Haya mahisa na maUTT yenu Kuna vilio vinakuja, watu hawataamini

Umeongea vizuri sana mkuu. UTT sio fursa ya kutajirikia...bali kutunza tu pesa. Kuliko uweke hela bank ikaambatana na makato. Kwann husiweke tu UTT ambapo maybe in 1 year utaikuta oesa yako kama ilivyo, au japo imeongezeka kidogo. The same na kwenye hisa, japo kwenye hisa kama bei za soko zitashuka...basi utakuwa umengia hasara pia kidogo.

All in all, hisa na UTT ni kwa ajili ya mtu ambaye maybe anapesa zake za akiba ..na hataki kutakerisk kubwa kwenye kuwekeza kitu, maybe anaiweka pesa yake itulie kama ilivyo
 
Kwahiyo mkuu unaweka mil 10 ili upate laki 1 kwa mwezi au upate mil 1 kwa mwaka au usubiri miaka kadhaa ambayo bado hairudishi investment ulioweka tofauti na miaka 10 wewe hiyo unaona imekaa sawa hasa kwa kijana mwenye nguvu?
 
Sifa ya mtu yeyote mwenye akili ni pamoja na kuwa na wasiwasi(Tahadhari).

Ingawa umetumia lugha ya hovyo lakini kichwani kwako 'zimo'. Usipuuzwe!
 
Kwahiyo mkuu unaweka mil 10 ili upate laki 1 kwa mwezi au upate mil 1 kwa mwaka au usubiri miaka kadhaa ambayo bado hairudishi investment ulioweka tofauti na miaka 10 wewe hiyo unaona imekaa sawa hasa kwa kijana mwenye nguvu?
Mimi nimeshangaa huyo anayesema watu wanatafuta utajiri kwa kuweka pesa UTT ndipo nikamuuliza 12% inatosha kutajirisha?
 
Uwekezaji gani unakuhakikishia safety angalau 70% na inatoa return 30% ya Uwekezaji wako??
 
Kwahiyo mkuu unaweka mil 10 ili upate laki 1 kwa mwezi au upate mil 1 kwa mwaka au usubiri miaka kadhaa ambayo bado hairudishi investment ulioweka tofauti na miaka 10 wewe hiyo unaona imekaa sawa hasa kwa kijana mwenye nguvu?
Huyo kijana mwenye nguvu akiweka huko pesa, anakutegema wewe kwa chakula? Anakuja kwako kuomba mavazi na malazi?
 
Uwekezaji gani unakuhakikishia safety angalau 70% na inatoa return 30% ya Uwekezaji wako??
Hicho kitu akipo ,, asilimia 30% lazima uwe kwenye risk na sio safety unayoitaka. Risk ndio maendeleo yenyewe. Yani ufanye biashara ya milion 10 upate faida milion 3 kwa mwezi halafu risk isiwepo ? Hiyo biashara haipo 😂
 
Kwahiyo mkuu unaweka mil 10 ili upate laki 1 kwa mwezi au upate mil 1 kwa mwaka au usubiri miaka kadhaa ambayo bado hairudishi investment ulioweka tofauti na miaka 10 wewe hiyo unaona imekaa sawa hasa kwa kijana mwenye nguvu?
Miaka inavyoenda kiasi cha faida kinaongezeka. Waza mtu anayeweka milioni 100. Ndani ya miaka 6 hiyo hela inakua double. Utt na masoko sio kitu cha kubeza. Wabongo tuache kutaka faida ya chapchap
 
Hicho kitu akipo ,, asilimia 30% lazima uwe kwenye risk na sio safety unayoitaka. Risk ndio maendeleo yenyewe. Yani ufanye biashara ya milion 10 upate faida milion 3 kwa mwezi halafu risk isiwepo ? Hiyo biashara haipo 😂
Ndio ajue kua wanaoweka hela UTT sio wajinga..me UTT nimeweka hela hili inilipie kodi ya nyumba tu..

Fikiria unaweka mahala million 50 ambayo huna kazi nayo,ipo safe 99.99,ukiitaka unaichukua muda wowote,but ilipo kila mwezi inakuingizia 558,000/= tsh ambayo unalipa kodi..

Huku una biashara or kazi nyingine inakuingizia kipato,hiyo sio good deal??.

financial illiteracy Tatizo kubwa kwa watanzania ndio maana watu wengi wanazeeka masikini,hii mada kwa karne hii ya utandawazi haikutakiwa kujadiliwa kwa mlengo huu...
 
Very good deal. Achana na hizo pesa ndefu hivyo Mimi mwaka mzima napata 1.8 kwa ajili ya kusaidia ada za watoto. Principal yangu ipo pale pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…