Mwishoni mwa Utawala wa awamu ya nne, Serikali si ilitoa uraia kwa warundi zaidi ya 200,000 kwenye kambi za Mishano kule Rukwa?
Kama Serikali wakati huo ilifikia kujitapa kuwa imevunja rekodi ya ukarimu ya UNHCR na kusifiwa....
Hao raia wapya si walikuja kujumuishwa kwenye shughuli za kiraia ikiwemo kuajiriwa Serikalini?
....Hawakupiga kura hawa?
Hawakupewa vitambulisho vya taifa, kupiga kura na pasi za kusafiria?
Hii hoja ya kibaguzi kama ikiendelezwa na hasa kwa hatua hii ya Jeshi kuingilia mambo ya kisiasa, nchi itasambaratika muda si mrefu.