Hawa wote hawalipi KODI hapa Tanzania

Kwenye daily income yao wanalipaje kodi?
Ukisema mafuta kumbuka hata vituo vya mafuta vinavyotumia jenereta hununua mafuta na EFD receipts lazima wakate ambazo ni 18% ya kodi kila anapohudumia mteja.

Je wenye daladala hukatwa 18% kila wanapopakia abiria??
Kodi ya mafuta usiiongelee maana hata wanaotumia mafuta kusaga unga nao hulipia hayo mafuta yakiwa na kodi
 
Nimepitia mjadala kuanzia page ya kwanza hadi ya mwisho; nimegundua kua kuna ulazima wa elimu ya kodi ianze kufundishwa kuanzia shule ya msingi au awali tena kwa haraka zaidi.

Ile blabla ya somo la historia ya Tanzania ilitakiwa iwe ni somo inayohusu kodi na tungefika mbali sana.

Mfano rahisi tu. Mtu analipia fremu ya biashara na mwenye fremu nae anatakiwa alipe kodi pindi anapopokea hiyo pesa ya pango. Mpangaji anapouza bidhaa anatakiwa alipe kodi pindi anapopokea pesa kutoka kwa mnunuzi wa bidhaa. Jioni anapoenda nyumbani kwa usafiri wa pikipiki au gari akiweka mafuta sheli inakua na kodi.

Sasa unasangaa wanasema kua boda sijui anastika hatakiwi kulipa kodi kutokana na pesa anayopata kutoka kwa Abiria. Kama kodi ya kwenye mafuta ata anaetembea na gari la private nae ananunua mafuta. Sijui LATRA...na n.k ni sawa na pango la mwenye duka.

Elimu ya kodi ipelekwe haraka sana shuleni siyo kufanywa elimu ya ngazi ya juu tu.
 
Unalipa nauli ya DAR to Mwanza TZS50,000 alafu unapewa ka risiti ambayo haioneshi kua kodi ni kiasi gani...upuuzi mtupu. Hapo njiani Abiria wanapanda na kushuka wengi.
 
kuna hoja nzito hapa lakin watu huwa wanasubiri mambo yawe mabaya zaid ya ubaya ndo hupiga yowe. nafikiria mkurupuko wa makato ya kodi ya uzalendo utadhan imeibuka jana yake! kuna kitu watz hatuko sawa. kila kitu tunafanya kwa mihemko. tuwe tunapashana mapema sana. naona kuhusu ubovu wa katiba kupashana kumeanza mapema afadhar
 
JAZENI POST.WEE

MSIKOSEE NA MSIWAGUZE

MADADA POA PLS HAWA NDIO WANATU NZA NDOA ZA WAZAZI WETU NA WENGINE HUMU

AHSANTENI
TUVAEBARAKOA
COVID INAUA
RGDS
MWEKA HAZINA
(UMOJA WA WATUNZA NDOA TANZANIA)
 
WALE WACHEZAJI WANAOKUJA KUTOKA NJE KAKAMATENI KODI HUKO NAKO KUWASAIDIE
 
We jamaa
Machinga analipa income tax ipi
Hapati kipato?bodaboda je?

wabunge wanalipa PAYE ipi?.
Wana mishahara hawana?
VAT na tozo ta uzalendo ndo kila mtu analipa

ila sio income tax
rudi shule wewe
 
Ndiyo maana mwendawazimu mmoja asiyelipa kodi kasema tuhamie Burundi
Yaani ndugu yangu mie mpinga tozo kubwa, nishatangulia Burundi aisee ingawa nitarudi jumapili Kigoma kuangalia mechi ya Simba Vs Yanga......... nimekubali yaishe.
 
Unalipa nauli ya DAR to Mwanza TZS50,000 alafu unapewa ka risiti ambayo haioneshi kua kodi ni kiasi gani...upuuzi mtupu. Hapo njiani Abiria wanapanda na kushuka wengi.

Watu elimu ya Kodi hawana..
Kwenye fremu kuna dalali mfano unampa Kodi ya mwezi mmoja halipi kodi..
Wenye Daladala wanagawana jioni
Dereva elfu 50
Konda elfu 25
Mmiliki elfu 80..
Zote hawakatwi kodi..

Mtu anataja mafuta as if mafuta yananunuliwa na wenye Daladala peke yao
 
Kwani Rais sio mtumishi?
Das? DC sio watumishi?Why hawalipi PAYE?

Hao wote hawalipi kodi..
Hata mshahara wa askofu unatakiwa kukatwa PAYE..wa Imam vile vile..

Bodaboda wanatakiwa wakupe Risiti za efd..
Madalali wa nyumba..

Hoja yako ni takataka! Weka ushahidi kua uliowataja hawalipi Kodi
 
We jamaa
Machinga analipa income tax ipi
Hapati kipato?bodaboda je?

wabunge wanalipa PAYE ipi?.
Wana mishahara hawana?
VAT na tozo ta uzalendo ndo kila mtu analipa

ila sio income tax
rudi shule wewe


Watu wengi hata elimu ya Kodi bado sana
 
We jamaa
Machinga analipa income tax ipi
Hapati kipato?bodaboda je?

wabunge wanalipa PAYE ipi?.
Wana mishahara hawana?
VAT na tozo ta uzalendo ndo kila mtu analipa

ila sio income tax
rudi shule wewe


Watu wengi hata elimu ya Kodi bado sana
 
Kwanza tunahtaji tafsiri machinga ninani.

Zaman alikuwa ni mfanyabiashara yeyote asiye na kitu.anayetembeatembea.

Leo kila mtu amegeuka mmachinga.

Leo Wana vituo.wamegawana mabarabara.
wenzao wanalipia kodi ya sehem ya biashara.wao bure.

Serikali imekiri kuwa vitambulsho vyote vya wamachinga ni milion 2 tu.

Wao ni zaidi ya milion kumi.walipaji ni m2.

Maoni:

Wamachinga walipishwe kodi maalum ya maeneo wanayopanga bidhaa zao nje ya ile elf 20

Barabara ni mali ya wote.matumizi yake yanajulikana.
sasa hawa watu wayalipie coz wanayatumia kinyume na ilivyokusudiwa.

faida ya pili, wataleta usawa (equality) kati yao na wanaogharimika kulipia frame zao.
maana bidhaa ni zilezile.

napendekeza kila chinga atoe sh 300 kila siku kwa ajr ya eneo.

300 mara 365=ni roughly laki moja kila mwaka.

mtu achague.alipe 300 daily au asipange bidhaa chini.atembee navyo kama tafsr inavyowaeleza.

pia mifumo ya tehama iwekwe sawa il hizo 300's zilipwe straight kielektronik

mtu asilazmishwe kulipa kulimbikza.hata kama ana hela ya siku moja ipokelewe.

mjini hakuna cha bure.hawa wamachinga hughalimika kwny mambo mengne mbona.

kuchimba dawa wanatoa hela,kula,nauli,vicoba,
wengne wanalewa mchana.

iwe malufuku kukanyaga viunga vya mijini bila kuvaa id
 
Kodi gani?
Namba 18 (wamiliki wa daladala) sio kweli, hadi unaiona daladala barabarani tayari inalipa tozo kibao aisee...!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…