Haya mafuriko ya leo Ifakara ni hatari

Haya mafuriko ya leo Ifakara ni hatari

Utasikia viongozi wa serikali ya CCM ikiwaambia wananchi wahame maeneo hayo.

Majanga haya ya mvua kubwa, El Nino n.k yanalilia serikali ijipange wa kufikiria pale inapowezekana kujenga mabwawa mengi kuvuna maji haya kwa ajili ya kilimo, ufugaji pia mabwawa ya maji yatalinda miundo-mbinu kama reli, barabara, madaraja , mashamba na makaazi yasiharibiwe.

Hii ni kilio cha Asili kuwa ni fursa kuvuna maji haya yote ya mvua kwa maendeleo ya nchi. Ni wakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (Climate Change) ibadilike kuwa fursa kwa kujenga mabwawa mengi.

Bwawa la kihistoria la Hombolo:

View: https://m.youtube.com/watch?v=TKwMmfccVSM
Mabwawa mengi dizaini ya yale ya mkoloni aliyojenga Mkalama Dam mwaka 1928 likafuatia Biringi Dam mwaka 1945 na Hombolo mwaka 1957 kuvuna maji ya bonde la Bahi Basin yanatakiwa yajengwe mengi zaidi kuvuna neema hii kipindi cha miaka yetu ya 2025 - 2050 na kuendelea

View: https://m.youtube.com/watch?v=CgjLPydnIeQ
 
Hahaa haya poleni sana wanetu
Hahaha tulitegemea tuona mafuriko yaani maji yapo kidevuni, yaani mtu kabeba kitoto juu kwa juu halafu macho yamebaki anajiokoa kwenye maji. Sasa eti anasema mafuriko huku watu wanatembea na ndala hahah
 
Utasikia viongozi wa serikali ya CCM ikiwaambia wananchi wahame maeneo hayo.

Majanga haya ya mvua kubwa, El Nino n.k yanalilia serikali ijipange wa kufikiria pale inapowezekana kujenga mabwawa mengi kuvuna maji haya kwa ajili ya kilimo, ufugaji pia mabwawa ya maji yatalinda miundo-mbinu kama reli, barabara, madaraja , mashamba na makaazi yasiharibiwe.

Hii ni kilio cha Asili kuwa ni fursa kuvuna maji haya yote ya mvua kwa maendeleo ya nchi. Ni wakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi (Climate Change) ibadilike kuwa fursa kwa kujenga mabwawa mengi.

Mabwawa mengi dizaini ya yale ya mkoloni aliyojenga Mkalama Dam mwaka 1928 likafuatia Biringi Dam mwaka 1945 na Hombolo mwaka 1957 kuvuna maji ya bonde la Bahi Basin yanatakiwa yajengwe mengi zaidi kuvuna neema hii kipindi cha miaka yetu ya 2025 - 2050 na kuendelea

View: https://m.youtube.com/watch?v=CgjLPydnIeQ

Mwenge uende na kauli mbiu mabwawa zaidi Kilombero, Ulanga na kote Tanganyika

View: https://m.youtube.com/watch?v=oh7oNlHbzv4
 
Umaarufu wa hapa Dar ni haya mafuriko?! Acha utoto tafadhali.
Yaani watu wengine ni wa ajabu sana.

Yaani kuleta taarifa hapa ni kutaka kushusha mafuriko ya Dar???

CCM watu wa ajabu sana. Tangu asubuhi Mkurugenzi na DAS, Polisi, watu wa uokoaji, maliasili na boti yao wote wapo hapa kuangalia bwawa!?
 
IMG_20240425_093414_405.jpg

Gari na nyumba vikiwa vimezungukwa na maji Ifakara.
IMG_20240425_093458_957.jpg

Kanisa eneo la Kwa shungu likiwa limezingirwa na maji.
 
Sijaupatia picha mto Lumemo kwa namna ulivyofurika! Maana kila maji yanapojaa kwenye huo mto, basi mafuriko lazima yaukumbe huo mji wa Ifakara.
 
Back
Top Bottom