashauri serikali iweke vizuri intelijensia yake ili kukamata waovu na wanaochunguza nchi, ila si kufukuza wageni. mgeni akiwa hapa kama hana matatizo, pesa yake ataspend hapa, though cha muhimu ajulikane yupo ili apewe masharti ya kuishi.
Hivi Bashungwa si aliwahi kuwa waziri wa ulinzi ? Na alitembekea kambi zote ? Na anajua maeneo nyeti na muhimu et ? Duuuh ngoja nikakijoe nilale
Mimi siyo Mtanzania, mimi Mtanganyika. Kumbuka hilo.
Labda huko ndani wameshindwa wameona walitoe nje..Watanzania tupo warahisi sana kuchezewa akili zenu. Lakini acha tu tuchezewe kwani huwa hatutaki kutafakari. Hivi jambo kama ni hili ni la utekelezaji au ni la kusemea kwenye majukwaa! Tuna idara za usalama, upelelezi na ulinzi.
Kama wamegundua kuna watu wa aina hii kwa nini wasiondolewa kwanza? Rais kila siku ni lazima apewe briefing kuhusu masuala mbali mbali ya nchi, ina maana hawakumwambia huko kwenye vikao?
Kwangu mimi hili ni suala la utekelezaji zaidi na siyo suala la kusemea jukwaani. Otherwise, kuna jambo fishy linataka kufanywa na huu ni mwanzo tu wa kulihalalisha.