Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hakuna mipasho.
Akisimama tena CDF akasema mafisadi wanaimaliza nchi halafu watu wakaanza kuwataja mafisadi.

Utakuja na swali hilo hilo mlikuwa wapi kuwataja? CAG anakula hela za serikali kwa kutoa ripoti zinazotupwa kapuni.

Vyombo vya usalama vinalipwa kwa kazi gani kama wameshindwa kung'amua hadi aje ataje madeleka?

Katibiwe bana. Tutakuchangia gharama za matibabu
Sasa ulishindwa nini kuandika hoja zako kama hivi mpaka uanze akili zangu zina majipu? Nimekudharau sana.
 
Sasa ulishindwa nini kuandika hoja zako kama hivi mpaka uanze akili zangu zina majipu? Nimekudharau sana.
Alikuwa wapi
Ulishindwa nini

Huwezi kuwa unawaza sahihi si bure.

Sitafuti kutukuzwa ndugu. Mimi sijakupuuza lakini nakuangalia kwa tahadhari kubwa
 
Usalama wazawa uliishia enzi ya Mkapa, enzi ya mwalimu TISS was real.

Recruitement ya TISS kwa sasa ni ya mchongo; full connection , zamani TISS ilikuwa ina focus kwenye intelligence na smartness bila ya kujali wewe ni wanani

Vijana wa TISS wa sasa ni wa kushinda Bar ,wengine ni form 4 failures


Unakuta hata kizimkazi anaweza kuwa na vijana wake hawana uwezo but aka recommend waingie TISS kama ilivokuwa kwa Ngosha, ngosha alikuwa anapeleka vijana TISS bila stages za vetting kukamilika

Mkwere alikuwa anaingiza vijana TISS based na ushikaji
Tanzania kupo uchi sana

The only way ni kuiondoa CCM. Madarakani to change all regimes

Shida , upinzani upi wa kuiondoa CCM ?

Kama ni huu wa mbowe na zito kabwe,
………. I am done , it will never happen
 
Ukienda Musoma, wajaluo na wakurya, wengi tu wanmesoma hadi shule kenya, wana ndugu zao kenya na Tanzania, ila hawana shida. ukienda Mtwara, wamakonde na wayao wapo pande zote mbili za msumbiji na Tanzania, ukienda Mbeya kuna muingiliano mkubwa sana na wazambia na wamalawi,wameoleana mno, in fact wafanyabiashara wazuri wengi wa Lusaka kwa wale waliofika kule, ni wakinga na wanyakusa, na wanaongea kinyakyusa, kikinga na kiswahili hiki cha kwetu na likizo za mwaka huwa wanarudi na hawafanywi kitu kwasababu wanalipa kodi kule zambia. ukienda kwa ndugu zangu wachagga, na wameru, sio ajabu majina ya koo kuingiliana pande zote mbili, kama wameru ndio hadi kenya kuna eneo na kabila la wameru, ukienda Tanga ndio usiseme wanaingiliana na makabila, hivyo ukienda kigoma, bukoba na Rukwa, usishangae kuona kuna wanyarwanda, warundi na wacongo wengi tu ila ni watanzania. mikoa ya mipakani ni kawaida kuwa na watu wa nchi zote.shida nadhani ni PK na sio makabila ya nchi hizo, watu hawampendi PK, kitu ambacho hata mimi huwa simkubali kabisa kabisa kwa ukatili wake. asingekuwepo PK hao wote wangeishi bongo kwa amani tu na suala hili lisingejitokeza.

hata hivyo, serikali ina mkono mrefu, kama wapo wanaoishi hapa kiitellijensia hao hawana nia nzuri, serikali ikamate mmoja mmoja kimya kimya uone kama wote wenye nia mbaya hawajakimbia kimya kimya. wataambizana kwamba mwenzetu kakamatwa na watasepa, ila wale wema hawana haja ya kufukuzwa. wengine ni wake za watu na waume za watu wanaprovide kwa dada zenu hapahapa tz.
Umenena vyema ila tatizo sio PK tu bali huo ukanda wote wa Burundi, Rwanda na DRC una watu wapumbavu sana wenye roho za kinyama. Mikoa mingine ya pembezoni ina wahamiaji wengi lakini si unaona hata CDF hajaitaja? Sumbawanga pale pamejaa wazambia lakini fresh tu maisha yanasonga.
 
Mwishoni mwa Utawala wa awamu ya nne, Serikali si ilitoa uraia kwa warundi zaidi ya 200,000 kwenye kambi za Mishano kule Rukwa?

Kama Serikali wakati huo ilifikia kujitapa kuwa imevunja rekodi ya ukarimu ya UNHCR na kusifiwa....

Hao raia wapya si walikuja kujumuishwa kwenye shughuli za kiraia ikiwemo kuajiriwa Serikalini?

....Hawakupiga kura hawa?

Hawakupewa vitambulisho vya taifa, kupiga kura na pasi za kusafiria?


Hii hoja ya kibaguzi kama ikiendelezwa na hasa kwa hatua hii ya Jeshi kuingilia mambo ya kisiasa, nchi itasambaratika muda si mrefu.
 
Nilichojifunza baada ya kutembea nchi kadhaa hasa za watu wenye uelewa wa dunia, katika maisha unachotakiwa kujali ni namna gani unaingiza kipato chako na usalama wa familia yako na nchi yako tu, otherwise, unaweza kuishi popote na ukapaita nyumbani. ndio maana nashauri serikali iweke vizuri intelijensia yake ili kukamata waovu na wanaochunguza nchi, ila si kufukuza wageni. mgeni akiwa hapa kama hana matatizo, pesa yake ataspend hapa, though cha muhimu ajulikane yupo ili apewe masharti ya kuishi.
Umenena vyema ila kiukweli hao Burundi, DRC na Rwanda wana roho mbaya. Hakuna nchi watakayoenda wasisumbuliwe. Hapo Zambia wananyanyasika sana wakati kuna watanzania wengi hata vibali hawana lakini wanaishi fresh bila usumbufu.
 
Watanzania tupo warahisi sana kuchezewa akili zenu. Lakini acha tu tuchezewe kwani huwa hatutaki kutafakari. Hivi jambo kama ni hili ni la utekelezaji au ni la kusemea kwenye majukwaa! Tuna idara za usalama, upelelezi na ulinzi.

Kama wamegundua kuna watu wa aina hii kwa nini wasiondolewa kwanza? Rais kila siku ni lazima apewe briefing kuhusu masuala mbali mbali ya nchi, ina maana hawakumwambia huko kwenye vikao?

Kwangu mimi hili ni suala la utekelezaji zaidi na siyo suala la kusemea jukwaani. Otherwise, kuna jambo fishy linataka kufanywa na huu ni mwanzo tu wa kulihalalisha.
Labda huko ndani wameshindwa wameona walitoe nje..
 
Back
Top Bottom