Kwa hiyo na Ukraine , Congo ,Burundi nk ambapo kuna machafuko nao hawana elimu ya dunia na ni waisilam na ndio maana wanauwana?
Hapa duniani kuna nchi za kiislam zaidi ya 45 na kati ya hizo ni nchi zisizo zidi 6 ndo zenye machafuko na chanzo cha machafuko ndani ya nchi hizo ni uwaniaji wa madaraka na uvamizi kutoka nje hasa Marekani na washirika wake lakini cha kushangaza mnalazimisha ionekane ni dini ndo inasababisha.
Iraq imeingia kwenye machafuko mwaka 2002 baada ya uvamizi wa Marekani kwahiyo uislam ndo ulio ituma Marekani hiivamie Iraq na kusababisha machafuko ya aina hii?
Au uislam ndani ya Iraq imeingia mwaka 2002 huko nyuma haukuwepo na ndio maana Iraq haikuwa na vita?
Afghanistan ilivurugika miaka ya 1985 baada ya uvamizi wa Usoviet baada ya kupigana na kuwafurusha wasovieti ilitulia na kuwa na Aman, ikaja kuvugika mwaka 2002 baada ya uvamizi wa Marekani na imeanza kutulia sasa hivi baada ya Marekani kujiondoa ndani ya nchi hiyo.Ebu niambie tangu Marekani ajiondoe nchini Afghanistan umesha sikia mauaji ya kiholela yanaendelea ndani ya nchi hiyo kama mwanzo?
Sudan vita imesababishwa na majenerali 2 wanao wania madaraka kwa hiyo Uislam ndo umewatuma wapigane kugombania madaraka?
Na kama haya yote kwenye nchi hizo ni kwa sababu ya waisilam vipi kuhusu nchi nyingine zenye machafuko na hazina waisilam na penyewe machafuko hayo yana sababishwa na dini wanazo ziamini?
Kwa nn hujawahi kujiuliza kuwa ni kwa nn mambo ya sijui kujilipua yamevuma miaka ya 1990 kuja juu na sio huko nyuma kwahiyo uislam umekuja hapa duniani mwaka 1990 huko nyuma haukuwepo na ndio maana na ugaidi haukuwepo?
Machafuko yanayo endelea kwenye nchi mbali mbali hapa duniani ni matokeo ya wanasiasa wenye tamaa za madaraka na sio ujinga raia wa nchi hizo, hakuna raia asiye penda kuishi nchini kwake kwa amani.
Leo hii CCM wakivurugana huko juu na kuingia kwenye vita ya kuwania madaraka mm, ww na raia wote wote ndani ya nchi tutapoteana bila kujali umesoma ,au haujasoma,ww ni tajiri au masikini ww una akili au ni kichaa wote tutaharibikiwa maisha hali yakuwa hatuhusiki kwa lolote lile.
Hii tabia yenu ya kuwakejeli binadamu wenzenu walioko kwenye matatizo kisa nyinyi mnaishi kwenye nchi zenye amani ni ni tabia ya kijinga,maana hata hao unao wacheka na kuwakejeli nchi zao zilikuwa na amani kama ilivyo nchi yako.
Na kila mwanadamu hapa duniani ni mkimbizi wa kesho maana siasa hazijawahi kutabilika sehemu yeyote hapa duniani.