Haya mahesabu ya Wazungu dhidi ya Urusi ni hatari

Haya mahesabu ya Wazungu dhidi ya Urusi ni hatari

Unaona akili zako ? Tuna ardhi tunauza chakula Kenya, Uganda, congo mpaka Rwanda afu tuwategemee kwa chakula? Una akili kweli? Nje na ngano ambayo ni dili la Ccm ni chakula gani kinatoka kwao?
Sijaongelea chakula mkuu tuombe Mungu isijeibuka. Vita ya 3
 
Wale miaka yote walikuwa wanajiita wa Ukraine sasa wanasema tunarudi kwetu Israel

Ifike wakati Africa isaidiane kibiashara zaidi kwa kila kitu sio kutafutiana uchawi kuwa waacheni wapigane na sisi tuwauzie chakula
Maneno ya Rais mmoja alikuwa na roho ngumu huyo

Vita ikitokea tujiandae Ulaya kuwa na maisha magumu zaidi

Leo hii angalia [emoji636] bei ya diesel imefika £2 kwa lita (6,000)
Haijawahi kutokea
Hapa nasubiri vita vianze niibe meli moja nije nayo bongo nianze biashara na sitanii I will do it [emoji23]
Nani anataka ajira?
Aloweeehh[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Hawa jamaa leo wanataka kufanya jambo la kihistoria yaani kumwingiza Ukraine kwenye umoja wa Ulaya kama V.I.P membership wiki hii, kumbuka kuwa membership huchukua had miaka 5, hivyo Ukraine anapita directly bila mlolongo.

Kwa nini wanafanya hivi? Nia kubwa ni kutaka kuingia kumchapa mrussi direct, hili liko wazi kabisa, Mrusi anatafutwa akae kwenye Target.

Tuombe sana Mungu moyo wa Putin ashushe ghadhab dhid ya Ukraine maana itakua vita ya kihistoria.

Kumbuka Mkuu wa Majeshi wa Uingereza alitangaza majuzi kuwa ni wakati wa Ulaya kujiandaa kwa vita.

Mungu atusaidie tu maana tunawategemea sana Urusi na Ukraine kwa chakula na nishati.
Kelele mtapiga wenyewe urusi anakimbiza kimya kimya
 
Mzee kama EU wamechoka kuishi au wameichoka dunia bhs wajidanganye kuingia vitani na Russia nahis watoto wetu kwenye history watakua wanafundishwa kulikua na bara linaitwa ulaya”

Hakuna nchi Ulaya inayoweza pigana na Russia direct hata US mwenyewe hana huo ubavu. Mnajua wengi mmedanganywa na propaganda za west kuhusu majeshi yao ila kiuhalisia ni kawaida sana.

Wengi wenu humu mmeanza kuijua Russia wakati wa kipindi hiki cha mgogoro na Ukraine.

VITA PEKEE EU WANAYOWEZA NI VIKWAZO.
Punguza mapenzi na Russia! Russia anaweza kuipiga Ulaya nzima kweli?? Ana nguvu gani hizo?? Okay tusema sawa,anaweza ipiga! Then unadhan baada ya vita hii Russia ya sasa hivi itakua na nguvu gani tena?? Hebu weka mahaba pembeni! Generals waliopo huko Moscow, London, Pentagon na Tel Aviv ndiyo wawe hawajui,ila wewe mmatumbi wa huko Utete Lufiji ndiyo uwe unajua sana! Hapana,tusiwe brainwashed namna hiyo! Asante
 
Mkong'oto upi, jameni kila nikikaa nilinganishe Urusi ambayo niliiskia miaka yote na hii nabakii kushangaa sana, kainchi kadogo pembeni walipaswa wawe wamekafunika na kusimika uongozi wao unaoimba wimbo wa taifa wa Urusi.
Leo wameishia kuburuzana huko kwenye tumiji twa mipakani, naomba mtu yeyote mwenye akili timamu aitazame hii picha mara kumi na kupata aibu...
Kila nikiitazama yaani nashangaa sana

where-are-ukraine-&-russia.jpg
Waue raia wote? Hapana, operation itaenda slow but sure. Yote ni kuepuka madhara kwa raia wasio na hatia.
 
Nyie sijui mnakuwa na fikra za aina gani. Yaani Russia aivamie Moldova au Lithuenia au Estonia ndio vita ipiganwe kati ya russia na nato sababu tu warussia wamemgusa mwanachama mwenzao! Hii haiwezi kutokea. Labda aguswe German, France n alike. Sio hivyo vitakataka vinavyojiita nchi.
Hata akipigwa poland hapo hakuna member wa nato atakayekuwa tayari kupigana na russia.....wanaogopa firework za motherland

Sent from my LG-M200 using JamiiForums mobile app
 
Ameshatumia laser weapons, hypersonic missiles n.k zote hizi ni silaha za kisasa katika ulimwengu huu. Bado wanaendelea kumsoma tu.
Ukizingatia kwa taarifa zao western ni kuwa russia yupo ahead of then kwenye suala la missiles na electronic warfare....hell! Hata iran anauweza sana huo mchezo wa kujam system za usa na ndio maana alihack drone ya usa

Sent from my LG-M200 using JamiiForums mobile app
 
Unauliza alichochukua Russia ukraine? Mpaka sasa Russia anamilikia 30% ya eneo la Ukraine tena potential areas yes tunazungumzia bandari, kilimo na nishati kwa Ujinga wa comedian wenu sahv ananunua umeme wake ambao unashikiliwa na Russia. Sasa hii ni akili au matope.?

Kosa kubwa la Ukraine kuiamin US hapa ndo alifeli walimpa kiburi mwisho wa siku wamemwacha na maeneo yanamegwa juzi hapa wamemwambia akubali kuyaacha maeneo aliyochukua Russia ili operation iishe ila kakaza bado eti tutayarudisha.

Kuhusu America kuitawala dunia bado hajafanikiwa bado anakutana na upinzani kutoka Russia, china, NK nk hao EU ndo wamekubali kushikwa MATACORE na US. US anataka kuitawala dunia kishetani atuletee masuala ya NWO naam hayo mambo ya ushoga anayohangaika kuyaeneza unafikiri ni nini?? Na mnachekelea tu, nenda kaisome NWO vzr utapata mwanga otherwise nitakua natwanga maji kwenye kinu.

Hakuna jambo lilisokua na mwisho wala hakuna marefu yasiyo na ncha. Zilipita falme za maana enzi hzo zilianguka sembuse US ambaye ni mchumba tu hivi mzee kuna falme za kutisha zilianguka tunaanzia na wamedi na waaajemi, kulikua na wagiriki, warumi kuna akina Ottoman Empire wote walianguka.

Unafahamu kuwa uchumi wa US upo kwenye karatasi naam nazungumzia [emoji385] hapa ndo kiburi chake kilipo na hapa ndo uchumi wake ulipo. US anaprint pesa anajaza kule IMF mkakope nyie ndo mnamweka mjini. Ndomana tunamwita Mr. Canon wanaprint pesa wanapojiskia wanawapa afu mnawaona kila kitu maskin Africa[emoji1316]. Wametumia uhuni kuforce transactions zote za kimataifa tutumie dollar unajua why??? Inshort dollar ndo uchumi wao kidogo nakupiga msasa, soma kitu kinaitwa Fiat money na stable currency.

Russia amesha switch kwenda kwenye pesa yake Ruble, Saudia wameshaingia mkataba na china watatumia yuan, India naye amesema atauza bidhaa zake kwa rupee. Nchi karibu zote za uarabuni zinaipiga dollar chini sasa tunarudi mezani unajua impact yake???

Unajua transactions za matrillion zinafanyika kwenye nishati hasa oil, gas nknk kama tunatumia Ruble, yuan nknk unajua ni impact gani inakwenda tokea kwenye dollar?? Nchi dunian zimeamka zimechoka dhuluma ya US kawaua ndugu zetu gaddafi kisa jamaa alitaka kuswitch kwenda gold kuachana na dollar. Yote coz uchumi wake upo kwenye dollar hana JAMBO.

Nimekupa picha kidogo ujue ukweli kuhusu hao unaowaabudu ila kipindi hiki kakutana na kisiki cha mpingo. Dunia ya sasa inataka usawa na sio uwizi na unyang’anyi wanakwapua mali za Africa wanaleta migogoro ili mambo yao yafanikiwe bado wanawapa masharti mkubali ushoga sasa haya yote ni nini?

Utawala wa USA utaanguka. Tawala kubwa na za hatari zilipita kama upepo sembuse US na hizi ni dalili tu.
Kilichopelekea roma kuanguka ndio kinaikumba sasa usa
Ushoga
Currency manipulation
Empire overextenstion
Wars


Sent from my LG-M200 using JamiiForums mobile app
 
Jambo usilolijua EU ni ushirika au shirikisho la kiuchumi.

Siyo mambo ya kijeshi na kisiasa.
NATO ndiyo military alliance. Members wa EU hawana mandate ya kumshambulia kijeshi yeyote aliyemshambulia member mwenzao.
Ila member wa wa NATO kwa mujibu wa makubaliano yao anawajibika kuingilia kati kumsaidia member mwenzie wa NATO kijeshi.

Maneno machache yenye ujumbe mzito. Usiweke ushabiki wa kisiasa kwenye mambo makubwa usiyo yajuwa.
 
Punguza mapenzi na Russia! Russia anaweza kuipiga Ulaya nzima kweli?? Ana nguvu gani hizo?? Okay tusema sawa,anaweza ipiga! Then unadhan baada ya vita hii Russia ya sasa hivi itakua na nguvu gani tena?? Hebu weka mahaba pembeni! Generals waliopo huko Moscow, London, Pentagon na Tel Aviv ndiyo wawe hawajui,ila wewe mmatumbi wa huko Utete Lufiji ndiyo uwe unajua sana! Hapana,tusiwe brainwashed namna hiyo! Asante
Kama nato wanataka kupigana na russia ni vema wawe na supply ya kutosha ya diaper sab haitachukua muda kugundua kuwa kumbe russia sio libya au iraq pale icbm zitakapo anza kusherehesha anga la nato hasa nchi za ulaya

Sent from my LG-M200 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom